MAGONJWA YA KUKU, DALILI, CHANJO NA TIBA

Leo napenda nikuonyeshe baadhi ya magonjwa ambayo huwapata kuku mara kwa mara , dalili, chanjo na tiba.
hivyo kua nami ili kupata elimu hiyo

UTANGULIZI 
Magonjwa husababishwa na vitu vifuato
  • virusi
  • bacteria
  • protozoa
  • upungufu wa viini lishe 
MDONDO/NEW CASTLE 
Huu ni ugonjwa ambao unaweza kuwapata kuku wadogo na wakubwa na pia husababishwa na virusi


DALILI
  • Kuku kuacha kula
  • kuharisha
  • kutoa machozi
  • kutoa kamasi
  • kupumua kwa shida
  • wengine upooza kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
TIBA NA KINGA
  • Ugonjwa huu hauna tiba ila unaweza kukinga kwa kumpa chanjo kila baada ya miezi mitatu
GUMBORO
Ni ugonjwa ambao unasababishwa na virusi pia , virusi usambazwa kutoka kwa kuku alie athilika kupitia kinyesi

DALILI
  • Dalili huanza kuonekana kuanzia wiki ya 6 hadi 18
  • kuku uharisha majimaji
  • maambukizi yanaweza kufikia 100%
TIBA
Pia ugonjwa huu hauna tiba ila kuku anatakiwa kupewa chanjo ya gumboro siku ya 14

NDUI YA KUKU/FOWL POX
Pia ugonjwa huu husababishwa na virusi ba uhasiri sana vifaranga  wanaokua na hujitokeza zaidi wakati wa mvua

DALILI
Kuku hua na vipele kama nundu kichwani
pia kuku huzoofika
hupoteza hamu ya kula

CHANJO NA TIBA
Chanjo itolewe kabla ya msimu wa mvua kubwa kuanza'
dawa za kuua vimelea kama joto ya vidonda  hupunguza makali ya vidonda

KOKSIDIOSIS
Ni ugonjwa wa vimelea na uhathiri sana kuku wakiwa na umri mdogo  kuanzia umri wa wiki 1

DALILI
  • Kuku kudhoofika
  • manyoya huvulugika
  • kuku kuzubaaa
  • kinyesi hua kahawia hau kujaa damu
  • kuku kua kama amevaa koti
KINGA NA TIBA
  • Kokisidiosis hutibiwa kwa dawa maalum kama  AMPROLLIUM au SULFA
  • dawa huzuia kuitokeza kwa ugonjwa pindi inapo tumika ipasavyo.
MINYOO
Minyoo siku zote hukaa tumboni  na inamadhala kama yafuatayo
  • kupunguza kutaga
  • kuharisha
  • kupoteza uzito
TIBA
Unaweza kuwatibu kwa kutumia dawa kama vile PIPERAZINE 
VIROBOTO UTITILI
Viroboto hukaa katika sehemu tofauti mbali mbali za mwili hasa ushambuli sehemu za kichwa 
TIBA NA KINGA
Tumia dawa za kuua wadudu kama AKHERI POWDER au SEVIN DUST  wamwagie kuku pamoja na maeneo wanayo ishi
pia unaweza kutumia PROMECTIN - ORAL 100ML

No comments