UTANGULIZI
Katani ni moja kati ya zao la biashara
Jina la kisanyansi; Agave sisalana
Jina maalufu; sisal au katani
Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine nyingi,kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius. na nizao ambalo hutumika sana kutengenezea bidhaa nyingi.
HALI YA HEWA
joto lidi; katani hukua vizuri katika maeneo ya kisubtropikia, yaan hukua vizuri kwenye maeneo ya joto yeje joto kati ya 10-32 oC na joto ya juu zaidi inapidi kua 30 hadi 40oC na joto ya hali ya chini zaidi ni 5oC.
Mvua; pia mvua huchukua nafasi muhimu katika kilimo cha katani zao hili huzaa vyema zaidi katika maeneo yenye mvua 500mm na zaidi kwa mwaka na wastani wa mvua 600mm hadi 1500mm na pia huweza kukua kwenye maeneo yenye mvua chini ya hapo.
Udongo; zao la katani halibagui sana udongo lakin hukua vyema kweye maeneo ambayo yana unyevu wa kutosha na aina nyingi za udongo isipo kua udongo mfinyanzi na pH 4.0 hadi 6.0 ni muhimu.
MBEGU
Katani hupandwa kwa kutumia bulbils na suckers
suckers; ni vile ambavyo vinakua karibu na mmea na utokana na matokezi (buds) na vinaweza kuchukuliwa na kupandwa moja kwa moja shambani
bulbils; pale katani inapokua huzaa maua katika mlingoti wake, hivi huchukuliwa na kupandwa katika kitalu na watu wengi hupenda kuoanda hivi kwa kua hua na sifa kamili kama ya mmea ambao ni mzazi
KUANDAA SHAMBA
Mfumo unao itajika ni ule wa mistali miwili yaan double rows.
hivyo andaa shamba kwa kulipalilia vizuri na kuondo taka zote.
KUPANDA
Kama nilivyo sema hawali bulbils lazima zipandwae kweye kitalu kwanza vinapandwa 10cm x 10cm na hukaa kwenye kitalu kwa mda wa miezi 6 na baada ya hapo huamisiwa tena kwenye kitalu kikubwa ambapo hupandwa kwa 30cm x 30cm ,
Na baada ya miezi 12 hadi 18 mimea hua tayari sasa kwakupandwa katika shamba kubwa na nafasi kati ya mistari hua ni 1 hadi 1.5 m na 4 m na kina cha kupanda mmea hua ni 3cm katika kuhamishia shambani mizizi midogo pembeni ya mmea hukatwa na majani ya chini yanaweza kuondolewa.
MBOLEA
Mala nyingi katani hua haiitaji sana mbolea kwakua hua na urafiki na mazingira pale inapo pandwa kwenye eneo jipya , lakini inapo pandwa kwenye eneo ambalo limekwishatumika mbolea huitajika , unaweza kutumia UREA, lime ammonium nitrate (LAN) na superphosphate.
UMWAGILIAJI
Kilimo cha katani hakiitaji umwagiliaji kwa kua huimili ukame japo kua katika kuprocess maji hutumika sana.
UPALILIAJI
Kupalilia ni muhimu sana ndani ya miaka miwili ya mwanzo yaani miaka 2 hadi 3 ni vyema sana kupalilia baada ya kuamishia katika shamba kubwa unaweza kutumia jembe la mkono au hata kemikali, unaweza kuacha magugu kukua wakati wa mvua na ukaya palilia wakati mvua zimeisha
MAGONJWA NA WADUDU WAALIBIFU
WADUDU
- Weevil wa katani
- nguruwe
- nyani na sokwe
MAGONJWA
- Madoa ya majani
- kuoza kwa mringoti
KUVUNA
Kuvunwa kwa mazao inategemea na eneo, kiasi cha mvua udongo na hali ya hewa,m lakini kwa kawaida katani huvunwa kwa mara ya kwanza kati ya miaka 3 hadi 4 baada ya kupanda.
mimea hua na majani 120 hadi 125 ambayo hua na urefu wa 60 cm unatakiwa kuvuna majani ambayo tu yaapo tayari .
majani hua tayari pale rangi inapo badilika kutoka brown iliyo koza hadi kua brown iliyo pauka na majani huvuna kwa interverl kwa maana hiyo unaweza kuvuna majani 25 kwa kila mmea kwa mwaka.
ASANTE............
0 Comments