MUONGOZO WA KILIMO CHA MAHINDI KIBIASHARA
Mahindi ni moja kati ya zao linalo limwa kwa wingi sana hapa Tanzania, hii ni kutokana na sababu kwamba mahindi ni moja kati ya zao kuu la chakula hivyo uhitaji wake wa kila siku ni mkubwa lakini mahindi pia husitawi katika maeneo na mikoa karibia yote hapa Tanzania, licha kutofautiana misimu ya kulima hii ni kutokana na kutofautiana kwa mazigira. Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni.
Maandalizi ya shamba.
shamba liandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Na Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba hivyo mkulima unatakiwa kuandaa shamba kuligana na uwezo wako lakini pia ukubwa washamba.
- Jembe la mkono – wengi wanatumia
- Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
- Power tillers
- Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, hivyo kwa ufanisi zaidi tunashauri uweze kutumia trekta, power tiller au jembe la kukokotwa na ngómbe.
Uchaguzi wa Mbegu
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
- Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo
- Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili – composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).
Tunashauri uweze kumuuliza afisa ugani katika eneo lako au duka la pembejeo za kilimo katika eneo lako, ili kufahamu mbegu inayostawi na kufanya vizuri katika eneo lako. Kwani mbegu hutofautiana kuligana na sababu tajwa hapa chini.
- Mwinuko kutoka usawa wa bahari
- Kiasi cha mvua katika eneo husika
- Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mfano wa mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615,WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115 kutoka ARI ILONGA na nyingine nyingi.
Upandaji wa mahindi
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.
Kwa mavuno mengi ni lazima mkulima uzingatie kupanda mimea yako kwa nafasi, nafasi za kupanda hutofautiana kutokana na sababu mbalimbali za kitaalamu, lakini tajwa hapa chini ni nafasi tunazoshauri mkulima atumie kupanda.
- Kwa nafasi ya 90 sm X 30 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 25 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 50 sm, panda mbegu mbili na uweke vizibo viwili vya mbolea
Matumizi ya Mbolea.
Mbolea za kupandia zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia.
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha mifuko 2 ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari). Ikiwa mbolea ya minjingu phosphate itatumika basi mifuko mitatu itatosa kwa hekta mfuko mmoja na nusu kwa ekari). Na endapo utaamua kuitumia mbolea ya minjingu mazao basi tumia mifuko minne na nusu kwenye hekta moja au mifuko miwili kwa ekari moja.
Mbolea za kukuzia ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:
- UREA: 46% N
- Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
- Sulphate of Ammonia, SA: 21%
Wakulima wengi hutumia UREA katika kukuziakutokana na urahisi wake katika kupatikana, lakini pia bei yake ipo chini kidogo na hatapia watu wengi wanauzoefu wa kutumia UREA. Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa.
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium. Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi hiki cha mbolea:
- UREA: kizibo kimoja cha soda
- CAN: vizibo viwili vya soda, na
- SA: kizibo kimoja cha sodaS
KUPATA MUONGOZO WA UFUGAJI BORA WA NGURUWE BOFYA HAPA
PALIZI
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini lakini pia yanaweza kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno.
Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono (yaani) kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (herbicides) hasa 2-4D.
Ni muhimu shamba lako lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.
UVUNAJI
Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa. Mahindi hutofautiana katika siku na kiasi cha kuvuna kulingana na aina ya mbegu unayotumia.Kama unatumia mbegu za muda mufupi huwezakuchukua hadi siku 75 -120 lakini pia Kama unatumia mbegu za muda mrefu inaweza kuzidi hapo.Kwa makuadilio kitaaalamu mkulima hutakiwa kuvuna kiasi cha gunia 15- 30 katia shamba la ekari moja.
KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI
i) Maize streak virus
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies).
ii) Smut (Fugwe)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo kamili.
iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi)
Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili kuoza.
Wadudu Na Wanyama Wanaoshambulia Mahindi
a) Viwavi Jeshi
Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina. Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo;-
- Kuondoa vichaka karibu na shamba
- Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
- Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1L
b) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer)
Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
- Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
- Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.
- Njia za kudhibiti zinazotumika
- Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde km vile maharagwe
- Kung’oa mahindi yaliyoshambuliwa
- Sumu za asili mwarobaini
- Sumu za viwandani km vile Karate. pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
c) Cutworms (Vikata Shina)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili.
d) Wanyama waharibifu
Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.
Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.
KUPATA MIONGOZO WA KILIMO BORA CHOCHOTE NA MIONGOZO YA UFUGAJI WASILIANA NASI WAKATI WOTE. 0764148221
Post a Comment