UFUGAJI WA MENDE UTAJIRI UNAOPUUZWA

 Na Imani Lubaba

    Picha na Nicky Maruchu
 

Kipindi mende anachukuliwa kua mdudu ambae ni adui mkubwa sana wa binadamu kutokana na imani kwamba mdudu huyo ni mchafu, watu wengine wamemtumia mende kama fursa kwao Inawezakua inashangaza lakini ukweli ni kwamba mende ni mdudu mwenye faida nyingi sana, lakini pia anaweza kua biashara ambayo inaweza kubadili maisha yako. Team ya TANZANIA NA KILIMO na RUBABA TV tulipata fursa ya kuweza kutembelea moja kati ya wafugaji hao wa mende, kwa lengo la kukuwezesha wewe msomaji na mtazamaji wetu kuweza kujifunza na kufahamu fursa na utajiri ulio jificha ndani ya mende.

Mfugaji huyo Maarufu kama Mama Mende aliweza kutueleze vitu vingi kumhusu mende ambavyo hata sisi binafsi ilikua ni ngumu sana kufahamu. Mfano unafahamu kwamba kinyesi cha mende kinaweza kutumika kama tiba lakini pia mbolea nzuri sana.. Inashangaza!! Mende pia anaweza kutumika kama kitoeo kizuri sana  kwa binadamu na wanyama  chenye protini cha ajabu zaidi mama huyu amekua akitumia kinyesi icho kama majani ya chai na amesema kimeweza kusaidia kumponya magonjwa.

Tulizungumza mengi sana ambayo yanafurahisha na kushangaza sana kumuhusu mende, na unaweza kutazama na kujifunza zaidi jinsi mende anavyoweza kubadilika na kua biashara kwa kutazama video.


 

KUPATA MAFUNZO NA MUONGOZO WA UFUGAJI WA NGURUWE KIBIASHARA WASILIANA NASI.

Email: rubabaimani@gmail.com I Phone: +255 764 148221

No comments