Mpunga hulimwa sana hapa Tanzania na endapo mkulima akifata ushauri wakitaalamu kwa hakika ataweza kupata mavuno mengi. Kupitia muongozo huu utaweza kufahamu hatua kwa hatua jinsi gani unaweza kufanya kilimo hiki kwa tija.
KUTAYARISHA SHAMBA.
Hii ni hatua ya kwanza na muhimu sana, Kusanya taka na mabaki ya mazao na kuyazika shambani. Yakioza hua ni mbolea nzuri sana hivyo usitoe mabaki ya mazao acha shambani na yaoze. Lainisha na sawazisha shamba vizuri kabla ya mvua kwa wakulima wanaotegemea mvua, ili kuwezesha maji kusambaa vizuri hivyo kuleta unyevu unaohitajika.
v Zingatia kusafisha shamba mapema angalau mwezi mmoja kabla kuwezesha magugu kukauka na kufa mapema.
Baada ya shamba kusafishwa kinachotakiwa kufanyika ni kusawazisha shamba, hii husaidia kuhakikisha mbolea na maji yanatawanyika shambani kwa uwiano. Unaweza kufahamu miinUko na mabonde katika shamba lako wakati wa kusawazisha, kwa kuruhusu maji kidogo kuingia shambani.
Kutengeneza kingo shambani ni swala la muhimu na lisilo kwepeka, Kwaani husaidia kuhifadhi maji shambani. Hakikisha unaweka sehemu ya kuruhusu maji kuingia na kutoka shambani, ili kuweza kusaidia katika kudhibiti kuwe na kiasi stahiki cha maji shambani.
Kiasi cha vipimo vya kingo kinacho pendekezwa
Upana Wa juu |
Sm 35 hadi 45 |
Kimo |
Sm 40 hadi 50 |
Kitako |
Sm 135 hadi 165 |
Hatua kwa Hatua namna sahihi ya kutengeneza jaruba la Mpunga
1. Tumia futi au kamba ya mkonge kwa kuweka alama katika mipaka ya jaruba
2. Tumia jembe au chepe kukusanya tabaka la juu la udongo, kisha weka katikati ya jaruba lako.
3. Udongo wa chini utakusanya na kutumiwa kutengeneza kingo za jaruba lako na hakikisha zimeshindiliwa vizuri
4. Udongo wa tabaka la chini uliobakia usawazishwe na kushindiliwa vizuri.
5. Sambaza udongo wa tabaka la juu na hakikisha kila sehemu ya jaruba imesawazishwa na kufunikwa na udongo huo, unaweza kutumia njia ya kuweka maji kuhakikisha unasawazisha kwa usahihi.
UCHAGUZI WA MBEGU NA UPANDAJI
Matumizi ya mbegu bora ni swala la msingi sana katika upatikanaji wa mavuno mengi,kuna makundi mawili ya mbegu ambapo mkulima anaweza kuchangua.
Mbegu za Asili: Mbegu hizi hatushauri sana kwani nizamuda mrefu sana, zinauwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na rahisi sana kuanguka.
Mbegu zilizoboreshwa: Zimeboreshwa kutoka mbegu za asiri. Mfano Katrin, IR54, TXD88, TXD85 na TXD306. Hakikisha unafanya utafiti wa mbegu ambayo inafanya vizuri katika eneo lako kwani kila siku mbegu huboreshwa. Hivyo hizo nilizo zitaja hapo juu ni mfano unaweza kua huru kuulizia na kufanya utafiti wa kina kufahamu ipi ni mbegu bora zaidi.
Jinsi ya Kupanda
Kupanda mbegu moja kwa moja, katika njia hii mbegu hupanda moja kwa moja shambani kwa kutumia mistari au bila kutumia mistari (broadcasting). Mkulima ambae hutumia njia hii anashauriwa kutumia njia ya mistari kwani hupunguza matumizi ya mbegu lakini pia kuhakikisha mavuno.
Kupandikiza, mbegu hupandwa katika kitalu na kuhamishiwa shambani siku ya 18 had 21 kwa mbegu za muda mfupi na 21 hadi 35 kwa mbegu za muda mrefu baada ya kuota. Unashauriwa kusoma maelezo ya mbegu na maelekezo yake ya kupanda kabla. Njia hii ndio njia ambayo inashauri kutumiwa kitaalamu,hivyo mkulima tumia njia hii kwa uhakika zaidi.
Jinsi ya kutayarisha na kutunza kitalu.
Kitalu kiandaliwe katika eneo lenye rutuba na maji ya kutosha lakini pia kuwe na ulinzi. Zingatia kutengeneza kitalu karibu na shamba ili kurahisha wakati wa kuhamishia shambani. Matuta 40 yenye upana wa mita 1 na urefu wa mita 10 hutosha kabisa kupata miche itakayo toshereza shamba lenye ukubwa wa hekari moja. Hakikisha udongo unakua na unyevu wa kutosha kwa kipindi cha wiki moja kabla ya mbegu kutoka, na kidogo kidogo ongeza kiasi cha maji kutegemea urefu wa miche.
Ø Kupanda mbegu moja kwa moja tumia kilo 60 au debe 4 kwa hekta (debe 1.5 kwa ekari) kwa mbegu ndefu, kilo 80 au debe 5.5 kwa hekta( debe 2 kwa ekari) kwa mbegu za muda mfupi. Hii ni kwa watu wanaopanda kwa njia ya kumwaga shambani.
Ø Kwa wakulima wanaopandikiza kiasi cha kilo 35-40 hutoa miche ya kutosha kuweza kupandikiza shamba lenye ukubwa wa hekta moja.
upandikizaji
Wakati wa kuandaa miche ya kupandikiza hakikisha inagólewa na kupandikizwa siku hiyo hiyo na hakikisha unamwagilizia maji ya kutosha kabla ya kungóa kuepusha kukata mizizi vibaya. Hakikisha miche inayochaguliwa ni ile yenye afya na kimo kimoja na hakikisha inangólewa kwa umakini na kuwekwa katika beseni lenye maji kuepusha miche kunyauka.
Miche 2 hadi 3 ipandikizwe kwenye kila shimo lenye kina cha sm 3 kwa nafasi ya sm 20 kwa 20 kati ya miche na miche na mistari kwa mstari kwa kutumia kamba maalamu iliyotengenezwa kwa vipimo, katika maeneo yasiyo na rutuba ya kutosha unaweza kuongeza nafasi hadi kufikia sm30 x sm30.
v Miche yote iliyobaki ifungwe vizuri na kupandikizwa sehemu moja kwaajili ya kurudia kupanda kwa maeneo ambayo mbegu hazitaota na hakikisha zoezi hili lisizidi siku 10.
UTUNZAJI WA SHAMBA
Mpunga hupita hatua tatu kubwa na muhimu kuanzia siku miche inachipua hadi kufikia hatua ya kukomaa. Mpunga hutofautiana katika urefu wa awamu ya kukua hii nikutokana na tofauti za mbegu, lakini awamu za uzazi na ukomaaji hua sawa bila kujali umetumia mbegu gani.
Kupanda hadi mche kufikia hatua ya kuhamishiwa shambani |
Mche kupandikizwa na kushika vizuri |
Machipukizi kuchipua |
Kurefuka kwa pingili |
Mmea kuanza kutoa suke |
Kuchanua |
Kujaza punje na kukomaa |
AWAMU YA UKUAJI SIKU 35-55 KWA MBEGU ZA MUDA MFUPI SIKU 55-75 KWA MBEGU ZA AINA YA KATI SIKU 75-95 KWA MBEGU ZA MUDA MREFU |
AWAMU YA UZAZI
SIKU 30 – 35 |
AWAMU YA KUKOMAA SIKU 30-35 |
Ø Mpunga husitawi vizuri katika maji mengi, hivyo hakikisha katika majaruba kunakua na maji ya kutosha. Baada yay a upandikizaji kina cha maji lazima kiwe kiasi cha sm3 na ongeza hatua kwa hatua hadi kufikia sm5-10 na kukiacha kiasi icho hadi siku 10 kabla ya kuvuna.
Udhibiti wa Magugu shambani.
Magugu huanza kudhibitiwa mapema kwa kuanza kuandaa shamba lako mapema sana. Na unaweza kuyaacha magugu yaote kabla ya msimu. Unaweza kutumia njia mbalimbali katika kudhbiti magugu, inategemea na uwezo pamoja na ukubwa wa shamba lako.
Ø Kwa kutumia jembe la mkono
Ø Kwa kutumia dhana za kupalilia
Ø Kwa kutumia viuagugu
Kwa wakulima wanaotumia viuagugu dawa mifani ya dawa tunazopendekeza ni
2-4D , solito, stam, nominee gold |
Kwa kuua magugu ya aina ya mbogamboga na ndano yani yasiyo jamii ya nyasi |
Servian, tiller gold, amine |
Huwekwa kabla yamiche kuchepua |
Roundup, gugusate, paraquat na gramoxone |
Huua magugu ain azote yaani hazichagui |
KUPATA MUONGOZO MZIMA WA KILIMO BORA CHA MPUNGA WASILIANA NASI
+255764148221 Email: Rubabaimani@gmail.com
Ø Hakikisha unafata masharti na maelekezo yote wakati wa kutumia viuagugu na hakikisha unavaavifaa kwaajiri ya kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na hizo kemikali.
L
K
0 Comments