UFUGAJI BORA WA NGURUWE

Habari mpenzi ,msomaji leo nataka nikuoneshe vitumuhimu katika ufugaji wa nguruwe kwa kua ni moja kati ya wanyama wenye faida sana.




“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata nguruwe  bora.
 Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.

Ufugaji
Nguruwe hawa itaji mtaji mkubwa sana ili kuwafuga,hata wakulima wadogo  wanaweza kumudu kufuga nguruwe kwa kua huitaji mtaji mkubwa sana ili kuwa fuga na pia huleta faida kubwa pale wanapo fiki hatua ya kuya wakubwa

BANDA
Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa sakafu ya zege au ukachanganya mchanga na siment unaweza chagua kulingana na uwezo wako
. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka nguruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.

CHAKULA
Uzuri wa nguruwe hua hawana gharama kubwa sana katika kuwalisha. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali,pumba.napia unaweza kuwalisha na mashudu aina ya Wheat Poland,au mabaki ya chakula chabinadamu.japo kua kunakua na aina maalum kwa ajili ya chakula kwa ajili ambacho unaweza kuwalisha kilo 1-2 kwa siku


KUPANDISWA
Nguruwe wakike yan sow ka lugha ya kitaalam anapandishwa pale anapo ingi kwenye joto kama mnyama yoyote yule.
na unaweza kujua kama ameingia kwenye joto pale anapokua msumbufu/lestless, anakua anawapanda wenzae,uteute mweupe unatoka kwenye uke wake,na pia vulva inabadilika nakua nyekundu.

KUZAA
Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114 yan miez mitatu na na siku kadhaa.
 Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 6 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.


JINSI YA KUWATUNZA
Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula na maji ya kutosha cha kutosha na ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku2 au3 toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.


BAADHI YA MAGONJWA YA NGURUWE
Kila siku magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama yanatokea.lakinm kunamagonjwa ambayo kama mfugaji lazima uyajue kwakua ndio yanayo jitokeza.


UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO
Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe.
Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.


Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja

Dalili,dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika
Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.


HOMA YA NGURUWE(SWINE FEVER)
Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa

Dalili, nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu.
Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.


Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine kwa  kua huu ni viral  disease


UGONJWA WA MAPAFU (PNEUMONIA)
Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe,Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Dalili, nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana
Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.


KIMETA(ANTHRAX)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.


Muhimu:nguruwe alie kufa kwa kimeta usimshkew kabsa kwa sababu hata binadamu anaupata huu ugonjwa, chimba shimo mbali na watu  mwagia mafuta ya taa ndani ya hilo shimo kisha fukia mzoga.,
dalili ya nguruwe alie kufa kwa kimeta damu hua aigandi na pia hata nzi hawasogei kwenye mzoga kwa hiyo kua makini.


AINA ZA NGURUWE

Largewhite

characteristics
  • hii ndio aina kubwa kabsa kuliko aina zote tatu
  • anakua na mwili mweupe pote
  • masikio yake yamesimama wima
  • ni mama mzuri
  • anakua na mdomo mbinuko
landress
characteristics
  • anakua mweupe pia au anaweza kua na mabaka meusi
  • ni  mkubwa kuasi
  • masikio yake yamelala
saddleback

characteristics
  • anakua mweusi ila anakua na mkanda mweupe shingoni 
  • pia ni mpole
  • anamasikio ya kulala
  • anakua mkubwa kiasi

natumaini umejifunza kitu kwa elimu zaidi usisite kunitafuta
rubabaimani@gmail.com
+255764148221
+255653882567 

je ulipitwa na somo la UFUGAJI BORA WA SAMAKI? bofya hapa 

Post a Comment

33 Comments

Anonymous said…
asante sana kaka kwa elimu uliyotoa nimepiga hatua
Unknown said…
thanx for knowledge
Denis Desdery said…
Nimejifunza mengi sana
Salute kwako mkuu
Rubaba Imani said…
asante kwa kunitia moyo endelea kua nami kujua meng zaid
bernard said…
vipi kuhusu soko na bei
Rubaba Imani said…
soko na bei la nguruwe hutegemea na sehem husika.
ila kwa ufupi tu nguruwe ni wanyama wenye faida na soko sana
unaweza kupata soko kwa kuwachinja na kuwauza au kuweka ubia na maoteli wanakua wanachukua nyama kwako.
kuuza watoto wake,kuuza kwa watu pia
hiyo ni mifano ambayo unaweza kupata soko pia.
Marvin pm said…
Karibu katika group LA whatsapp tushirikiane ktk kutatua changamoto mbalimbali za ufugaji WA nguruwe....pig keeping TZ.... Txt me whatsapp namba 0712694084

Marvin pm said…
Karibu katika group LA whatsapp La PIG KEEPING TZ Tushirikiane kutatua changamoto pamoja
Click link kujiunga
https://chat.whatsapp.com/5uHk9ZENTuUG3LhN3tw7s0
Rubaba Imani said…
asante nakuahidi tutakua pamoja
Unknown said…
Mkuu hiyo link haifunguki, add me kwa 0677175360, please
Unknown said…
0719172072 ni add
Unknown said…
Marimba niunge kwenye group 0767258869

Nguvila the son said…
Uko vizuri sana. I wish nijoin darasa lako.
Unknown said…
uko vizuri sana ndugu.natamani ningekuwa na hiyo elimu .natamani sana kufuga nguruwe,sijaanza bado lakini nitafuga sio muda mrefu,ila nahitaji kwanza elimu ya kutosha .
Rubaba Imani said…
Karibu sana kujifunza mengi
Unknown said…
Mimi naitaji begun kubwa ambayoinaongezekauzito halaka . mm nafuganguruwe ila hawana umbilekubwaa nawakati akinyonyesha hukonda nifanyeje?
Rubaba Imani said…
Kuhusu mbegu tunaweza kuwasiliana 0764148221,
Lakin pia ili nguruwe asikonde wakati wa kunyonyesha jitahd kumpa chakula Bora na kinachotosha, pia zingatia kumpa maji ya kutosha
Unknown said…
Plz niadd kwenye group 0677496617
Jafeti said…
Add me please 0745142831
Aidan said…
Naomba uniunganishe na grupu la whatsapp la ufugaji nguruwe na mimi pia nijifunze na nitekeleze.
Aidan said…
Niadd kwa 0622589315
teleni said…
add me on WhatsApp 0743557016
ili nijifunze zaid
Unknown said…
Mko vizuri, niunge kwenye group 0659821393
Unknown said…
0713400778
nia add namimi
Anonymous said…
Nimesoma lakini je sisi wsmikoani munaweza kutumia mbegu maana tunapatashina sana hasa yanguluwe large white na land race Sasa naomba Muni add kwenye group la Whatsapp nb, 0788612111
kino said…
Thanks nimegain alot,as long ndio nategemea kuanza project so nauliza interval ya umri wa kununua mbegu na pia nategemea kama nianze na kama piece 20 naomba kujua ratio ya jike na dume iweje ili pia iwe rahisi kuwamanage na uzao wao.

Ikiwezekana na bei kwa kila umri ambao utanishairi nianze nao.
kino said…
Thanks nimegain alot,as long ndio nategemea kuanza project so nauliza interval ya umri wa kununua mbegu na pia nategemea kama nianze na kama piece 20 naomba kujua ratio ya jike na dume iweje ili pia iwe rahisi kuwamanage na uzao wao.

Ikiwezekana na bei kwa kila umri ambao utanishairi nianze nao.
0716830953/0783378529
kino said…
Thanks nimegain alot,as long ndio nategemea kuanza project, so nauliza interval ya umri wa hizo mbegu (piglets) maana nategemea kama nianze na piece 20, naomba kujua ratio ya jike na dume iweje ili pia iwe rahisi kuwamanage uzao wao.
Na unanishairi mbegu ipi bora zaidi inayohomili maradhi na kujua haraka pia uzito mzuri.
Ikiwezekana na bei kwa kila umri ambao utanishauri nianze nao.
0716830953/0783378529