UFUGAJI BORA WA NGURUWE
Nguruwe hawa itaji mtaji mkubwa sana ili kuwafuga,hata wakulima wadogo wanaweza kumudu kufuga nguruwe kwa kua huitaji mtaji mkubwa sana ili kuwa fuga na pia huleta faida kubwa pale wanapo fiki hatua ya kuya wakubwa
BANDA
Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa sakafu ya zege au ukachanganya mchanga na siment unaweza chagua kulingana na uwezo wako
CHAKULA
Uzuri wa nguruwe hua hawana gharama kubwa sana katika kuwalisha. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali,pumba.napia unaweza kuwalisha na mashudu aina ya Wheat Poland,au mabaki ya chakula chabinadamu.japo kua kunakua na aina maalum kwa ajili ya chakula kwa ajili ambacho unaweza kuwalisha kilo 1-2 kwa siku
KUPANDISWA
Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114 yan miez mitatu na na siku kadhaa.
JINSI YA KUWATUNZA
Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula na maji ya kutosha cha kutosha na ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku2 au3 toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.
BAADHI YA MAGONJWA YA NGURUWE
Kila siku magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama yanatokea.lakinm kunamagonjwa ambayo kama mfugaji lazima uyajue kwakua ndio yanayo jitokeza.
UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO
Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe.
Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja
Dalili,dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika
HOMA YA NGURUWE(SWINE FEVER)
Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa
Dalili, nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu.
UGONJWA WA MAPAFU (PNEUMONIA)
Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe,Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.
Dalili, nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana
KIMETA(ANTHRAX)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi
Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.
Muhimu:nguruwe alie kufa kwa kimeta usimshkew kabsa kwa sababu hata binadamu anaupata huu ugonjwa, chimba shimo mbali na watu mwagia mafuta ya taa ndani ya hilo shimo kisha fukia mzoga.,
AINA ZA NGURUWE
characteristics
- hii ndio aina kubwa kabsa kuliko aina zote tatu
- anakua na mwili mweupe pote
- masikio yake yamesimama wima
- ni mama mzuri
- anakua na mdomo mbinuko
- anakua mweupe pia au anaweza kua na mabaka meusi
- ni mkubwa kuasi
- masikio yake yamelala
characteristics
- anakua mweusi ila anakua na mkanda mweupe shingoni
- pia ni mpole
- anamasikio ya kulala
- anakua mkubwa kiasi
natumaini umejifunza kitu kwa elimu zaidi usisite kunitafuta
rubabaimani@gmail.com
+255764148221
+255653882567
je ulipitwa na somo la UFUGAJI BORA WA SAMAKI? bofya hapa
Post a Comment