KILIMO BORA CHA TANGAWIZI



UTANGULIZI
 Tangawizi ni moja kati ya mazao ya iana ya tungulu(rhizome).
na kwa jina la kitaalamu huitwa Zingiber officinale. Asili yake ni Asia yaan china, india na  japan na baadaye kusambaa katika mabara mengine kama amerika kusini na Africa.kwa hapa Tanzania tangawizi hustawi vizuri katika mikoa ya TANGA, KILIMANJARO,MBEYA, KIGOMA, MOROGORO NA PWANI Napia hutumika kwa matumizi mengi sana kama vile dawa na kiungo ana pia kama kinywaji.

HALI YA HEWA NA UDONGO
Husitawi vizuri katika maeneo ya ktropikia , mwinuko wa mita 1400- 1500  kutoka usawa wa bahari.
pia huitaji mvua kiasi mm 1200-1800 na joto nyuzi 20-25.na ustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usio tuamisha maji.Udongo wa alikali haufai katika kilimo cha tangawizi , pia hautakiwi kupanda tangawizi katika shamba hilo hilo kila mwaka hivyo unatakiwa kubadili mazao,
PH ya udongo inayo itajika katika kilimo cha Tangawizi  ni 5.5- 6.5

MBEGU
Tangawizi hupandwa kwa kutumia tungulu kwa kukata mzizi wa mmea mama, na kila tungulu linalo tumika kupanda hutakiwa kua na afya nzuri na lenye urefu wa cm 2.5 hadi 5na uzito wa gram 20- 25 na uwe na vitokezo(buds) 2 au 3 kwa kila tungulu moja. tungulu linalo tumika kupanda linatakiwa kutibiwa na Dithane M-45
ni muhimu pia kuzingatia mbegu zilizo bora

KUANDAA SHAMBA
 Ardhi hutakiwa kutifuliwa angarau mala 3 hadi 4 ili kuweza kuweka udongo katika hali nzuri ya kupanda.unaweza kutifua kwa kutumia trekta, jembe la ng'ombe au jembe la mkono
 pia andaa vitalu venye upana wa mita 1 na unene wa cm 15 na pia kuwe na nafasi ya cm 50  kwa kila kitalu, na unatakiwa kuweka mbolea ya asili mfano mavi ya ngo'ombe kiasi cha tone 15 hadi 20 kwa hecta kabla ya mkatuo wa mwisho.

KUPANDA
Muda mzuri wa kupanda Tangawizi ni may na june, na kiasi cha mbegu kinacho weza kutumika ni kg 1500 hadi 1600 katika hekta moja. 
pia mbegu hutakiwa kutibiwa na 25% agallol na macrotophos kwa dakika 30 hadi 40 kabla ya kupanda ili kuzuia nzi wa tunguru na pia zingatia kuaandaa mbegu katika kivuli. 
pia kuna aina tofauti tofauti ya kupanda Tangawizi.
  • kama unatumia vitaru vilivyo inuka nafasi ni cm 30 x 30 na ukitumia vitalu ambavyo havijainuka nafasi ni cm 25 x 22.5 .
  • pia katika kupanda zingatia jicho la kitokezi yaan bud linatakiwa kuangalia juu na panda kwa kina cha sm 5 kwenda chini ya ardhi .
  • pia njia ya kupanda katika vitalu ambavyo viko flat ndio njia ambayo imeonekana kufanya vizuri zaidi.
 MAMBO MUHIMU KATIKA KILIMO CHA TANGAWIZI
  • Matandazo(mulching); hii ni muhimu husaidia kupunguza kukua kwa magugu na pia hupunguza mmomonyoko wa ardhi. na pia upunguza maji kupotea katika mmea, unaweza kutumia majani yoyte makavu kama matandazo  baadae huoza na kua kama mbolea.
  •   kivuli(shading);unaweza kuweka kuvuli kwa kupanda mbaazi kitaka kona ya vitalu vilivyo inuka
  • kupalilia(weeding);unatakiwa kupalilia kwa kutumia jembe la mkono katika miezi miwili ya kwanza  ili kuweka mmea safi  na unaweza kupalilia mara 5 hadi 7 ili kupata mazao mengi zaidi.
  • kuinulia udongo(earthinig- up); katika wiki ya kwanza september baada ya kupanda ,may au june unaweza kuinulia udongo hiyo inasaiudia kufanya mizizi kuweza kupenya vizuri na  pia mizizi hukua vizuri.
WADUDU NA MAGONJWA
  • vipekecha bua(shoot borel)-hawa ni wadudu wanao vyonza bua na bua hubadilika na kua na mashimo na kuwa yanjano. tumia dawa ya 0.1% malathion kwa kila mwezi mara moja kuanzia july hadi august 
  • nzi wa tungulu(rhizome fly); hawa nzi ufyonza tungulu, dhibiti kwa kutumia 0.05% methly kuanzia july na kuendelea
  • vivingilisha  jani(leaf rollers); hawa ni wadudu wanao kula majani ya tangawizi, zuia kwa kutumia 0.05% dimethoate itasaidia
  • scales; hawa pia ufyonza tungulu na kusababisha kusinyaa na kukauka, zuia kwa kutumia 0.05% dimethoate wakati wa kupanda.
  • chinese rose beetle; hawa wadudu hula majani na kuancha veins , wadudu wakiwa wakubwa hua na rangi nyekundu kuelekea kahawia hawa wadudu wanakula wakati wa usiku, kuzuia weka mwanga shambani kwa kua hula wakati wa giza.
MAGONJWA
  •  Muozo rain(soft rot); majani ya chin hubadilika rangi na kuelekea kua njano, ugonjwa unasambaa kutoka kwenye mbegu, tungulu na udongo, zuia kwa  kutinu mbegu kabla ya kupanda, kuweka kuisi sahihi cha maji katika kitalu na pia kwa kupulizia fungicide katika vitalu kabla ya kupanda au captafol @ 0.1%
  • madoa jani(leaf spot); madoa meupe na yenye kingo nyeusi ujitokeza katika majani pulizia 1% bordeaux husaidia
  • bacteria wilt; majani huanza kuonyesha michillizi mweusi zuia kwa kutumia streptocycline @ 200ppm 
KUVUNA 
 Kuvuna hutegemea na atua ambayo wewe unataka kutumia, kwa ujumla ukiitaji kuvuna Tangawizi ikiwa ya kijani uvunaji unatakiwa kufanywa kwa siku 215 hadi 220 baada ya kupanda  na ukiiitaji kuvuna ambayo imeanaza kukauka  unatakiwa kuvuna siku 250 had 260 baada ya kupanda, unatakiwa kuvuna pale majani yanapoanza kubadilika na kua yanjano .

na pia unaweza kuvuna Tangawizi ya kijani kias cha tonne 10 hadi 15/ ha kama ikiwa na matunzo mazuri na ilio kauka unawezam kuvuna tonnes 35 hadi 40/ha


No comments