UTANGULIZI
Kwale ni jamii ya ndege wa porini ambao kwa sasa hufugwa sana majumbani kutokana na kugungukika kua na faida, hasa mayai yake kua na faida nyingi mwilini.
kwale hutaga mayai kama kuku, kanga au bata, pia kwale hua na umbile dogo 280- 300g.hivyo nitaelezea mambo muhimu ambayo unatakiwa kuyafahamu katika ufugaji wa kwale.
UTUNZAJI WA VIFARANGA
vifaranga wa kwale hutakiwa kutunzwa vizuri kama ambavyo vifaranga wa ndege wengine hutakiwa kutunzwa.
- hivyo unatakiwa kuandaa mazingira mazuri kabla ya vifaranga wa kwale hawajeletwa bandani
- siku ya kwanza wanapofika unatakiwa kuwapa GLUCOSE ukiiichanganya kwenye maji, pakti moja kwa lita 20 za maji
- baada ya masaa 2 unaweza kuwakea chakula kilicho andaliwa maalum kwaajili ya vifaranga.
- siku ya pili hadi tano unatakiwa kuwawekea amin total kwenye maji, na uwape maji yasiyo changanywa kitu sita na kuendelea.
- pia watoto hutakiwa kuwapa joto unaweza kutumia bulb au chemri au jiko la mkaa kulingana na uwezo wak, vifaranga hutakiwa kupatiwa joto kwa masaa 24 ndani ya siku 7
- siku ya 15 -21 uhitaji wa joto utapungua unaweza kuwapa joto wakati wa usiku tu, ila hiki ndio kipindi ambacho vifaranga hula sana hivyo wanatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha pia.
- kuanzia siku ya 21na kuendelea nikipindi ambacho kwale hawaitaji joto hivyo chakula na maji ya kutosha ndio muhimu kwa kipindi hiki.
Kwale wakipewa huduma nzuri, chakula na maji ya kutosha huanza kutaga wanapofikisha wiki ya sita kuelekea ya saba ,kwa kipindi icho utaanza kuona kwale wakianza kutaga mayai kila siku , kwa wastani kwale mmoja anauwezo wa kutaga mayai 250- 300 kwa mwaka wakipewa chakula stahiki.
MAGONJWA
Kwa bahati nzuri kwale ni ndege ambaye hua na kinga sana mwilini kwake na sio rahisi sana kwa kwale kupata magonjwa kirahisi. na pia pindi wanapo ugua ni rahisi pia kutibika.
hivyo ni muhimu kuweka mazingira na banda safi ili kuweza kuzuia magonjwa kama typhoid, mafua na kuharisha.
Pia kwakua kwale ni jamii yandege kama alivyo kuku hivyo utakiwa kupewa chanjo ili kuweza kuzuia magonjwa
- siku ya 7 wapatie chanjo ya kideri/new castle ambayo inapatika kalibia maduka yote ya dawa za mifugo.
- siku ya 14 unatakiwa kuwapa chanjo ya GUMBORO ambayo pia hupatikana katika maduka ya dawa za mifugo
- siku ya 21 unatakiwa kurudia kuwapa chanjo ya kideri/new castle
- siku ya 35 unatakiwa kuwapa chanjo ya ndui/ fowl pox
FAIDA ZA KUFUGA KWALE
Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine
Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine
- chanzo cha kipato kwa wafugaji
- hawana gharama sana katika kufuga
- hawataji utaalam sana katika kuwafuga
- mayai yake ni tiba ya magonjwa mbalimbali
- mayai yake hayakosi soko
1 Comments