JINSI YA KUANDAA SHAMBA




 UTANGULIZI
 Habari za sahizi mpenzi msomaji, nitumani langu u buheri wa afya nami namshukuru mungu kwakuzidi kunipa afya njema.
kumekua na sababu nyingi sana ambazo husababisha wakulima wengi kushindwa kufikia malengo yao kwakua hawapati vile wanavyo taraji hivyo hukata tamaa nakusema kua kilimo hakina faida.
 na pia wakulima wengi wamekua wakiweka maandalizi mabovu ya mashamba kabla ya kupanda hivyo mazao kutoweza kusitawi na kuzaa kama inavyo takiwa.
hivyo nimeamua nikuletee mambo ya msingi ambayo wewe mkulima unatakiwa kuyafaham na kuyazingatia wakati wa kuandaa shamba lako wakati wa kilimo.
kama tunavyo faham baadhi ya maeneo tayari msimu wa kuaandaa shamba ndo umekaribia kuanza mfano biharamulo.
 
FAIDA YA KUANDAA SHAMBA 
Kama tunavyo faham  kuandaa shamba ni muhimu sana, inawezekana wewe mpenzi msomaji unaweza kua unafanya kilimo bila hata kuandaa shamba ipasavyo kwa sababu bado ujafaham faida za kuandaa shamba hivyo hizi ni baadhi ya faida za kuandaa shamba lako.
  • kupunguza kasi ya kuota magugu
  • kurainisha udongo ili kuwezesha mizizi kupenya vizuri ardhini
  • kuondoa na kupunguza magonjwa na wadudu shambani
  • pia husaidia kuongeza rutuba katika shamba
  • husaidia kuhifadhi unyevu katika shamba
  • husaidia pia kuweka shamba katika level moja 
  • kuondoa vitu visivyo itajika shambani mfano mawe na magogo
  • pia husaidia kufukuza wadudu hatarishi shambani mfano nyoka,nge na wadudu wengine hatari
  • hurahisisha upaliliaji
  • pia wewe kama mkulima unakua huru kutembelea shamba bila wasiwasi na kufika mahali popote shambani hivyo kua rahisi kufaham tatizo ambalo linaweza kutokea shamban.
  • husaidia kuweka mazingira rafiki ya zao ambalo unataka kulima. mfano mifereji ya maji
hizo ni baadhi tu  ya faida za kuandaa shamba hivyo wewe mkulima nadhani umepata mwanga kidogo na kuona jinsi kuandaa shamba inavyo kua ni jambo muhimu katika kilimo.

 MAMBO MUHIMU
Baada ya kuziona na kuangalia faida za kuandaa shamba hivyo nataka nikupeleke moja kwa moja ili uweze kufaham jinsi ya kuandaa shamba kwaajili ya kilimo.
  • fahamu ukubwa wa shamba, kabla ya kuandaa shamba ni muhimu sana wewe kama mkulima kufaham ukubwa wa shamba lako, hii itakusaidia kufaham ni kifaa gani ambacho wewe unaweza kutumia kuandaa shamba, mfano huwezi kua na hekta 100 na ukatumia jembe la mkono kusawazisha shamba lako.hivyo ukifaham ukubwa wa shamba lako itakusaidia hata kupunguza gharama pia.
  • fahamu aina ya zao unalotaka kupanda, hili pia ni jambo la muhimu sana bila kufaham aina ya zao ambalo unataka kupanda itakua pia kwa wewe mkulima kuandaa shamba lako. mfano ukitaka kupanda matikiti nilazime utengeneze vitaru tofauti na ukitaka kulima mahindi vitalu haviitajiki. hivyo bila kufaham aina ya zao unalo taka kupanda sio rahisi pia kuandaa shamba.
  • fahamu asili/tabia ya eneo, pia ni muhimu kuulizia na kufaham asili na tabia ya eneo hii pia itasaidia kurahisisha uandaaji wa shamba lako.mfano eneo kama lina asili ya maporomoko,Maporomoko au kutuamisha amji hivyo utajua jinsi ambavyo utaandaa shamba lako eidha utaweka matuta au la, hivyo pia nimuhimu sana kufaham asili/tabia ya eneo unalo taka kulima.
JINSI YA KUANDAA SHAMBA.
Kama tunavyo faham mazao ni tofauti, hivyo kila zao hua kunajinsi ambavyo shamba la zao flani linatakiwa kuandaliwa.
ila kama tunavyo faham binadamu pia tunatabia tofauti lakini kunatabia ambayo ni lazima kila mtu awe nayo mfano kula na kulala hivyo hata kwa  mazao kunavitu ambavyo ni lazima kila zao hutaji hivyo hapa nitaelezea maandalizi ambayo nilazima kabla ya kuanza kilimo ufanye
  • kusafisha shamba,baada ya kufaham mambo muhimu sasa nilazima katika eneo la shamba uondoe vichaka, visiki,railoni,mawe na miti mikubwa ambayo haiitajiki shambani, pia tafuta eneo na uchome takataka hizo. sio vyema kuchomea shambani kwa sababu unaweza kuua wadudu rafiki shambani hivyo unatakiwa kuchomea nje ya shamba. unaweza kutumia panga, shoka au fyekeo.
 
  • kusawazisha shamba,baada ya kusafisha shamba kinachofuta ni kusawazisha shamba, unaweza kutumia jembe la mkono, jembe la ng'ombe au trekta kulingana na ukubwa washamba pia na uwezo wako. hii ni muhimu sana kwa sababu unapo sawazisha shamba shamba lote linakua katika level moja pia husaidia kuvunja vunja udongo . wengine hutumia dawa za kuua magugu(round up ) yakisha kauka ndipo usawazisha shamba, na unatakiwa kuzika majani yaliopo shambani kwa sababu yanapo zikwa huoza na kugeuka kua mbolea. pia unatakiwa kusawazisha shamba mapema yaani mwezi mmoja kabla ya kuoanda, hiyo husaidia mazao na majani yaliyo zikwa kupata mda wa kutosha ili yaweze kuoza kabla hujaja kupanda.
 
  • kutifua shamba, baada ya mwezi mmoja sasa wakati wakukaribia kupanda unatakiwa kutifua tena shamba,hii husaidia kurainisha udongo pia kuwezesha kuchanganya udongo ili mbolea iweze sasa kusambaa katika shamba zima na pia huweka shamba tayari kwaajili ya kupanda. sasa hapo wewe kama mkulima unaweza kuchagua jinsi ya kufanya shamba kutokana  na aina ya zao unalotaka kupanda.

No comments