Jifunze Kilimo bora Cha strawberry


UTANGULIZI
Zao hili hustawi katika joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa, hasa katika nyumba maalumu ya kuzalishia mimea yaani green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari. Endapo unahitaji kuzalisha stroberi  katika maeneo ya bondeni itakulazimu kuwa na maji kwa wingi kwa ajili ya umwagiliaji wa mara kwa mara.

 UDONGO
Stroberi inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi.

 KUPANDA
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, bila vipingamizi, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). Katika kuzalisha stroberi baada ya kujenga green house andaa mabomba ya plastiki ambayo yatawezesha kutoboa matundu kwa urahisi,
• Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
• Ni vyema matundu hayo yakawa zigizaga, ili kuruhusu mimea utakayopanda kukua vizuri bila kuwekeana kivuli.
• Tandika karatasi la nailoni sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au sehemu ya kuhifadhia.
• Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
• Jaza kokoto, yenye mapande makubwa kiasi.
• Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea.
Au kama utapenda kutumia pots, mifuko at ndoo ni bora kutumia mchanganyiko mzuri kati ya udongo, kokoto, mbolea ya samadi, vumbi la mbao na mkaa.
Mchanganyiko huu he saidia kuweka udongo ktk hali ya tifutifu na kuruhusu mizizi kupenya ardhini kwa urahisi.

 KUMWAGILIA
Mimea ya stroberi inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.
Kama watumia pots, ndoo au mifuko ya simenti inakupasa kutumia local dripping drop. Chukua chupa ya maji yenye Lita 1½ toboa vitundu ili maji yadondokee mche wako kila dakika.

 MBOLEA
Uzalishaji wa kisasa wa stroberi, unaambatana na ufugaji wa samaki kwenye bwawa ndani ya green house. Mbinu hii husaidia mimea kupata mbolea inayotokana na chakula wanacholishwa samaki kwenye bwawa, kwani maji yanayofugia samaki ndiyo hayo yanayotumika katika mzunguko wa umwagiliaji. Hii inamaanisha kuwa hakuna mbolea nyingine inayohitajika kwa ajili ya stroberi.
Lakini km hauna mabwawa ya samaki waweza tumia mbolea ya Ng'ombe, mbuzi, kuku na unapaswa uiongeze kila baada ya miezi 4 kwa mbolea ya wanyama wa kienyeji na miezi 3 kwa mbolea ya wanyama wa kisasa.

 WADUDU NA MAGONJWA
Endapo stroberi inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi.

 DAWA
Endapo stroberi itashambuliwa na magonjwa ya ukungu na virusi, nyunyizia dawa za asili kama vile pareto, kitunguu saumu au mwarobaini, na baada ya muda kutakuwa na matokeo mazuri.

 UVUNAJI
Zao la stroberi, huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Na kati wauhudumia vizuri mtu wako, utazaa miaka 3 ndipo utazeeka na kufa. Kila wiki stroberi inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo. Ikishafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za kuvuna mfululizo. Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda  wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwa.

Usipitwe na mafunzo mengine bofya picha chini



No comments