MAGONJWA YA NGURUWE
Zifuatazo ni dalili za nguruwe mgonjwa;-
·
haonyeshi dalili
za kupenda chakula
·
anaweza kuhema
kwa kasi dalili ya homa
·
macho makavu
·
ngozi kavu
·
anakua anajitenga
·
masikio kulala
·
kwenye ngozi
nyeupe ngozi inaweza kua nyekundu
·
mkia kua
mwembamba
·
kuhalisha mda
mwingine kuhalisha damu
MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA WADUDU
Wadudu wa ndani
Minyoo ndo wadudud wakuu
wanaathiri tumoni kwa nguruwe, kuna minyoo zaidi ya 30,ila minyoo ambao
wanaathiri kwa wakati mwingi ni minyoo duara(round worm) na minyoo tape(tape
worm).
Round worm
Hii
ukaa kwenye utumbo mpana wa nguruwe na uchukua chakula kutoka kwa nguruwe hivo
nguruwe anaweza kukonda.minyooo mikubwa(Ascaris lumbricoides) hii ndo
inapatikana sana.minyoo hii nimikubwa
urefu wa penseli.maambukizi yanaanza pale myama anapo kula chakula chenye mayai
ya monyoo hao.
DALILI
·
Kunyonyoka
manyoya(anorexia).
·
Upungufu wa
damu(anaemia).
·
Baadae uzito
upungua.
·
Minyoo wakitibiwa
wakati washakua wengi wanaweza kukata utumbo na kusababisha kifo.
KUKINGA/PREVENTION
·
Kuzuia kwa kuweka
dawa kwenye chakula na kutumia vyombo visafi
·
Kuchunga kwa
kutumia njia ya mzunguko na kutibu nyasi
·
Kuwatenga watoto
na wakubwa
·
Kuwapatia dawa ya
minyoo mara kwa mara
·
Muoshe jike kabla
ya kuzaa
·
Unaweza kutumia
miti shamba aina ya moringa
Tape worm
Hawa
wanakua frat kama rebon na wanapatikana mahali tofauti tofauti dunian.hawana
utumbo hivyo wanakula kupitia ngozi yao na wanachukua virutubisho.hua
wanachukua folic acid na vitamin B-12 mwilini,wanaweza kusababisha sumu kwakua
baada ya kula wanaacha uchafu na unakua kama mpira ambao unakaa karibu na ini.
DALILI
·
Kudumaa
·
Upungufu wa damu
·
Ngozi kubadilika
nakua mbaya
KINGA/PREVENTION
·
Kuwapa dawa ya
minyoo
·
Hakikisha wanao
hudumia nguruwe wawe wanatumia choo na kusafisha
WADUDU WA NJE
Wadudu
wa nje inahusisha mange.lies na myiasis
Mange
Husababishwa
na wadudu wanao itwa mites wanaishi kwenye ngozi ya nguruwe maeneo ya machoni,
masikioni,miguuni na shingoni
DALILI
·
Nguruwe anakua
anjikuna kuna kwenye ukuta kwenye miguu,masikio,macho na masikio
·
Ngozi inakua na
mabaka kama vibarango na mistali mistali mwenkundu kama vidonda
·
Manyoya hua
yamevurugika
·
Ngome anakua
hatulii
·
Vifo
·
Na kupungukiwa
damu kwa watoto
KINGA/PREVENTION
·
Osha nguruwe mara
mbili kwa wiki
·
Madume wanatakiwa
kuoshwa pia
·
Wape dawa kila
nguruwe anapoingia shambani kwako
·
Usafi wa banda
TIBA/TREATMENT
·
Unaweza
kuwaosha pia kwa maji safi na sabuni
·
Unaweza kuwaosha
kwa organophosphate
·
Unaweza kuwachoma
Ivermectin kwakua inasaidia sana
CHAWA
Hawa
wanakua wananyonya damu na dalili zake ni upungufu wa damu na pia mnyama anakua
na madoa mekundu mwilini. Na pia unaweza kutibu Kwa kutumia viuadudu (insecticide)
benzene hexachloride ndo hua inatumika kuua chawa.
MYIASIS
Huu
ni ugonjwa unaosababishwa na nzi wanao taga mayai kwenye vidonda,mayai hayo
hukua hadi kufikia hatua ya kua nzi mkubwa na husababisha kidonda kua kikubwa
zaidi.
Kidonda
hua kichafu na kua kama na ukungu mweusi ambayo hayo ni mayai ya nzi,hivyo
kuzuia hii unatakiwa kusafisha banda na kupunguza idadi ya nguruwe katika banda wasisongamane
KUWAPA DAWA ZA MINYOO(DEWORMING)
Dawa
za minyoo ambazo zimehakikishwa nan i salama pale zinapo pewa kutokana na
maelekezo sahihi ni kama
vermectin
(Ivomec®), fenbendazole (Safe-Guard®), levamisole (Tramisol®, Levasole®),
pyrantel (Banminth®), dichlorvos (Atgard®) na piperazine.
Unaweza
kupanga ratiba ya kuwapa dawa zaminyoo na ukapanga na mtalaamu ili kua anawapa
chanjo ifikapo siku sahihi
·
Dume/Boars – kila
miezi 6 months
·
Jike/Sows – wiki 2
kabla ya kuzaa na baada ya kuwatenga watoto
·
Watoto/Piglets – wiki
1 baada ya kuwatenga
·
Wanao nenepeshwa/Fatteners
– wiki moja baada ya kuwatenga na miezi mitatu badae
·
Gilts – wiki 1 aada ya kuwatenga na unaweza
kurudia miezi mitatu badae
DAWA ZA WADUDU WANAO JITOKEZA MARA KWA
MARA
MINYOO NA HATUA
|
DAWA
|
Ascarids(adult)
|
Zote
|
Ascarids(hatua ya larva wanao hama)
|
Fenibendazole
|
Ascarids(hatua ya larva waalibifu)
|
Fenibendazole.pyrantel
|
whipworms
|
Feniendazole, , dichlorvos
|
Noduluar worm
|
Zote
|
Minyoo ya figo(wakubwa)
|
Fenbendazole, ivermectin, levamisole
|
Minyoo wa figo(larva katika ini)
|
Fenbendazole, levamisole
|
strongloydes
|
Fenbendazole
|
Levamisole, ivermectin
|
ANAPHRODISIAS
Pale nguruwe anaposhindwa
kuingia kwenye joto.hapa nguruwe anakua haingii kwenye joto hii inaweza
kusababishwa Na uzito mdogo kutokana na kuwalisha chakula kisicho tosha au
kisicho na virutubisho, uzito ulio zidi, upungufu wa madini, minyoo kwenye
utumbo, magonjwa sugu.
LEPTOSPIROSIS
Dalili ya ugonjwa huu ni
homa, kuhara,kukojoa damu na kupolomosha mimba kwa hatua ya mwisho na unaweza
kuwatibu kwa streptomycin kabla ya tendo. Na unaweza kutumia dawa za
antibiotic.
.
BRUCELLOSIS
Ugonjwa huu unatokea kwa
dume na jike na inakua na dalili kama vile kunyonyoka manyoya,homa,kupooza
miguu,kilema,na kutoa mimba mapema, na kwamjike ambao tayari wanazaa huzaa
watoto zaifu,uke hua na mwekundu na pia kondo hutoka nje na kwa dume hua na uvimbe kwenye mapumu ya nguruwe.
Na ugonjwa huu hauna tiba
hivyo chinja nguruwe wenye ugonjwa huu.
UTERINE PROLAPSED
Ugonjwa huu usababisha
uterus kutoka nje,napia ugonjwa huu hauna tiba hivyo mnyama hutakiwa kuchinjwa.
.
MASTITIS
Bacterial husababisha
kuvimba kwa kiwele na kupelekea kubadili uzalishaji wa maziwa,
Dalili za ugonjwa huu ni
kiwele kuvimba kua chamoto na maumivu napia uzalishaji wa maziwa upungua.
Unaweza kutibu kwa kukanda
chuchu ambazo na usiruhusu watoto kunyonya,toa maziwa yote kwenye kiwele baada
ya hayo tumia antibiotics.penicillin-streptomycin.
.
ATROPHIC RHINITIS (KUVIMBA KWA PUA)
Dalili ya ugonjwa huu kwa
watoto wanakua wana koroma,kukohoa na kupumilia mdomo na unaweza kutibu kwa
kutumia antibiotics na usafi pia ni muhimu
GREASY PIG DISEASE
Huu ni ugonjwa unao
sababisha mabaka,vibarango kwenye ngozi,pia mnyama upungua kilo na anaweza
kufa.zuia kwa kuzuia ugomvi wa nguruwe
kwa kuwakata meno,kuwapa chakula cha kutosha,usafi na tumia antibiotics
FOOT AND MOUTH DISEASE (FMD)
huu ni ugonjwa wa mdomo na
miguu na inadhulu wanyama wenye kwato
Dalili zake nguruwe
anaweza kua kilema,homa na vidonda mdomoni na miguuni
unaweza kutibu kwa kutumia
antibiotics.
Vaccination Disinfection
No therapy (treatment)
ANTHRAX/kimeta
Kimeta
kinasababishwa na kuwalisha nyama nguruwe na dalili zake ni kupumua kwa shida,kuvimba
shingon,homa na kutoa kinyesi chenye damu
na mnyama alie
kufa na kimeta hutoa damu maeneo ya wazi mwilini.
Na unaweza kutibu Kwa kutumia antibitics.
Post a Comment