KILIMO BORA CHA APPLE



UTANGULIZI(Malus pumila)
     Apple ni moja kati ya matunda yanoyo pendwa sana, na wengine wamefikia mbali hadi kulifanya apple kua tunda la ishara ya upendo, pia kuna aina mbili za matunda ya apple yaani yanoyo liwa bila kupikwa na yale ambayo ni lazima yapikwe ili uweze kuyala.
  
    Matunda ya apple hayafanyi vizuri katika maeneo ya joto, huitaji hali ya hewa iliyo tulia na isio kua na joto kali, kutokana na mahitaji haya apple hukua vizuri Tanzania kwenye maeno ya umbali wa 2000- 3000 miters kutoka usawa wa bahari. mfano Mbeya, Arusha na Iringa.

  AINA 
    Aina nyingi za apple hutegemea hutegemea miti ya aina nyingine iliyo pandwa karibu ili kuwezesha kuichavusha(pollination) hivyo mkulima ni lazima kupata ushauri kutoka katika office za mboga mboga na matunda(holiticultural) ili kuweza kupata aina nzuri zaidi.

    kwa Tanzania utafiti wa apple hufanywa katika kituo cha uyole kilichopo Mbeya  na kituo cha Tengeru kilichopo Arusha unaweza kupata aina nzuri zaidi kutoka katika hizo taasisi.

JINSI YA KUPANDA
kwa kawaida miche ya apple upatikana kwa kutumia njia ya grafting na unaweza kupata miche hiyo katika taasisi binafsi au za serikali nilizo zitaja hapo awali.
nafasi ya upandaji inategemea na aina ambayo unataka kupanda]
  1. aina ndogo 2m x 2m
  2. aina ya kati 2.5m x 2.5m
  3. aina kubwa 3.0m x 3.0m
KUANDAA SHAMBA
Kama ardhi unayo panda inamtelemko ni lazima ufate  mistari ya kontua, pia chimba mashimo ya kupandia kila shimo linatakiwa kua na 60cm upana na 60 cm urefu.

KUPANDA
 Miche ambayo imekuzwa katika kitalu inatakiwa kuiamishia shambani katika kipindi ambacho hakuna joto, lakin miche ambayo imekuzwa kenywe poti au karatasi za plastik zinaweza kupandwa mda wowote ule.
unapopanda panda katikati ya shimo na hakikisha mizizi yote umeitandaza,  changanya udongo wa juu(top soil) na ndoo mbili za 20 liters za mbolea ya samadi,na baada ya kupanda hakikisha unamwagilia vizuri.
kama aina yako inaitaji kuchavushwa basi hakikisha unapanda miche ya uchavushaji kila baada ya mistari 2 au 3 ya aina ambayo unataka kuchavushwa.

KUKATIA (PLUNNING)
Miti ya apple inaitaji sana kupruniwa katika miaka 3 ya kwanza ili kuweza kukua vizuri na kutengeneza umbo lililo zuri.
baada ya miaka 3 na mti umeshakua na umbo linalo itajika unacho takiwa ni kupluni au kukata matawi yaliyo vunjika, yaliyo kauka au yaliyo kua nje ya utaratibu.

MBOLEA
Kama mbolea ya samadi au mboji inapatikana unatakiwa kuweka liter 20 za mbolea katika kila mche kwa kila mwaka pia DSP na CAN au SA inaitajika kwa kila mwaka. unaweza kuwasiliana na afisa ugani wa eneo lako ili kupata ushauri zaidi.

KUVUNA
matunda hua madogo pale yanapo kua na msongamano, ili kuepusha hilo zingatia kuvuna matunda yote yanayo kua yamekomaa ili kuyapa n afasi mengine.

MAGONJWA NA WADUDU WAHALIBIFU
Wadudu wahalibifu ni 
  • wooln aphids
  • bui bui wekundu
  • mchwa
magonjwa
  • ubuli unga
  • kuoza mizizi
  • apple anker 
  • apple scab
unaweza kuzuia kwa kutumia dawa za wadudu au wasiliana na afisa ugani aliyo karibu nawe.
unaweza kuungana na ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya hapa

6 comments

Unknown said...

je mbegu zake unaweza kuzipata vipi

Rubaba Imani said...

unaweza kuzipata katika taasisi ya utafiti wa kilimo uyole mbeya

AUGUSTINO YOHANA KORONDI said...

Je nikipanada mbegu zake zinaweza kumea? Je kwa mikoa ya kanda ya ziwa mmea huo unaweza stahimili?

Rubaba Imani said...

Ndugu yohana, Nivizuri zaidi kununua miche ambayo tayari imeshachipu, na zao hili linafanya vizuri hasa kwenye maeneo yenye baridi

Anonymous said...

Mti mmoja unatoa wastani wa matunda mangapi kwa mwaka?

Anonymous said...

Enock Simon,Iringa.Dawa kwa magonjwa yanayo ikumba mimea hii ni zipi?,Unaweza vuna kwa mda gani mpaka mmea kupoteza nguvu ya kutoa matunda bora?