KILIMO BORA CHA NAZI



UTANGULIZI

   NAZI(cocos musifera)
Ni zao lenye jamii ya palm na hukuzwa rasmi kwaajili ya kutoa nazi ambalo ndilo hutumika kama kiungio cha chakula, kutengeneza mafuta ya kula na yakujipaka na hutumika kama kinywaji. lakini nazi linaweza kuvunwa likiwa limekomaa au likiwa bado changa(dafu).

HALI YA HEWA NA UDONGO
    Nazi hukua na kusitawi vizuri katika maeneo yenye mvua ya kutosha, zao hili huitaji kwa mwaka mvua kiasi cha 2500mm kwa maeneo yenye mvua chache mavuno hua sio mazuri na ukame huathiri utengenezaji wa maua. Nazi husitawi vizuri katika maeneo ya kikostor kwa hapa Tanzania nazi hustawi vizuri mikoa ya pwani, tanga na dar es salaaam.
   pia nazi ustawi viziri kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha na kwa maeneo yasio na rutuba ya kutosha unaweza kuongeza mbolea.

AINA 
aina zingine ni ndefu na hujulikana kama East African Tall na aina nyingine ni fupi ili kufahama zaidi kuhusu aina inayo fanya vizuri katika maeneo yako wasiliana na afisa kilimo wa eneo lako.

 KUANDAA SHAMBA
 kumbuka kuandaa shamba kwa kuondoa taka na visiki vyote shambani, andaa mashimo kwa nafasi ya 8m x 8m au 9m x 9m. mashimo hutakiwa kua na upana wa 60cm na urefu wa 60 cm na mashimo yakae kwa mda wa wiki 3 hadi 4.


KUPANDA
Nazi hupandwa kwa kutumia mbegu zake ambazo ndio nazi, nilazima uchagua nazi ambazo zimekomaa na unapopanda usitoe kifuu na pia unatakiwa kufukia robo tatu ya nazi lote na kwa maeneo yasio na unyevu wa kutosha zingatia kumwagilizia.
 Toka kupandwa kwa mbegu miche hua tayari kuamishiwa shambani ikiwa na umri wa mwaka mmoja ambapo hua na majani 3 hadi  4 , zingatia kuchagua miche yenye afya wakati wa kuamishia shambani, pia unatakiwa kuhamishia miche shambani mwanzoni mwa mvua ndefu.

    Kwa shimo moja unatakiwa kupanda mbegu moja, fukia mbegu yako kwa 30 cm  na jaza kwa udongo wa juu ukiwa umechanganywa na mbolea ya samadi au mboji. na pia usiizibe mbegu yote ziba sehem ya chini na utajaza udongo pole pole pale mche unapo zidi kukua. na kwa miaka miwili ya kwanza unaweza kupanda shambani mazao yenye asili ya legume yaani leguminous plants mfano maharage.

MBOLEA
Mbolea husaisidia kuongeza mazao hivyo unatakiwa kutumia CAN, Double superphosphate na potash katika udongo kwa kila mmea, weka mbolea zote kwa kiasi cha 1/2 kg kwa kila mmea kwa kuzungushia kisha changanya na udongo.

KUPALILIA
Pale miche inapokua midogo unatakiwa kupalilia kwa kutumia jembe la mkono kwa kila mmea na zingfatia umakini ili usije kujeruhi mizizi ya mmea na fyeka nyasi kwa eneo lililo bakia
pale mimea inapokua ni muhimu kuondoa vichaka vyote shambani na kufyeka eneo lililo baki au unaweza kuruhusu mifugo kuchunga shambani na pia zingatia kuondoa magugu yote karibu na mmea.

MAGONJWA NA WADUDU WA HALIBIFU 
Wadudu waharibifu ni
  • Rhocerous bettle
  • coreid bags
  • coconut beetle
magonjwa
  • kuoza shingo'
  • fungus
tumia dawa za kuua wadudu na dawa za fungus, napia zingatia kutojeruhi mmea wakati wa kupalilia au wakati wakuamishia shambani miche.

KUVUNA
 Kwa wale wanao taka kuvuna madafu hutakiwa kuvuna miezi 8 hadi 10 kutoka pale mimea inapotoa maua. na kwa nazi zilizo kuomaa unatakiwa kuacha mpaka zianze kuanguka zenyewe au unaweza kutumia wataalam wanao jua nazi zilizo komaa.

No comments