KILIMO BORA CHA KUNDE
UTANGULIZI
COW PEA ( vigna unguiculata)
Kunde ni moja ya zao ambalo pia hulimwa sana Tanzania, Majani yake yanaweza kupikwa na kuliwa au kunde yenyewe inaweza kuchemshwa na kuliwa kama mboga, au inaweza kukaushwa na kutumiwa kwa matumizi ya baadae.
HALI YA HEWA NA UDONGO
Kunde husitawi vizuri katika hali ya joto na udongo wa kichanga na inaitaji mvua chache ukilinganisha na maharage ya kawaida kwa maana hiyo kunde hustawi vizuri katika maeneo yenye mvua za wastani.
AINA
Kuna aina nyingi za kunde ambazo kuna kunde nyeupe, malai, kahawia, zambarau na nyeusi hivyo unaweza kufanya chagua kama utakavo penda. lakini aina ambayo hutumiwa sana katika maeneo tofauti tofauti ni SV-53, Tumaini, fahari, TK5 na vuli.
KUPANDA
Mkunde hupandwa kwa kutumia mbegu zake ambazo ndio kunde, na huitaji kiangazi wakati wa kukua hivyo panda mbegu zako miezi 2 kabla ya kuisha kipindi cha masika.
nafasi ya kupanda ni 75 cm mstari kwa mstari na 20 cm kati ya mmea kwa mmea.
MBOLEA
Kabla ya kupanda weka mbolea ya TSP kwa kiasi cha 100kg/ha, na ikiwezekana unaweza kuweka mbolea ya kukuzia yaani SA baada ya wiki 3 toka kupanda.
PALIZI
Kunde huitaji palizi hasa katika wiki 6 za mwanzo, na kwakipindi hiki palizi mbili zinatosha .
MAGONJWA NA WADUDU
Kama maharage kunde hushambuliwa na wadudu na magonjwa ya aina nyingi,wadudu ni kama vile mende wanao kula majani,kipekecha ganda na kidudu mafuta, magonjwa ni kutu jani na virusi vya mosaic.kupanda mapema, kupanda mbegu safi na kusafisha shamba husaidia kupunguza kasi ya wadudu na magonjwa au unaweza kuwasiliana na afisa kilimo katika eneo lako.
KUVUNA
kama unataka kutumia majani ya kunde kama mboga unatakiwa kuvuna kabla hayajakomaa japo kua kuvuna majani zaidi ya mara 3 inaweza kuadhili upatikanaji wa mazao, na kama ulitumia chemical za kuzuia magonjwa na wadudu unatakiwa kuacha wiki 2 ndio uvune.
na unaweza kuvuna kunde kwa hawamu kadri zinavo komaa au unaweza kuvuna zote kwa wakati mmoja na lazima uzianike tena kama unataka kutunza kwa matumizi ya baadae.
Post a Comment