INUKA MKULIMA

Karibu kwenye programu yetu mpya inayolenga kuwawezesha wakulima kuvuka changamoto zao na kufikia mafanikio makubwa zaidi! Hii ni fursa maalumu kwako:

Jina la Programu: Inuka Mkulima

Manufaa kwa Wakulima

1. Msaada wa kitaalam: Upate ushauri wa kitaalamu, miongozo na elimu kutoka kwa wataalamu wa kilimo waliobobea katika nyanja zote.

2. Rasilimali za Kilimo: Pata habari za hali ya hewa, mbinu bora za kilimo, na teknolojia za kisasa.

3. Fursa za Soko, Mitaji, mikopo na Luzuku: Ungana na masoko na wafanyabiashara wa kilimo kwa njia rahisi pia utakutana na watu na taasisi zitakazo kusaidia kwenye maswala ya mitaji na pesa

4. Ushirikiano na usimamizi: Shiriki mikutano na warsha zinazojenga ujuzi na kukuza mawasiliano na wakulima wenzako na watu au taasisi zinazoweza kukusaidia.

Jinsi ya Kujiunga:

Jaza fomu yetu rahisi mtandaoni kwa kutembelea tovuti yetu rasmi HAPA. Pia, tuwasiliane moja kwa moja kwa simu kwa maelezo zaidi. HAPA


Tunakualika kuwa sehemu ya INUKA MKULIMA na kuleta mapinduzi kwenye kilimo chako. Jiunge nasi leo na uwe sehemu ya mabadiliko!

No comments