JINSI YA KULIMA MATIKITI MAJI

     Asante mpenzi msomaji kwa kuendelea kua na mimi siku zote..,
hii ni siku nyingine ambayo mungu ametupa ili tuendelee kuishi katika ulimwengu.., bila kupoteza mda leo ningependa kukupa elimu kidgo kuhuisiana na kilimo cha matikiti maji
 Matikiti maji ni moja kati ya matunda ambayo yanapendwa sana kutumiwa na watu wengi na hii ni kwasababu ni matamu
faham sasa jinsi ya kuyalima haya matunda..,

Kama unavo jua ili kitu kistawi na kizae vizuri kuna vitu muhimu ambacho kinaitaji na ili matikiti matikiti maji ya sitawi na kuzaa vizuri yanaitaji vifuatavyo;

  kuandaa shamba..,ninapo sema kuandaa shamba na maanisha kusafisha shamba kwa kufyeka majani yote shambani kutifua udogo at least 5cm kwenda chini ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi,mbolea na hewa kupita kirahisi kwenye udongo.Na hii inafanywa mwezi mmoja kabla ya kupata.. kuandaa hamba inajumuisha pia na kuweka seed bed pamoja na farrows yani mitalo ambayo ndio hua mbegu zinapandiwa.
  
kuweka mbolea,hapa mara nyingi hua tunaweka mbolea ya samadi au mboji kwa kua ndio mbolea bora na znarudisha virutubisho kwenye udongo na badae kuweka mbolea za chemikali zitakapo itajika ,

upandaji.., hapa ni sehem muhimu pia inamaana ukikosea hapa unaweza ukapata mazao yasio bora na machache..,matikiti maji hua tunapanda mbegu mbili au tatu lakn baada ya kukua kidogo unang'oa na unabakiza moja na siku zote hua inabaki ile ambayo imestawi vizuri  kuliko zingine. na pia inatakiwa kua muangalifu pale unapo kua una ng'oa ili usiikate mizizi  ya ule ulo baki.
na pia hua ni 1m yan 100cm kutuko shina hadi shina na 2m au 200cm kutoka tuta hadi tuta.

upaliliaji, ua siku zote tuna palilia siku 14 au wiki mbili baada ya kupanda na kuendelea kupalilia siku ambapo utaona majani yameanza kua mengi katika shamba..

umwagiliziaji na kupiga dawa.., mazao yote hua yanatakiwa kumwagiliziwa asubuhi na jion  kadhalika na kupulizia dawa kwa kua sitomata ambazo zinasababisha maji kuingia ndani ya mumea  zinakua zimefunguka wakati wa asububhi na jion.,napia unatakiwa kumwagilizia maji ya kutosha yasizidi sanaa wala ya sipungue yakizidi husababisha fungal disease na yakipungua yanaweza kusababisha mimea kunyauka na kushindwa kukua vizuru.

matching..,hiki ni kitendo cha kuliwekea tunda nyasi kavu ili kuepusha tunda kuoza au kwa kuguswa na m aji na hii ufanywa pale tunda linapo anza kutokeza..,lakn usije kuweka ntasi mbichi  na pia matching inasaidia kuifadhni maji katika mumea..,

note..,matikiti maji ni kati ya mazao yanayo sitawi na kuzaa sana sehem yenye joto hasa ukanda wa pwani matikiti  maji uchukua siku 90 hadi kuvunwa  lakni kwa maeneo ya baridi uchukua siku 120 na hua sio  matamu sana



natumaini ndugu msomaji umepataka  kitu kwa kusoma makala hii na utakaua umepata mwanga kwa kilimo cha matikiti  maji..,
mpaka wakati  mwingine twena mungu akitupa uzima

Post a Comment

4 Comments

Gharama zinazo weza kutumika kuanzia undaaji Wa shamba hadi mazao kukamilika kwa 1eka jumla naomba msaada wako
Rubaba Imani said…
asante ndugu AHAZI kwa swali lako zuri
ila nivigum sana kukuambia bei kamili ya gharama kwa kua kila eneo lina tofautiana bei ya vitu mfano dawa,gharama za kulima yaan vibarua
ila kiufupi ukiwa na mil 1 inaweza kua mtaji mzuri sana kwa kilimo icho
Unknown said…
Uko sahihi,milion 1 Hadi 1.2M kulingana na maeneo
Rubaba Imani said…
Asante kwa mchango wako