Utangulizi
Vitunguu ni moja ya mazao ambayo yanatumika sana inchini Tanzanania. na kitunguu ni zao ambalo linatumika kutegenezea vyakula vya aina nyingi sana mfano kachumbali,kiungo cha mboga, nyama na samaki na pia majani yake yanatumika kama mboga pia.
VITU MUHIMU KATIKA KUZALISHA ZAO LA VITUNGUU
Zao la vitunguu ni kati ya mazao ambayo haya itaji mvua nyingi hvo ustawi vizuri kwenye maeneo yasio na mvua nyingi, pia maeneo yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na jotokali pamoja na ukungu na wakati wa kukomaa zao la vitunguu hustawi vzuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha udongo unao ruhusu maji na hewa kupita vizuri na unao ifadh unyevunyevu kama vile udongo wa tifitifu na mfinyanzi.
UPANDAJI WA VITUNGUU
Kwa hapa tanzania upandaji wa mbegu za vitunguu katika vitalu uanza mwezi marchi hadi mwez mei kutegemea na msimu wa kiimo.
kilimo hiki ufanywa baada ya mvua za masika kubwa kuisha. na mbegu za vitunguu huoteshwa mapema sana vikikuziwa kwenye kitalu
kunaaina mbili za kupanda mbegu kwa kitalu eitha kupanda kwa mistali au kuzitawanya kwenye kitalu
. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya msitari na mstari
na baada ya kupanda mbegu zinafunikwa kwa udongo na baadae unaweka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mbegu zinapoota matandazo yanaondolewa na baada ya apo unaweka kichanja cha nyasi kavu ili kuweka kivuli kwa mmea na mbegu huota baada ya sku 7 had 10.
KUPANDIKIZA MICHE BUSTANINI
Upandikizaji wa miche ya vitunguu bustanini hufanyika baada ya miche kukua na kufikia unene wa penseli.
Mara nyingi miche hii itakuwa imesha kaa kitaluni kwa siku 40 baada ya mbegu kupandwa.
zingatia mda wa kupandikiza miche bustanini. Kwa sababu miche mikubwa sana itaweza kutoa maua badala ya kutoa tunguu. Na hivyo mara nyingi vitunguu namna hii hubaki na suke la maua.
Wakati wa kupandikiza miche haishauriwi kukata wala kupunguza majani. Miche ipandikizwe katika nafasi ya sm 30 kati ya mstari na mstari na sm 10 kati ya mche na mche.
Upandaji wa miche bustanini unaweza kufanyika kwenye mistari katika matuta au kwenye vijaruba. Vijaruba vya mraba hutumika
kwenye maeneo yenye ardhi tambarare na iliyo kame ili kuhifadhi maji baada ya kumwagilia. Kwa sehemu zenye udongo mzito na
zenye maji mengi tumia matuta yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm15 kutoka usawa wa ardhi.
MATUNZO YA BUSTANI YA VITUNGUU
UMWAGILIAJI
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu.
Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa
tifutifu na mfinyanzi.
vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba ili kuharakisha kukomaa unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya
kumwagilia kadri zao linavo kua.
Pia nivizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna mda kamili wa kukomaa na kuvuna
ni siku 90 hadi 150 kutokana na aina ya mbegu utakayo tumia.
KUDHIBITI MAGUGU NA MAGONJWA
Kitunguu ni zao lisilo weza kushindana na magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza
magonjwa na husababisha kudumaa kwa vitunguu.
Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia ya kutifulia kwa jembe dogo, kung'olea kwa mkono
na pia kwa kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu kwani
mizizi ya vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua.
Hakikisha kuwa mashina ya vitunguu vyako ndani ya udongo kama sentimita 5. Pia kuna aiina ya vitunguu utoa
tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokua.
natumaini kwa maelezo hayo mpenzi msomaji umepata mwanga kwa kilimo cha vitunguu usisite kunitafuta
0 Comments