KILIMO BORA CHA CHINESE CABBAGE
UTANGULIZI
Chinese cabbage ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania.asili yake ni china na badae likasambaa katika nchi za Ethipia,south africa,zimbabwe na Tanzania.
HALI YA HEWA
JOTOLIDI;Chinese cabbage linastawi na kukua
vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 hadi 22oc
Unyevunyevu; chinese cabbage ni zao linalo tegemea
umwagiliaji hivo linaitaji maji mengi
wakati wa ukuaji.
Udongo;chinese cabbage linakua vizuri kwenye
udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha
PH; 5.5 hadi 7.6
KUANDAA
SHAMBA
Udongo
unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au
machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.
KUANDAA
KITALU
Kitalu
kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yan sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani
sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka
nje ya kitalu.kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari
na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.
KUPANDA
Kwa kupanda
moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda
nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.
Na kwakupandikiza
hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na
chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.
MBOLEA
Kama
unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu
chenye mita 5
Na pia weka
mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea
unapofikia majani matano.
PALIZI
Tumia jembe
la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.
MAGONJWA NA
WADUDU WAALIBIFU
WADUDU
v Sota (bagrada bugs)
v Dudu mafuta(cabbage aphids)
v Minyoo ya chini(cut worm)
Tumia
chemicali za kuua wadudu kama vile ninja,
supercorn, wilcron na perfecron na
pia kuondoa magugu pamoja na mimea yenye wadudu
na pia weka shamba safi wakati wote.
MAGONJWA
v Ubuli unga(powdery meldew)
v Kuoza kwa mizizi(black rot)
v Rub root
Zuia kwa
kupanda mbegu safi na kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa.
KUVUNA
Chinese
ukomaa baada ya miezi 3 hadi 4 inategemea na aina
Vuna
kwa kung’oa kwa mkono au unaweza kutumia kisu kukata.
UTUNZAJI
Maisha
ya chinese ni mafupi hivyo unatakiwa kusafisha kwa kuosha na pia baada ya hapo
unaweza kutunza kwenye friji ili kuzuia
kukauka.
Post a Comment