KILIMO BORA CHA MICHUNGWA
UTANGULIZI.
Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukandawa
pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa
kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa
kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini
mwilini.
Hali
ya hewa.
Michungwa huweza kukuzwamaeneo yenye joto na hata yale
yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika
joto la nyuz ijoto 15.5c – 29c.
Kuandaa
mbegu.
Mchungwa kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka
katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha
mbegu zake na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.
Kuandaa
kitalu.
Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha
changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako
na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha mwagia maji kila siku na
baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kichipua, baada ya miche kufikia kiasi cha
sentimita 3 – 5, miche ihamishwe kwenye pakiti zenye udongo (viriba) wenye
mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi.
Kuunga
miche.
Miche ikifikia urefu wastani wa sentimita 30 – 45 huungwa
ili kupata michungwa. Kwa michungwa kuna aina mbili kuu hapa Tanzania ambazo ni
Jaffer na Valencia. Jaffer ni rahisi kuunga sababu vikonyo vyake ni vikubwa na
viko wazi kwenye miti, miti yake ni mikubwa na inazaa sanalakini huathirika
sana jua likiwa kali na matunda yake huanguka, pia machungwa yake hukua kwa
haraka sana ilasoko likiwa baya huishia
shambani kwa kuanguka. Vlencia ni miti ya wastani , vikonyo havipo wazi kwa hiyo
huwapa kazi waungaji (hawaipendi) ina uzao wa wastani na inakaribia ukame na
matunda yake hayaivi haraka.
Upandaji.
Baada ya uungaji kukubali unaweza kuandaa shamba lako kwa
kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kusubiri msimu wa mvua, miche ipandwe mara
tu baada ya mvua za kwanza kunyesha, umbali wa kupanda ni mita 8 * 8 kwa Jaffer
na mita 5 * 8 kwa Valencia.
Palizi
na matumizi ya mbolea.
Palizi ifanyike si chini ya mara 2 – 4 kwa mwaka na miche
ikifikisha miaka 3 unaweza ukasafishia miaka mitatu unaweza ukasafishia
visahani na kufyeka sehemu nyingine. Kwenye mbolea weka samadi iliyoiva debe
moja hadi mbili kwa shimo, changanya mbolea na udongo wa kwanza kutoka shimoni,
iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK na Mijingu Phosphate
changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top soil).
Uzao.
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza kutoa maua na kuzaa na
huchanganya kuzaa baada yamiaka mitano, miche huendelea kuzaa hadi kufikia
miaka mitano 25 – 30 tangu kupandwa.
Magonjwa
na wadudu katika michungwa.
Magonjwa.
1.Vidonda
katika shina.
Huletwa na aina fulani ya ukungu. Dalili za ugonjwa huu
nikutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Dalili;
Huongezeka ukubwa na baadae kutoa utomvu.
Kudhibitisha;
Hutokea
sana sehemu iliyo na udongo ambao huatamisha maji.
2.
Ugonjwa wa kukauka miti.
Husababishwa na virusi ambavyo husambazwa na chawa weusi.
Dalili;
Sehemu ya shina hunyauka na ndani yake hutokea mipasuko pasuko,kasha mmea
hudhoofika polepole na kutoa matunda madogo madogo, na majani hubadilika ghafla
na kuwa ya njano.
3.Ugonjwa
wa kutobadilika rangi kwa machungwa yanapokomaa.
Hutokea hasa kwenye sehemu za miinuko ya kati na
kusambazwa na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa kuchukua vikonyo na
kubebeshea kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za ugonjwa.
Dalili;
Hutokea mabaka ya njano kwenye majani, pia matunda huwa ya ukali nay a njano
sana.
KUZUIA:
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza kutokea angalia wadudu kama
chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche kwenye kitalu. Wakiwepo,
majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu ya juu. Vilevile epuka
kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za ugonjwa huu.
WADUDU:
1.Nzi
weupe (white fly).
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye majani
ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, na hii husababisha mmea
kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Njia ya kiusalama zaidi ni kwa
kupandisha shambani wadudu aina ya Cales noacki ambao huwala hawa nzi
weupe na kuzuia kusambaa kwao.
2.Wadudu
mafuta (aphids).
Hawa ni wadudu weusi ambao hukaa kwenye
majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, nah ii pia
husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Tumia kiuwa wadudu (insectside).
Kuvuna
Mchungwa huwa tayari kuvunwa miezi 3 – 4
baada ya kupandwa. Kuvuna ni kwa njia ya mikono au kwa kutumia kikapu cha
kuvunia.
Hifadhi
Machungwa huhifadhiwa kwenye ghala safi
lenye kuruhusu hewa. Ghala lijengwe nje ili kuruhusu hewa safi ili yasioze.
Soko
Soko la ndani na nje ya nchi lipo. Kiasi
kikubwa cha machungwa hutumika hapa nchini, pia huuzwa nchi za jirani. Bei ya
chungwa ni shilling 200 – 300 kwa kila moja na hadi 500 hufikia kulingana na
aina ya msimu.
Hitimisho
Ili kupata mmea wa mchungwa kama tunda
ambalo linanunuliwa, huna budi kuitunza mbegu hiyo kwenye unyevunyevu kasha tu
baada yaya kuzitunza kwenye tunda na kuziotesha katikahali ya unyevu; na pindi
mmea uchipuapo hapo ukapandwe kwenye udongo kusudiwa.
Post a Comment