KILIMO BORA CHA CARROT

UTANGULIZI
Carrot ni moja ya mazao ya mbogamboga iliyo katika jamii ya mazao ya mizizi, pia ni zao ambalo linalimwa sana nchini japo kua asili yake ni nchini Ulaya na kusini mwa Asia.
Kwa hapa nchini carrot inalimwa sana  katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Kagera na Kilimanjaro.
na utumika kama kiungo kwenye mboga, juice, kutengeneza mafuta na vipodozi na pia utafunwa na pia ni chanzo cha vitamin A na C.

UDONGO NA HALI YA HEWA
carrot usitawi vizuri kwneye maeneo yenye nyuzi joto 15- 27 napia usitawi vizuri kwenye udongo wa tifutifu na kichanga, udongo mfinyazi haufai kwa kilimo cha carrot kwakua hudumaza carrot.
    


KUANDAA SHAMBA
kama mazao mengine shamba linatakiwa liandaliwe mapema kwa kutumia trekta,jembe la mkono au jembe la ng'ombe na lisawazishwe vizuri na kutolewa uchafu wote.
  • tifua udongo urefu  wa cm 30-45 kwenda 
  • tengeneza matuta yenye mwinuko wa cm 28-  40 
  • matuta yawe na upanda wa m1 
  • umbali kati ya tuta na tuta uwe ni m1.5 
UPANDAJI 
Carrot inaweza kupandwa moja kwa moja au kwa kitaru kisha kuamishiwa shambani pale mimea inapo chipua vizuri
  • changanya mbengu na mchanga ili kuwezesha mbegu kuto ondolewa na upepo
  • tengeneza mifereji yenye umbali wa cm 15 had 20 ndani ya tuta
  • weka mbegu zako ndani ya mifereji kwa kutumia kopo lililo kwatwa kwenye mfuniko
  • funika mbegu kwa kutumia mchanga au samadi
  • mwagirizia vizuri matuta yako ili kuakikisha kunakua na unyevu wa kutosha ndani ya  tuta
  • funika tuta lako kwa sandarusi lenye rangi nyeusi ili kuwezesha kua na joto ya kutosha
  • funua na angalia  siku ya tatu na kama miche imeanza kutokeza ondoa sandarusi lako na usifunike tena.
MBOLEA
Unaweza kutumia mbolea ya samadi au ya kiwandani
  • weka mbolea ya SA kilo 100 kwa hekta wakati wa kupanda au kilo 50 kama ulitumia mbolea ya samadi
  • baada ya wiki 6 toka umepanda weka mbolea ya NPK
  • Na unaweza kutumia mbolea ya maji kila baada ya wiki mbili 
  PALIZI
Palizi ni muhimu sana ili kuweza kupata mazao mengi 
unaweza kupalilia kwa kutumia jembe la mkono au kwa kungorea kutokana na uwezo wako na pia palilia pale tu unapo ona magugu yameanza shambani.

KUVUNA
carrot hua tayari kuvunwa kuanzia wiki 11 toka siku inapandwa.
httpp//;www.tanzanianakilimo.blogspot.com
MAGONJWA NA WADUDU WAHALIBIFU
 
WADUDU
  • Imi wa karoti
  • minyoo fundo
MAGONJWA
  •  Madoa jani
  • kuoza miziz
  • mabaka meusi
tumia dawa ya kuua wadudu mfano sapa diazinon ili kuuwa wadudud
na tumia dawa za magonjwa kama vile kocide,champion na anthrocal ili kupambana na magonjwa 
 

Post a Comment

0 Comments