Mpenzi msomaji wa blog hii leo napenda nikuletee kitu kingine tofauti kidogo na ambacho blog nyingi za kilimo, ntapenda kukuletea baadhi ya vifaa ambavyo hutumika shambani hivyo wewe kama mkulima, mdau wa kilimo au mtu yoyote na ungependa kufahamu zaidi kuhusu mashine na vifaa vinavyo tumika shambani usisite kuwasiliana na mimi kwa kubofya hapa.
TRACTOR |
Tractor ni moja kati ya mashine ambazo ni maalufu sana, bila shaka kila mmoja ameshawahi kuliona, wengi wanaweza wakawa hawafahamu nini hasa kazi za tractor.pia tractor hutofautiana kwa umbile, wats na hata ubora.
- hutumika kama usafiri kwa mizigo na watu pia
- hutumika kama chanzo cha umeme sambani mfano mashine za kusaga zinaweza kuunganishwa na kufanya kazi
- hutumika kuunganisha vifaa tofauti tofauti vinavo tumiwa shambani mfano plough.
jifunze zaidi kwa kubofya hapa
𝐓
HALLOW |
hiki kinaweza kua kifaa kigeni kwa watu ambao hawafahamu mambo ya shamba hasa, lakini ni kifaa maarufu kwa wakulima. hallow hua na disc ya maumbo tofauti na hutumika baada ya disc plough. kazi yake hasa ni
- kusawazisha shamba.
- kuchanganya udongo na mbolea
- kuruhusu udongo kua katika hali nzuri inayo ruhusu, maji na hewa kupenya ndani ya udongo.
|
corn seeder nikifaa ambacho hutumika kupandia mahindi, kifaa hiki hua
hakitumii umeme au mafuta ili hufanya kazi kwa kuunganishwa katika power
tiller. hua si kukubwa sana kwa umbo na nirahisi kuhamishika na hata
kusafisha.
FARM TRAILER |
Hiki ni kifaa ambacho ni maalufu sana, farm trailer ni tela kama inavofahamika na wengi. kazi yake kubwa ni kubeba mizigo, mazao na hata watu. na hua maalumu kwaajili ya matumizi ya shamba na hata shuguri zingine za kiuchumi na kijamii pia. na huvutwa kwa kutumia tractor.
jifunze mambo mengi zaidi kwa kubofya HAPA
MAIZE DRYER |
Maize dryer kama inavo itwa hua nikifaa maalumu ambacho kimetengenezwa ili kukausha maindi baada ya kuvunwa.
BOOM SPLAYER |
Boom sprayer hua ni kifaa ambacho kimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kupulizia viuagugu au viua dudu shambani. na hua na mfano kama splayer zinazo tumika kiupulizia dawa za kuua kupe kwa wanyama, ila tofauti yake ni kwamba boom sprayer hua ni kubwa sana na huvutwa kwa kutumia tractor. hivyo utumika kupulizia dawa katika mashamba. boom spalayer hua na ukubwa tofauti tofauti mfano zingine huchukua 300 liters, 600 liter n.k
COMBINE HARVESTER |
Hii ni mashine ya shamba na hua na umbo kubwa mfano wa scaveter na hutumika katika kuvuna mazao mbali mbali mfano mpunga na ngano.
DISC PLOUGH |
Disc plough pia hufanya kazi kwa kuunganishwa katika trekta, hutumika katika kuvunjavunja udongo ulio katika hali ngumu.
POWER TILLER |
Hii pia nimashine maalufu sana, imekua ikitumika katika maeneo mengi tofauti tofauti na hua nakazi nyingi kama ilivyo trekta
- usafirishaji
- hutumika kulima
- chanzo cha umeme pia
Bila shaka umeza kufahamu baadhi ya vifaa vinavyo tumika shambani na kazi zake, nitumaini kangu umeapata uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya vifaa hivyo.
japo imekua nichangamoto sana kwa wakulima jinsi ya kupata vifaa hivyo kutokana na upatikanaji mdogo wa vifaa hivyo.
hivyo wewe kama muuzaji au msambazaji wa vifaaa mbalimbali ni fursa kwako sasa kuweza kuweza kuonesha au kujulisha wa kulima jinsi ya kuvipata vifaa hivyo kupitia kwako.
WASILIANA NA MIMI MOJA KWA MOJA ili tuweze kulisukuma gurudumu la maendeleo ya kilimo.
0 Comments