Mkuu
 wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (wapili kulia) baada ya kupewa 
zawadi ya nguo ya jadi na wafugaji wa kata ya Naisinyai kwenye ziara 
yake Wilayani Simanjiro, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania 
Chaula na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro 
Jackson Leskar Sipitieck na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Arnold 
Msuya. 
Ng'ombe
 341,098 wamepigwa chapa Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ili 
kutekeleza agizo la Serikali la upigaji chapa mifugo kwa ajili ya 
utambuzi na kuepuka migogoro ya mara kwa mara. 
Katibu
 Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary, aliyasema hayo juzi wakati 
akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti. Omary
 alisema lengo la wilaya hiyo ni kupiga chapa ng'ombe 437,925 hivyo 
wamefikia asilimia 79 hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana. 
Alisema
 zoezi hilo lilitarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka jana ila baada 
ya serikali kuongeza muda hadi Januari 31 mwaka huu, watakuwa 
wamefanikiwa kukamilisha. Alisema
 wilaya hiyo ina mabwawa mawili ya Nyumba ya Mungu na Kidapash, ambayo 
shughuli za uvuvi zinafanyika na jitihada za kudhibiti uvuvi haramu 
zimefanyika. 
Kwenye
 sekta ya kilimo, umwagiliaji na ushirika alisema kuna ekari 346,000 
zinazofaa kwa kilimo ambapo takribani ekari 144,00 hutumika kwa kilimo 
cha mazao ya chakula na biashara. "Mahitaji
 ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wote ni tani 42,000 za nafaka na hali 
ya chakula ni ya kuridhisha kwenye maeneo mengi kwani wananchi wanatumia
 chakula kilichovunwa msimu wa Kilimo wa 2016/2017. 
Alisema
 kwa upande wa mradi wa maji kutoka mto Ruvu hadi mji mdogo wa 
Orkesumet, serikali itautekeleza kupitia sh40 bilioni, za fedha za ndani
 na ufadhili wa benki ya maendeleo ya watu wa uarabuni. Mkuu
 wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti aliagiza kila wilaya ya mkoa huo 
kuhakikisha inakuwa na viwanda 15 ili kutekeleza agizo la serikali la 
kila mkoa uwe na viwanda 100.
Mnyeti
 alisema wilaya ya Simanjiro iwe na viwanda 15 na nyingine zitekeleze 
hilo ili kuhakikisha uzalishaji wa ajira unafanyika na kufikia lengo la 
kuwa na uchumi wa kati.


write your comment here