VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VYAAGIZWA KUANZA KAZI IFIKABU JULAI
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu
wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi
Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi
maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi
akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele)
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya
ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika
Wilaya ya Butiama leo.
Mkuu
wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu
haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani
Musoma leo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa
kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la
kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi
haramu Kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akisoma majina ya Wavuvi
Haramu
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata
samaki na mazao yake vilivyofungwa katika Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza
kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki
kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua kabla ya kufikia mwezi
Machi mwaka wizarani kwake.
Alivitaja
viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited
vilivyopo Mwanza na Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited
katika mkoa wa Mara.Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa
kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum
ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi
kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.
“Mimi
kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda
raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba ulinzi wa raslimali hizi ni wa
kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha hapa nchini”
alisisitiza Mpina
Waziri
Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya
Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki
katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu
zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi
linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.
Kamanda
anayeongoza kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na
utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alimweleza
Waziri Mpina kuwa operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma,
Butiama, Rorya na Bunda na kufanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu
zenye thamani ya sh. bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa
samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya sh.
milioni 189.
Waziri
Mpina aliziagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua Maafisa Uvuvi
wa Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu
kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na
ikithibitika wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vincent Anney amesema kwamba hayuko tayari
kuona Wilaya yake inaendelea kuishi na watumishi wanaojihusisha na
uvuvi haramu na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni
pamoja na kuwaondoa katika wilaya hiyo.
Aidha
Waziri Mpina ameiagiza Wizara yake kuandaa bei elekezi ya kununua samaki
itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha hovyo bei
pindi samaki wanapoongezeka na hivyo kuwadhulumu wavuvi kupata malipo
stahili yanayotokana na kazi yao.Waziri Mpina alisema Ziwa Victoria ni
hazina na raslimali kubwa kwa Tanzania ambapo inaaminika kuwa ni la
kwanza kwa ukubwa katika bara la Afrika kwa kuwa na eneo la 68,000Km2 na
la pili duniani.
Alisema
pamoja na umuhimu wa ziwa hili katika kukuza uchumi na kuboresha maisha
ya watanzania bado linakabiliwa na shughuli za uvuvi haramu uliokithiri
ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kama hakutakuwa na jitihada za haraka
za kutokomeza uvuvi haramu, ziwa hilo hali halitakuwa na raslimali za
uvuvi ikiwa ni pamoja na samaki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Alitaja
uvuvi haramu unaofanywa kuwa ni pamoja na kuvua katika maeneo
yasiyoruhusiwa, kutumia valiyombo visivyosajiliwa, kuvua bila
leseni,kutumia sumu, kutumia nyavu za utali na kuvua samaki wachanga ama
wazazi wasioruhusiwa.
Uvuvi
haramu mwingini nikuvua kwa kokoro na nyavu zenye macho madogo chini ya
kiwango kinachokubalika kisheria, katuli, kumbakumba na gizagiza ambapo
alisema Serikali imedhamilia kutokomeza uvuvi huo haramu.
Aidha
alisema operesheni hiyo katika kanda ya Ziwa Victoria dhidi ya uvuvi
haramu ni ya kudumu na inafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na.22
yaMwaka 2003 na Kanuni 58(1) ya Uvuvi ya Mwaka 2009 na Sheria ya
Mazingira Na 20 ya Mwaka 2004 kifungu Na(1), 65(1)a pia Sheria ya
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na 29 ya Mwaka 1994 ili kudhibiti
uvuvi haramu ulioshamiri kiasi cha kutoweka kwa raslimali ya samaki
katika ziwa hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.
Waziri
Mpina alisema Tanzania inamiliki 51% ya Ziwa hili ikifuatiwa na Uganda
43% na nchi ya Kenya inamiliki 6%. Ziwa hili ni moja ya maziwa
yanayozalisha samaki kwa wingi duniani kwa makadirio ya takribani tani
1,000,000 kwa mwaka ambapo asilimia 60 ya uzalishaji wa samaki wake
unatoka Tanzania hivyo juhudi za pamoja za kutokomeza uvuvi haramu
zinahitajika.
Post a Comment