JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU SEHEMU YA PILI(2)
Ndugu mpenzi msomaji wa blog yetu, tunaendele na somo letu ambalo tulilianza hapo hawali. Na leo tutapenda kuzuanza na;
BOFYA HAPA KAMA ULIPITWA NA SOMO LA NYUMA
VYOMBO VINAVOTAKIWA KUWEKWA KENYE BANDA LA VIFARANGA
- .VITALU,Vifaranga hutunzwa ndani ya kitalu kilichotengenezwa kwa mbao au karatasi ngumu zinazotumika kujengea dari. Au katika mazingira ya kijijini unaweza kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia. Upana wake uwiane na wingi wa vifaranga ulionao na kina chake kama mita moja. Ukuta wake uwe na tabaka mbili za magunia hayo zilizoachana kwa nafasi ya inchi tatu au nne. Katikati ya nafasi hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za mpunga. Tayari utakuwa umepata kitalu cha kulelea vifaranga.Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.
- . TAA YA CHEMLI. Kutegemeana na hali ya hewa taa moja ya chemli inaweza kulea vifaranga 50 au zaidi. Hakikisha kuwa unayo akiba ya mafuta ya taa ya kutosha, vioo, utambi n.k. Taa moja hutumia debe moja la mafuta ya taa kwa muda wa siku 16 hadi 20. Unashauriwa uweke mafuta kwenye taa asubuhi na kukagua jioni kama yanatosha kwa sababu taa ikizimika usiku utapata hasara ya vifo kwa vifaranga kujikusanya na kukosa hewa .Weka mafuta ya kutosha lakini usijaze taa. Joto la taa za chemli hurekebisha kwa kupandisha au kushusha utambi pia kuongeza au kupunguza idadi ya taa.
- JIKO LA MKAA, Jiko la mkaa linaweza kutumika badala ya taa kwa ajili ya kuwapa vifaranga joto. Unapotumia jiko la mkaa ni hakikisha kwamba mkaa unaotumia hautoi moshi na chumba kinapitisha hewa safi na ya kutosha. Pia jiko liwekwe juu ya matofaili ili kuzuia vifaranga wasiliguse.
- MWANVULI, Mfugaji akimudu anaweza kutengeneza mwamvuli wa kuning’inia juu ya kitalu cha kulea vifaranga kwa kutumia makaratasi magumu ya “hardboard”. Mwamvuli unasaidia kupunguza upotevu wa joto na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya taa. Kwenye mwamvuli wa duara toboa tundu moja ili kupitisha hewa yenye joto. Angalia mviringo wa mwamvuli wako uwiane na ukubwa wa kitalu chako. Ili kuwapa vifaranga uhuru wa kufuata au kuepuka joto. Ni lazima mwamvuli uwekwe juu ya matofali na kila juma inabidi uinuliwe juu kiasi cha cm 5 (inchi 2, kufuatana na hali ya hewa.
- VYOMBO VYA CHAKULA (Vihori) ,Ili vifaranga wakue vizuri vyombo vya chakula lazima viwafae. Vipimo pamoja na idadi ya vyombo vya chakula ni vya muhimu viwatosheleze. Chombo chenye urefu wa (futi 3 x inch 3) kinatosha vifaranga 100. Ukitumia mbao kutengeneza vyombo vya chakula unashauriwa mbao ziwe unene wa cm 1/25 (inchi ½). Pia, unaweza kutumia sahani za kawaida unazotumia nyumbani kuwawekea vifaranga chakula.
- VYOMBO VYA MAJI, Chombo chochote chenye kina kifupi kinafaa kwa kuwayweshea kuku ila budi kiinuliwe ili vifaranga wasiweze kuingiza takataka za chini kwenye maji. Pia kama ni cha wazi maji yawekewe changarawe safi kabisa ili kuzuia vifaranga wasiloane maji. Au tumia sahani na makopokama ifuatavyo. Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza maji katika kopo halafu lifunike kwa sahani na ligeuze. Kinywesheo cha vifaranga
Bila shaka mpenzi msomaji umepata kitu mpaka hapo na usisite kuendelea kua nasi likufahamu mengi zaidi.
+255764148221 EMAIL rubabaimani@gmail.com
Post a Comment