WAKULIMA WANATAKIWA KUACHAMABAKI YA MAZAO SHAMBANI ILI KUONGEZA RUTUBA
Anga
jeupe na jua likiwaka katika milima kijani yenye miinuko mikali katika
maeneo ya mlima Meru kaskazini mwa Tanzania. Mkulima Bi. Felix Nassari
akiangalia kama mabua ya mahindi ya msimu uliopita kama yameoza vizuri
shambani ili ajiandae kupanda karoti kwa msimu huu. Anasema, “Kabla
sijapanda ninaacha mabaki ya mazao ya msimu uliopita yaoze shambani.”
Mama wa-miaka-32 na binti yake wa-miaka-sita wanaishi kijiji cha
Ndoombo katika njanda za juu za Meru, kama kilomita 40 kutoka mji wa
Arusha. Katika eneo hili wakulima wengi wanalima kilimo hifadhi ili
kukabiliana na mmomonyoko wa udongo kama anavyofanya Bi. Nassari. Hii
inawawezesha wakulima wanaoishi katika maeneo haya yenye mteremko mkali
na yanayokumbwa na mmomonyoko wa udongo kutokana na mafuriko yatokayo
milimani kuweza kulima.
Bi. Nassari analima na kubadilisha mahindi, kabichi, viazi, na karoti
katika shamba lake la hekari mbili. Baada ya kuvuna mahindi anaacha
mabua kuoza na kuwa mbolea shambani.
Pia anatengeneza matuta na kwa umakini anatumia jembe lake la mkono
kupiga mashimo shambani. Hii unasaidia kuepuka kumomonyoka kwa udongo wa
juu wenye rutuba. Anaelezea: “Ninatengeneza matuta [katika kila
sentimita 70 kwenye miteremko] kupunguza kasi ya maji shambani, na nina
panda kwa kutumia jembe la mkono. Nina epuka kuchimba mashimo marefu
kuepuka kutengeneza mitaro ya maji.”
Sheilah Yusuf ni afisa ugani katika eneo hili. Alipoanza kufanya kazi
miezi 18 iliyopita katika maeneo haya ya miteremko, alishangaa sana
jinsi wakulima wanavyoweza kuzalisha katika eneo hili.
Anasema: “Kwa mara yangu ya kwanza kutembelea mashambani,
nilishangazwa sana jinsi wakulima wanavyoweza kuzalisha katika maeneo
haya ya miinuko mikali ya miteremko. Kwa miaka mingi wamejifunza wenyewe
jinsi ya kutunza ardhi yao.”
Bi. Yusuf anasema, katika maeneo ya miteremko mikali ya meru wakulima
wamekuwawakilima kiliomo hifadhi kwa miaka mingi kukabiliana na
mmomonyoko wa udongo. Mbinu hizi ni pamoja na kutengeneza matuta,
kukwatua kwa kina kidogo, kilimo mseto na kilomo mzunguko, na kuacha
mazao kuoza shambani baada ya mavuno.
Julius Naftari Nasari analima katika hekari tatu, anachanganya
mahindi na maharage na baada ya kuvuna mahindi yake anapanda karoti na
viazi.
Bw. Nasari anasema anapendelea kulima kwa jembe la mkoni ili
asisumbue muundo wa udongo. Ansema kulima kwa jembe la mkono ni rahisi
kuliko kulima kwa trekta kwasababu ni vigumu kupandisha trekta katika
miinuko.
Anaongeza: “Mashamba yako katika miteremko mikali, wakati wa kipindi
cha mvua shamba lako linabidi liwe na udongo mzuri wenye uwezo wa
kukinga mmomonyoko; kinyume na hapo, rutuba yote itachukuliwa na
mafuriko.”
Bw. Nasari anapalilia kwa mikono na anaongeza mboji shambani kuboresha udongo.
Lakini Bw. Nasari ansema mbinu hizi zinahitaji vibarua. Anaelezea:
“Inachukua muda mrefu kupalilia kwamikono, kupanda kwa kutumia jembe la
mkono, na inagharimu kuongeza mbolea juu ya majani ili kuboresha udongo.
Lakini hii ni namna pekee ambayo tunaweza kulima na kuvuna katika eneo
hili.”
Kulingana na Bw. Nasari, siri ya kuweza kupata mavuno mazuri katika
eneo hili ni kutunza ardhi. Ansema sikuzote wanunuzi wanaokuja kununua
mazao katika maeneo haya wanashangazwa sana jinsi wakulima wanavyoweza
kulima vizuri katika maeneo haya ya muinuko yenye miteremko mikali.
Wanunuzi wanalazimika kuacha magari yao barabarani na kubeba magunia ya
mazao begani kupeleka kwenye gari kwasababu magari hayawezi kupanda
milimani.
Mbali na changamoto katika miinuko hii, Bw. Nasari anasema kwa miaka
mingi wakulima katika maeneo haya wameweza kuzalisha mazao mengi ambayo
yanauzwa masoko ya karibu na mengine yakiuzwa mpaka Arusha mjini.
Bw. Nassari anasema, kwa kutumia mbinu kama kulima kwa kina kifupi na
kiacha mabaki ya mazao kuoza shambani kumemsaidia kuboresha udongo.
Msimu uliopita Bi. Nassari alivuna gunia 40 za karoti na gunia 50 za
viazi mviringo, kila guni lina ujazo wa kilo 100. Anauza karoti kwa
shilingi 500-700 (sawa na dola US$0.22-0.31) kwa kilo, na na viazi kwa
800 shillingi (sawa na dola US$0.35) kwa kilo.
Anasema, kupitia kilimo, amemsaidia mume wake kujenga nyumba nzuri
yenye bati. Kwa kuongezea sasa wanamaji ya uhakika nyumbani kwao.
Kazi hii imefanywa na msaada wa Canadian Foodgrains Bank kama
sehemu ya mradi, “Kilimo hifadhi kujenga usatahimili, kilimo cha kisasa
cha kuzingatia hali ya mazingira.” Kazi hii imefadhiliwa na serikali ya
Canada, kupitia Global Affairs Canada, www.international.gc.ca.
Post a Comment