UTANGULIZI
Zao la mpunga linazalishwa na
nchi zipatazo 40 za Afrika, umuhimu wa zao hili umekuwa ukiongezeka kwa kasi
kubwa kuliko mazao mengine ya chakula kwa sasa. Mpunga umechukua nafasi ya pili
kwa chakula aina ya nafaka baada ya mahindi, katika nchi nyingine kama zile za
kaskazini mwa Afrika mpunga unachukua nafasi ya kwanza. Kwa muktadha huo taasisi za utafiti wa mazao
ya kilimo Afrika na Dunia kwa ujumla wameanza kufanya tafiti mbalimbali na
kuzalisha aina kadhaa za mbegu bora ya mpunga zinazoweza kupatikana kwa
wakulima.
Katika bara la Afrika mpunga unalimwa
sana magharibi mwa bara 42%, kaskazini 23%, kati 1.2% na kusini karibu 1%. Nchi
zinazolima mpunga ni Benin, Burkina, Cameroon, Demokrasia ya Kongo, Kongo,
Chad, Ivory Coast, Gabon, Gambia,
Guinea, na Bissau, Madagascar, Mali, Mauritania, Senegal, Togo,Nigeria, Liberia,
Sierra Leone, Misri, Tanzania, Kenya, Ruanda na Uganda.
Karibu 75% ya mpunga katika bara la Afrika unazalishwa
na wakulima wadogo wanaozalisha wastani wa chini ya tani 2 kwa hekta, kwenye
maeneo ya umwagiliaji chini ya 11% ya ardhi inayoliwa barani Afrika.
Ukanda wa Afrika ya Mashariki
mpunga unaopatikana ni 58% tu ya mahitaji. Wastani wa mavuno ya mpunga kwa
hekta nchini Tanzania ni tani 2.4 Kuna umuhimu wa kupata mbegu itakayowezesha
wakulima kupata mpunga wa kutosha na kulingana na matakwa yanayokusudiwa na
mkulima kujitosheleza kwa chakula na ziada kuweza kumsaidia kupata mahitaji
yake baada ya kuuza.
MBEGU DUNI YA MPUNGA
HUSABABISHA MAVUNO HABA
Kinachosababisha wakulima
kutopata mavuno mengi kwa kifupi ni matumizi ya mbegu duni zinazotoa mavuno
haba, sababu nyingine ni matumizi kidogo ya mbolea, teknolojia duni ya
uzalishaji na uhaba wa maji. Kuhusu tatizo hili la mbegu duni inaonekana tatizo
hilo limeanza kushughulikiwa kama nilivyotangulia kueleza hapo awali, kuhusu
jitihada zinazofanywa na taasisi za utafiti ili kutoa mbegu zinazoweza
kumsaidia mkulima kuongeza uzalishaji zinahitajika kupata muunganiko wa taarifa
na maarifa ili kukidhi matakwa ya wakulima na kuzikubali kwa kuwa wakulima wamekuwa
na matakwa yao ya kuchagua mbegu kwa kuzingatia ladha, harufu na muonekano wake bila kujali
kiasi cha mavuno kinachopatikana. Kama kutakuwepo njia za kuwaaminisha na
kuwafanya waanze kuzitumia mbegu bora zilizozalishwa na ambazo zinatoa mavuno
mengi, zenye ukinzani dhidi ya wadudu na magonjwa, zenye kuvumilia ukame, hali
ya hewa, kukomaa haraka, zenye faida za lishe, na kuwa na ubora unaokidhi
mahitaji ya soko (mlaji), kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza mavuno katika zao
hilo na kuwafanya wakulima wajitosheleze kwa chakula na ziada kuweza kuuza na
kuongeza kipato kuboresha hali ya uchumi katika familia zao kama wataweza pia
kuboresha mbegu zao za asili wanazozotumia sasa.
MBINU ZA KUCHAGUA MBEGU
BORA YA MPUNGA SHAMBANI
Mkulima, Afisa Ugani na wadau
wengine wa kilimo kwa kuzingatia muongozo huu mfupi wataweza kuboresha mbegu
hasa zile ambazo zinaonekana kuanza kuchanganyika na mbegu nyingine na kupoteza
sifa zake za awali kwa kuzingatia hatua zifuatazo:
Chagua moja au baadhi ya mbegu
ulizonazo unazotaka kuziboresha wewe mwenyewe kwa kuzingatia mwongozo ufuatavyo:
·
Mbegu ikisha chaguliwa katika msimu wa kwanza ipandwe
tena na utaratibu wa kutunza mbegu uliotumka mara ya kwanza ufuatwe katika
hatua zote kama inavyoelezwa katika jedwali hapo chini.
·
Mbegu itatambuliwa kuwa ni bora nakuthibitishwa
baada ya kupitia hatua za kuchaguliwa na kupandwa kwa misimu mitatu hadi minne
mfululizo kwa kuzingatia hatua na vigezo vilivyotajwa hapo chini.
·
Mkulima na wa wadau wa mbegu wataipitisha mbegu
yao kuwa ni nzuri na kuithibitisha pale watakapo ridhika na muonekano wake na
ufanisi waliokuwa wanatarajia kutoka katika mbegu hiyo, mfano uotaji na
uchanuaji wa sawia, mashine manene na imara, wingi na ujazo wa masuke, ukomaaji
wa sawia, upungufu wa mapepe, rangi na umbo zuri la punje uliosawa, mimea na
mazao yasiyo shambuliwa na magonjwa.
VIGEZO NA HATUA ZA KUFUATA KUPATA MBEGU ILIYOTHIBITISHWA NGAZI YA WAKULIMA
AU JAMII
NB:
uchaguzi wa mbegu shambani ubora uzingatiwe hasa katika siku ya 100 hadi 120.
Uchaguzi wa mbegu wakati wa kuvuna na kwenye
ghala, uanze wakati wa kuvuna, kuanika, kupembua hadi kuhifadhi.
|
UCHAGUZI
WA MBEGU YENYE VIGEZO VYA MBEGU ILIYOTHIBITISHWA
|
|||
GHALANI
AU KABLA YA KUPANDA
|
SHAMBANI
WAKATI WA UZALISHAJI
|
|||
TABIA
|
UAMUZI
|
TABIA
|
UAMUZI
|
|
Ya miezi 3 hadi 6
|
Itenge inafaa
|
Fupi kuliko nyingine
|
Ing’olewe hima
|
|
Ya zaidi ya miezi 6
|
Usiitumie
|
Ndefu kuliko nyingine
|
Ing’olewe hima
|
|
Yenye ukungu
|
Usiitumie
|
Nyembamba mno
|
Ing’olewe hima
|
|
Rangi mchanganyiko
|
Usiitumie
|
Nene kupita kiasi
|
Ing’olewe hima
|
|
Umbo mbalimbali
|
Usiitumie
|
Majani membamba
|
Ing’olewe hima
|
|
Iliyo vunjika vunjika
|
Usiitumie
|
Majani mapana sana
|
Ing’olewe hima
|
|
Inayonukia
|
Itenge, nzuri
|
Inayonukia
|
Iache iote shambani
|
|
Yenye uzito mkubwa
|
Itenge, “
|
Yenye masuke mengi
|
Iache iote shambani
|
|
Yenye punje nyeupe
|
Itenge, “
|
Yenye masuke imara
|
Iache iote shambani
|
|
Punje zilizojaa
|
Itenge, “
|
Majani mafupi, wima
|
Iache iote shambani
|
|
Iliyokauka vizuri
|
Itenge, “
|
Isiyoathirika na jua
|
Iache iote shambani
|
|
Isiyo na mapepe
|
Itenge, “
|
inayokubali mazingira
|
Iache iote shambani
|
|
Isiyochanganyika
|
Itenge, “
|
inayoota sawa na zote
|
Iache iote shambani
|
|
Isiyo na ugonjwa
|
Itenge, “
|
Isiyoathirika/ ugonjwa
|
Iache iote shambani
|
|
Isiyo na wadudu
|
Itenge, “
|
Isiyoathirika/ wadudu
|
Iache iote shambani
|
MBEGU ILIYOTHIBITISHWA
Itakuwa ni ile iliyochaguliwa na
kutengenezwa na wakulima wenyewe kwa kuzingatia mwenendo wa zao hilo shambani
katika kila hatua ya uotaji. Mbegu hiyo itakuwa ni ile iliyobaki baada ya kuondolewa
makando na kasoro zinazoweza kuathiri ufanisi wa mbegu mfano mbegu dhaifu, zilizodumaa,
zilizoshambuliwa na magonjwa na wadudu, zinazo refuka kuliko zingine,
zilizofupi kuliko zingine, zenye rangi tofauti, zenye maumbo na tabia tofauti
na tabia za jumla za zao husika la mpunga.
Mbegu itathibitishwa na wakulima
kuwa ni bora endapo itarejea sifa yake ya awali kama kuwa na uotaji
unaolingana, kufanana kwa kila hali, rangi, umbo, ladha na harufu nzuri, uzao
mkubwa, uimara wa suke na ukinzani idhidi ya magonjwa, ukame, hali ya hewa nk.
NB;
Uthibitisho huo hautawahusu
wakulima wengine wasiohusika na mchakato wa kuthibitisha mbegu hiyo na wala wakulima
waliohusika hawatakuwa na dhamana ya kudai haki ya kuwa watengenezaji wa mbegu hiyo,
wakulima wengine wanaweza kuitumia mbegu hiyo na kukubaliana na matokeo na
ufanisi wa mbegu hiyo kulingana na maelezo ya wakulima waliohusika na mchakato
wakuthibitisha mbegu hiyo.
Aidha, mbegu hiyo haitahusishwa
na mbegu nyingine zinazo zalishwa kwa kuzingatia hatua za kisayansi. (seed
breeding, varietal seed selection, etc) bali ichukuliwe kama njia ya kuboresha
mbegu ya wakulima wa eneo hilo tu, (Improving seed quality).
Nawatakia kilimo chema chenye
tija na kinachotosheleza haja zenu,. Tunaweza kuwasiliana kwenye mtandao kwa
kutumia nywila iliyopo hapo chini. Ahsante sana!
Makala hii imeandikwa na kuandaliwa na
Gift Mayagila.
Mto wa Mbu, Monduli- Arusha.
Giftgogo70@yahoo.com
Imeletwa kwenu na mtandao ulio jikita katika kusaidia wakulima na wafugaji wadogo wadogo
IMANI LUBABA
rubabaimani@gmail.com
+255764148221
Usiache kutembele Channel yetu, ili kupata elimu zaidi kwa kubofya picha juu, na pia subscribe ili kua karibu nasi zaidi.
na unaweza kujiunga na blog yet.
BOFYA HAPA KAMA ULIPITWA NA MAKALA HII
BOFYA HAPA KAMA ULIPITWA NA MAKALA HII
0 Comments