Serikali yawaunga mkono wakulima kukataa bei ya korosho, yasitisha mnada+



Jana 26 October 26, 2018 Serikali imewaunga mkono wakulima kukataa kuuza Korosho zao kwa bei ndogo na imesitisha minada yote hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Katika hatua nyingine Wizara ya Kilimo imetakiwa kujitathimini na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho ametakiwa kurudishwa Wizarani huku wanaobaki wakitakiwa kuendelea na majukumu yao kwa nguvu na maarifa yote ili kumsaidia mkulima.
Maazimio hayo yamepitishwa leo 26 October 2018 katika mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya RC Lindi, ukiwahusisha wadau wakuu wa mikoa inayolima korosho wakiwemo Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, Wawakilishi kutoka Bodi ya Korosho.
Mkutano huo umeitishwa kufuatia mvutano wa bei ya zao la korosho katika Mikoa ya kusini kati ya wakulima na wanunuzi kulikosababishwa na bei ya korosho kuwa ndogo minadani (Chini ya Tsh.3000) ukilinganisha na misimu iliyopita, hali iliyopelekea wakukima wagomee kuuza korosho zao.
Akitangaza maamuzi hayo ya serikali, Waziri Mkuu Majaliwa amesisitza kuwa hawana nia mbaya bali lengo la serikali ni kuhakikisha Wakulima wananufaika na zao hilo.

No comments