KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
UTANGULIZI
Pilipili Mbuzi ni moja ya mazao yanayolimwa kwa uwingi kiasi katika mikoa ya Arusha Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Kagera, Iringa, Mbeya. Hutumika kama kiungo kinachochangamsha ladha ya chakula kwa harufu na ladha yake ya muwasho.
Zao hili huota na kustawi vizuri katika udongo wa hali (texture) mbalimbali, ili muradi tu usiwe udongo unaotumia maji Chachu ya udongo (pH) kati ya 4.3 hadi 9.7 huvumiliwa. Ni zao lisilovumilia kivuli cha muda mrefu. Katika maeneo ya joto, maendeleo ya mmea ni ya haraka zaidi kuliko maeneo ya baridi. Mmea huu huweza kuishi hadi miaka 3 endapo hali nzuri na bora ya matunzo itaboreshwa, hustawi na kuzaa sana katika mwaka wa kwanza, baadaye mavuno huongezeka kidogo mwaka wa pili, mwisho hupunguza uzalishaji na kufa. Kibiashara, zao hili hulimwa kama zao la msimu (mwaka) mmoja, kama ilivyo kwa jimii zote za pilipili, lakini kwa msimu mrefu /kipindi kirefu tofauti na aina nyinginezo.
MBINU ZA KULIMA
Ni vizuri na inashauriwa kusia mbegu kitaluni kwanza na kuitunza miche kitaluni kisha baadaye itahamishiwa shambani. Hii husaidia sana kuitunza miche kwa usawa katika hatua za awali. Kuotesha mbegu kitaluni Tengeneza tuta lenye vipimo hivi; Upana mita moja (1m) Urefu mita kumi (10m) Kimo cha santimita 15 hadi 20 Hivyo unaweza kuwa na matuta mawili hadi matatu unapoandaa kitalu cha kutosha ekari moja (unaweza kutumia trey maalum za kuotesha miche) kama zinapatikana kwa urahisi.
Chora vifereji kwa kijiti au hata kidole katika umbali wa sentimita 10,15 hadi 20 kati ya vifereji Nyunyiza mbegu katika vifereji, wastani wa mbegu 100 au pungufu katika kila kifereji ili kuipa miche nafasi ya kutosha wakati wa ukuaji Fukia mbegu kitaluni kwa tabaka dogo la udongo, mboji au samadi iliyooza vizuri kisha funika kitalu kwa matandazo (Mulch - majani yaliyokauka vizuri na yasiyo na mbegu ili kuepusha kuwa na magugu.) Baada ya hapo, mwagilia kwa kutumia keni kisha endelea kumwagilia kila asubuhi na jioni kuhakikisha kitalu kina unyevunyevu wa kutosha. Usizidishe maji- hupelekea shina kuoza na hatimaye mche kufa. Baada ya siku saba hadi kumi, miche itakuwa tayari imeshatokeza, utaondoa matandazo, huku ukiendelea na ratiba ya umwagiliaji kwa makini Ni vyema, wakati huo ukaanza program ya kuilinda miche dhidi ya wadudu waharibu na ukungu. Tumia Atakan/Amekan/Profecron au nyinginezo dhidi ya wadudu waharibifu Tumia Ivory 72WP/ Ivory 80WP au Ebony 72WP/ Ebony 80 WP au Linkmil dhidi ya ukungu- au nyinginezo zinazopatikana katika mazingira uliyopo. Spray kila wiki au kwa kufuata maelekezo. Baada ya kuondoa matandazo ni vyema ukaiwekea miche kivuli ili kuilinda dhidi ya jua kali au mvua, kisha kuilinda dhidi ya viumbe wengine wanaoweza kuharibu kama vile, kuku, bata, mbuzi nk.
KUTAYALISHA SHAMBA
Tayarisha shamba vuzuri, mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche (hivyo, pale unapoandaa kitalu ni vyema ukatayarisha shamba pia) Katua ardhi kwa kina cha kutosha (20m-30m) kwenda chini Andaa mifumo ya umwagiliaji mapema, unaweza kuwa umwagiliaji wa matone, mifereji au hata kwa ndoo (shimo kwa shimo) Kama utatumia mbolea za asili kama samadi, vyema ukaandaa mashimo na kuweka mbolea walau kilo moja kwa kila shimo (mche) Kama kuna upungufu wa fosforasi katika udongo ambayo ni muhimu kwa kukuza na kuimarisha mizizi ya mmea, ni vyema ukatumia mbolea za viwandani kama TSP 40kg, DAP 40kg, NPK 40kg au YaraWinner NPK -40kg kwa ekari moja -
huleta matokeo mazuri zaidi Kupandikiza miche shambani. Miche huwa tayari kuhamishiwa shambani kati ya wiki nne hadi sita (pale itakapokuwa imefikia kimo cha kalamu (inch 5 hadi 8) Siku moja kabla ya kuhamisha miche mwagilia tuta (kitalu) ili kulainisha udongo Ng’oa na pandikiza miche mapema sana asubuhi, jioni au kukiwa na mawingu. Nafasi ya kupandikiza ni sentimita 90 (umbali kati ya mstari na mstari) na sentimita 60 (umbali kati ya mche na mche) nafasi hii itatupa wstani wa miche 7500 kwa ekari. Mara baada ya kupandikiza miche shambani mwagilia maji ya kutosha na endelea na umwagiliaji kwa ratiba maalumu. Kutunza shamba Umwagiliaji- mwagilia kwa ratiba maalumu kulingana na hali ya unyevu ya udongo ( walau mara moja kwa wiki –
au kila baada ya siku 5) Umwagiliaji (maji ) huboresha (huongeza) utoaji maua kwenye mmea na kuupa nguvu ya kustahilimishi mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu- ikiambatana na uboreshwaji wa rutuba ya udongo kwa mbolea za asili. Palizi – ni vizuri kupalilia shamba ili kuzuia ushindani wa vurutubisho muhimu, chakula, hewa na maji kati ya mimea na magugu. Kuweka matandazo (mulch) tandaza majani makavu yasiyo na mbegu zilizokomaa juu ya ardhi ili kuhifadhi unyevu,kuongeza rutuba ya udongo, kupunguza kasi ya ukuaji wa magugu na kuzuia mmomonyoko wa udingo. Kurutubisha ardhi
Ni vizuri kuuongezea udongo rutuba kwa kutumia mbolea za asili, kama mboji au samadi, au mbolea za viwandani. Ndani ya wiki moja ya kupandikiza miche shambani- weka DAP, NPK au YaraWinner - NPK inafenya vizuri zaidi – kiasi cha 5g kwa kila mmea, umbali wa 5 cm kutoka ulipo mmea. Baada ya siku 30 hadi 45 weka CAN, SA au YaraLiva Nitrabor – inafanya vizuri zaidi kiasi cha 5g kwa kila mmea umbali wa 5cm kutoka ulipo mmea. Kisha endelea kurudia mbolea za kukuzia kila baada ya siku 45 hadi 60. Mwagilia kila baada ya kuweka mbolea.
WADUDU NA MAGONJWA
Mmea wa pilipili mbuzi haushambuliwi sana na magonjwa mengi bali Ukungu na Kutu ndiyo huwa tatizo pale mimea isipokingwa mapema. Mnyauko pia mara chache huathiri mimea kitaluni au hata shambani pia. Kuikinga mimea dhidi ya ukungu – Ivory 72WP/ Ebony 72WP/ WP au Linkmil dhidi ya ukungu- kwa msimu wa mvua au nyinginezo zinazopatikana katika mazingira uliyopo. Ivory 80WP/ Ebony 80WP Linkmil 80WP kwa msimu wa kiangazi (usio na mvua) –
au nyinginzo zinazopatikana katika maeneo yako. Mnyauko mara nyingi husababishwa na Fungus tumia Ridomil Gold au Trichodema. Kwa upande wa kutu, hii husababishwa na kushindwa kutibu ukungu (ukungu kuwa sugu) japo utaikinga mimea dhidi ya ukungu ni nyema ukaikinga dhidi ya kutu pia kwa kutumia XANTHO. Wadudu waharibifu
Kati ya wadudu wanaoshambulia zao hili ni Panzi- ambao hushambulia miche michanga, mara nyingi baada ya kuhamishia shambani. Aphids – hawa huweza kushambulia miche tangu kitaluni, hadi shambani. Nzi weupe pia hushambulia mara kadhaa zaidi katika miche yenye umri mkubwa kidogo. Kukabiliana na wadudu hawa tumia sumu za kuua wadudu zinazofanya vizuri katika maeneo uliyopo.
Dawa kama Atakan, Amekan, Profecron hufanya vuzuri zaidi. Puliza kwa kufuata maelekezo
Imeandikwa na IMANI LUBABA
Na kuletwa kwenu na Tanzania na kilimo, mtandao ulio jikita katika kutoa elimu bora ya kilimo na ufugaji
Post a Comment