PICHA NA; BERNARD AHIMIDIWE |
W
|
akulima wengi nchini Tanzania wamekua
wakipitia changamoto nyingi sana katika kilimo, changamoto hizo zimechangia kwa
kiasi kikubwa katika kurudusha nyuma maendeleo ya kilimo na nchi kwa ujumla, kwa sababu kilimo ndio uti
wa mgongo wa taifa letu, na kutokana na sera ya serikali ya awamu ya (5) “serikali ya viwanda” ni dhahiri kua kilimo ni sekta muhimu sana.
Team ya vijana(5) tulifunga safari mpaka
mkoani Morogoro kuzungumza na wakulima wa mkoani humo ili kufahamu hali halisi
ya wakulima wadogo wadogo na kujifunza vingi kutoka kwao na kufahamu ni changamoto gani hasa wanazo
kumbana nazo kila siku, pia tulitumia fursa hiyo kuwapatia elimu na ushauri wa
kitaalamu itakayo wasaidia katika kufanya kilimo chenye tija .
Bi Jonisia Machibya(79)
ni mkazi na mkulima Lukobe mkoani Morogoro, yeye ni mkulima mdogo wa mahindi na
maharage, na analima kiasi cha ekari 2, anasema… hakumbuki hasa ni lini alianza
kilimo ila ni zaidi ya miaka 20, kwa kawaidia
huvuna kiasi cha gunia mbili hadi tatu za mahindi
kwa
hekari zote. Anasema…. kilimo mara nyingi hua kina changamoto nyingi sana na
pia hutofautiana kila mwaka. “mfano mwaka huu kilimo kimekua kigumu sana
kutokana na mvua kuchelewa kunyesha” Anaongeza.. Hawajui cha kufanya kwa sababu
wadudu wanashambulia mahindi shambani, hata ukipita mashamba mengine huko
ukiangalia wadudu wamekula mazao sana.
Pia anasema changamoto nyingine anayo pitia ni upatikanaji wa elimu ya kilimo,
Tangia miaka mingi amekua akilima mahindi lakini anasikia tu kwa watu wengine
lakini yeye ajawahi kuvuna zaidi ya gunia tatu, kutokana na changamoto kua
nyingi sababu na hajawahi kupata kupata fursa ya kupata elimu itakayo muwezesha
nayeye avune mazao mengi.
PICHA NA; BERNARD AHIMIDIWE |
Bi
Jonisia anasema anaiomba serikali iwakumbuke iwasaidie waweze kupata elimu
ya kilimo kwa sababu imekua ni changamoto kubwa sana kwao, na pia anaomba
serikali iwawezeshe kupata dawa za wadudu wanao shambulia mahindi yao. Alimaliza
kwa kusisitiza kua serikali iwasaidie mapema waweze kupata dawa za wadudu hao. Baada
ya kuzungumza na Bi jonisia, tulipata muda wa kukaa na kuzungumza nae kujifunza
kupitia uzoefu wake alio nao katika kilimo, pia tulimpatia elimu bora kuhusu
kilimo bora za mahindi, pia tulimuelekeza tiba na mbinu ambazo anaweza
kuzitumia ili kupambana na tatizo la wadudu shambani.
Baada ya kuzungumza na Bi jonisia
tuliamua kuelekea maeneo mengine kufahamu ni changamoto gani pia zinawakumba
wakulima katika maeneo mengine. Na tulifunga safari mpaka Mazimbu- Morogoro. Na
tulibahatika kupata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakulima wadogo maeneo
hayo.
Ndugu Salehe Ramadhani
ni mkulima mdogo anae patikana Mazimbu- Morogoro, yeye pia ni mkulima wa
mahindi na mboga mboga, na ameamua kujikita kaTika kilimo mda mrefu sana
Anasema ameanza kulima tangia Miaka ya 1970, Anasema kwa kipindi cha miaka hiyo
yote amekua akilima kwa kutumia jembe la mkono hadi sasa. Na tulipata fursa ya
kutembelea shamba lake pia kujionea hali
harisi ya shamba lake.
Ndugu
Salehe anasema yeye hulima ekari 1.5 na umchukua mda wa wiki mbili hadi tatu
kukamilisha kulima, anasema anachukua mda mrefu kutokana na kutokua na nyenzo
nzuri za kilimo. Anasema kwa kawaida yeye huvuna kiasi cha guni 6 hadi 10
katika eneo lake na mavuno hutofautiana mfano mwaka jana alivuna gunia 10.
Baada ya kuzungumza na Ndugu salehe na kufahamu mengi kuhusu kilimo
anachofanya, tukapata fursa ya kuzunguka na kututizama shamba lake. Nawakati
wakuzifahamu changamoto anazo zipitia ukafika. Ndugu Salehe anachema anapitia
changamoto nyingi sana katika shughuri zake za kilimo, ila changomoto kubwa
zikiwa ni: wadudu kushambulia sana shambani, anasema wadudu wamekua ni tishio,
unaweza kukuta robo tatu ya mahindi yote wadudu wameshambulia licha ya kutumia
dawa tofauti tofauti.
PICHA NA; BERNARD AHIMIDIWE |
Ndugu
salehe anaendelea kwa kusema changamoto nyingine ambayo inawakabili ni
upatikanaji wa mbegu bora, Anaelezea kua mbegu wanazo tumia mara nyingi hua
hazitoi mazao ya kutosha na pia ukuaji wake hua ni wakusuasua sana, Na
changamoto nyingine ambayo imetusumbua sana mwaka huu ni mvua kubwa kupita
kiasi, Anasema kama ukitazama unaweza
ukaona jinsi mvua ilivyo haribu baadhi ya mahindi, na pia mvua hizi kubwa
zimepelekea sana katika kuchochea ukuaji
wa haraka wa magugu, anasema amejitahidi sana kupalilia kwa wakati lakini baada
ya muda kidogo tu magugu yameshakua kwa kasi sana.
Ndugu
salehe anatoa wito kwa serikali na taasisi zingine zinazo husika ziweze
kuwasaidia waweze kupata mbegu bora ambazo zitakua na mazao mengi tofauti na
hizi wanazo zitumia sasa, pia anaomba serikali iweze kuwasaidia kupata dawa
ambazo zitaondoa kabisa tatizo la wadudu mashambani kwasababu wadudu
wamesababisha sana hasara kwao, wakisha ingia shambani wakashambulia mahindi
mara nyingi hata mavuno ya mahindi hua yanapungua sana na wengine husindwa kabisa
hata kurudisha gharama zao walizo tumia katika kulima.
Makala hii imeandikwa na; Imani
Lubaba
Mawasiliano; +255 764 148 8221
Barua
pepe: rubabaimani@gmail.com
Mpiga picha; Bernard
Ahimidiwe
Washiriki: Juvenal
Lasway
Abdallah Saidi
Selemani saidi
Bernard Ahimidiwe
Imani Lubaba
0 Comments