FURSA KWA WAZALISHAJI WA NGURUWE NCHINI.
Kumekua na ongezeko kubwa sana la wazalishaji wa nguruwe nchini, Lakini kumekua na changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa mbegu bora hapa chini, hivyo imepelekea wafugaji wengi na hata watu wanaotaka kuingia katika ufugaji kushindwa kuingia au kupigia hatua katika ufugaji wao.
Hivyo Tanzania na Kilimo ikiongozwa na IMANI LUBABA imeandaa mfumo maalumu kwaajiri ya kuwatambua na kuwafahamu wazarishaji wa mbegu bora za nguruwe nchini kwa lengo la kuwakutanisha wafugaji na wazarishaji wa mbegu bora na pia kusaidia kutafuta soko la nguruwe kwa wazarishaji
. Hivyo kama wewe ni mfugaji na unasifa zifuatazo unaweza kujaza form ya kujiunga.
SIFA
- Uwe mahali popote nchini
- uwe unafuga nguruwe wa aina ya Large white, saddleback au Landrace
- uwe na mawasiliano ya uhakika ikiwezekana uwe ni mtumiaji wa whatsup
- uwe na uwezo wa kuzalisha nguruwe wa kutosha kwaajiri ya kuuza.
Kwa kujiunga utaweza kujitengenezea soko la uhakika na pia kufahamiana na kushare ideas, uzoefu na ujuzi pamoja na wafugaji na wazalishaji wengine.
kama unasifa tajwa hapo juu usisite kujaza form kwenye link kwa kubofya HAPA
Post a Comment