UFUGAJI WA MENDE FURSA MPYA MJINI
Mende ni
moja kati ya wadudu ambao wamekua wakichukiwa na watu wengi sana. Hii ni
kutokana na mtazamo wa watu kua mende ni wadudu wachafu na hawastaili kuwa
karibu na binadamu. Lakini hii imekua tofauti kwa watu wengine hivyo wameamua
kuona fursa katika ufugaji wa mende. Mende ni moja kati ya wadudu wenye
matumizi mengi sana hutumiwa kama chakula kwa mifugo na hata binadamu,
inaaminika kua mende hua na kiasi kikubwa sana cha protini. Mende hutumiwa kama
kitoeo katika maeneo tofauti tofauti huku china, Denmark na Brazili ikiongoza
kwa kua na watumiaji wengi na uaminika kua mende hutumiwa na watu wenye kipato
cha juu hii ni kutikana na kua mende hua na gharama katika kuwanunua.
Mende
utumika kwa matumizi tofauti tofauti, hutumika kama chakula cha mifugo kama
vile kuku, bata, sungura, samaki, lakini pia utumika kama chakula kwa binadamu,hutumika
katika matumizi ya kielimu na hutumika kutengeneza bidhaa za urembo na dawa mbali mbali.
Kwa sasa
hapa Tanzania mende hufugwa na wafugaji
mbalimbali japo sio kwa kiasi kikubwa. Na kwa mujibu wa wafugaji wa mende hapa
Tanzania, Ni bora kufuga mende kuliko kufuga mifugo mingine. Hii ni kwa sababu
mende hua na faida kubwa sana, na hawana gharama katika kuwafuga. Wafugaji
wengi husema kua soko kubwa ni nje ya nchi na mende hununuliwa na wachina ambao
hutumia mende kama kitoeo na kwa kilo Moja ya Mende huuzwa 70,000Tsh, Japo pia
wafugaji wa mende wamekua wakipata wateja wazawa na taasisi mbalimbali ambazo
wao hutumia mende katika shughuri za
kielimu na kama chakula kwa mifugo, na kwa kawaida mende mmoja huuzwa kwa bei
ya 1,000Tsh.
Chakushangaza
ni kwamba licha ya mende kua na faida kubwa hugharimu pesa kidogo katika kuanza
kuwafuga na hata katika kuwatunza. Mende mzazi hununuliwa kwa bei ya TSH 1,000
kwa jike na dume na sanduku la kuwafugia huuzwa TSH100, 000. Hivyo ni gharama
ambayo mtu yeyote anaweza kumudu kuanza kufuga. Na kwa mujibu ya wafugaji wa
mende hugharimu kiasi kisicho zidi 5,000 kwa mende 3,000 katika kuwalisha. Chakula
cha mende hakiumizi kichwa kabisa kwa sababu chakula chake ni rahisi kupatikana
na pia ni kwa gharama nafuu sana. Mende hula unga, matunda ya aina yoyote ugali
e.t.c Hivyo mtu yeyote anaweza kufuga.
Soko la
mende limekua likikua siku hadi siku hivyo imefanya wafugaji washindwe kukidhi
soko hii nikutokana na kuzalisha mende wachache, hivyo wanatoa wito kwa
watanzania wengine kuweza kuchangamklia fursa kuanza ufugaji wa mende.
TAZAMA VIDEO KWA KUBOFYA PICHA JUU NA SUBSCRIBE KUA WAKWANZA KUPATA ELIMU KILA WIKI
Imeandaliwa
na kuandikwa na IMANI LUBABA, +255 764148221, rubabaimani@gmail.com
Post a Comment