USIFANYE MAKOSA HAYA KATIKA UFUGAJI WAKO WA NGURUWE


Siku za hivi karibuni, tulitembelea mfugaji mpya wa nguruwe aliyepo katika maeneo ya Fella Jijini Mwanza kwa lengo la kumsaidia na kumpa huduma ya kitaalamu kwa nguruwe wake anayetarajia kuzaa. Tulifurahishwa kuona juhudi zake kubwa katika kuhakikisha nguruwe wake wako katika hali nzuri kiafya.

Hata hivyo, tulimpa ushauri wa namna gani anaweza kumuhudumia nguruwe wake anaezaa na watoto kwa ujumla na pia jinsi ya kuboresha zaidi mazingira ya banda lake, hususan kwenye usafi. Usafi wa banda ni jambo la msingi kwa afya ya nguruwe, hasa wakati wa uzazi. Mazingira safi yanapunguza hatari ya magonjwa na huongeza ustawi wa wanyama, jambo ambalo linahakikisha uzalishaji bora.

Katika ziara hiyo, tuliweza kumuelekeza hatua za kuchukua ili kuhakikisha nguruwe wake wanazalisha vizuri zaidi na wanakuwa na afya bora. Tumeandaa pia video ya ziara hiyo, ambayo unaweza kuitazama Video Hapa


Koudijs: Suluhisho Bora la Lishe kwa Nguruwe

Kwa ufugaji wa nguruwe wenye mafanikio, lishe bora ni jambo lisiloweza kupuuzwa. Koudijs imeleta suluhisho bora kwa wafugaji wa nguruwe kwa kutoa chakula kilichosheheni virutubisho muhimu vinavyosaidia ukuaji wa haraka, uzalishaji mzuri wa nyama, na afya bora.

Bidhaa za Koudijs zina viwango vya kimataifa na zimeundwa mahsusi kwa mazingira ya Afrika Mashariki. Zimepokelewa vyema na wafugaji kote nchini kwa sababu ya matokeo yake bora.

Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa za Koudijs kwa nguruwe na jinsi zinavyoweza kuboresha ufugaji wako, wasiliana na Daktari wa Mifugo Dr. Uledi kwa namba 0768 864 628.


Post a Comment

0 Comments