Jinsi Lishe ya Koudijs Ilivyobadili Ufugaji Wangu wa Nguruwe

0

"Nilipoanza ufugaji, nilikua natumia formula zangu mwenyewe. Kila mfugaji alikuwa na formula yake — jambo ambalo lilileta changamoto kubwa sana. Lakini tangu nianze kutumia bidhaa za Koudijs, mambo yameenda vizuri sana. Ndani ya miezi sita tu, nguruwe wangu wamefikia kilo zaidi ya 100."
Ndugu Japhet, mfugaji wa nguruwe kutoka Kahororo, Bukoba.

Katika kijiji cha Kahororo, nje kidogo ya mji wa Bukoba, Ndugu Japhet ni miongoni mwa wafugaji waliogeuza changamoto za ufugaji kuwa fursa ya mafanikio. Akiwa na uzoefu wa awali wa kutumia mchanganyiko wa chakula alichokitengeneza mwenyewe, Japhet alikumbana na changamoto nyingi zikiwemo ukuaji duni wa mifugo, uzani mdogo, na gharama kubwa za matibabu.

Hali hiyo ilibadilika kabisa baada ya kugundua na kuanza kutumia bidhaa za lishe za Koudijs — kampuni inayojulikana kimataifa kwa utengenezaji wa chakula cha mifugo chenye ubora wa hali ya juu.

Mafanikio Yaliyochochewa na Lishe Sahihi

Japhet anasema kuwa ndani ya miezi sita tangu aanze kutumia lishe ya Koudijs, aliona tofauti kubwa katika ukuaji wa nguruwe wake. Kwa kipindi hicho kifupi, baadhi ya nguruwe wake walifikia uzito wa zaidi ya kilo 100 — matokeo ambayo hayakuwahi kutokea alipokuwa bado anatumia formula zisizo rasmi. Mbali na ongezeko la uzito, Japhet pia aliona maboresho katika afya ya mifugo, kiwango kidogo cha magonjwa, na gharama ndogo ya uendeshaji. Mafanikio haya yalimpa ari ya kuwekeza zaidi kwenye ufugaji na kuwa mfano kwa wafugaji wengine katika eneo lake.

Umuhimu wa Lishe Bora katika Ufugaji

Koudijs imejikita katika kutoa suluhisho la lishe lililofanyiwa utafiti wa kina kwa ajili ya kukuza mifugo yenye afya, uzito sahihi, na tija kwa mfugaji. Lishe bora huchangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya ufugaji, hasa wakati huu ambapo ushindani katika sekta ya kilimo na ufugaji unazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe ya mifugo, matumizi ya chakula kilichosindikwa kitaalamu huongeza ufanisi wa mifugo kwa zaidi ya asilimia 30 ikilinganishwa na matumizi ya chakula cha kawaida au kisicho na uwiano sahihi wa virutubisho

Kupata Elimu Kamili Tazama video 


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

write your comment here

write your comment here

Post a Comment (0)

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top