Katika harakati zetu Rubaba Media kuelimisha na kushauri wakulima na wafugaji kote nchini, tukishitikiana na Koudijs safari yetu ya hivi karibuni ilitufikisha mkoani Mara — hasa maeneo ya Tarime, Nyamongo, na vitongoji vyake. Tulikutana na wafugaji wapya na waliopo tayari waliodhamiria kwa dhati kuhakikisha ufugaji wa nguruwe unabadilisha maisha yao.
Lakini pia tuliona jambo moja la msingi: Ufugaji wa nguruwe bado haujachukuliwa kwa uzito unaostahili na watu wengi, ilhali ni moja ya sekta zinazolipa sana ukizingatia mahitaji ya soko la nyama na mbegu bora zinazoongezeka kila siku.
🐷 Mfano Hai wa Mr & Mrs George – Waanzilishi Wenye Maono
Wakiwa wakazi wa Tarime, Mr & Mrs George ni mfano bora wa familia mpya iliyodhamiria kuingia kwenye ufugaji wa nguruwe kwa maandalizi ya kisasa. Wameanza kwa kuchagua mbegu bora, kujenga banda la kisasa lenye uingizaji hewa mzuri na mazingira safi, na zaidi wamechagua kupata elimu ya kina kutoka kwa wataalam ili kuepuka makosa ambayo yamekuwa kikwazo kwa wafugaji wengi.
Wanaamini kuwa, kwa mipango sahihi, ufugaji wa nguruwe si tu chanzo cha kipato cha uhakika, bali pia njia ya kujenga biashara endelevu kwa familia.
🐖 Mr. Julias – Kutoka Nguruwe Wachache Hadi Mzalishaji wa Mbegu Bora
Mwaka 2021, Mr. Julias alikuwa na ndoto tu — alianza na nguruwe wachache katika kijiji chake Tarime. Leo hii, ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa mbegu bora za nguruwe katika kanda ya ziwa. Anauza majike na madume yenye afya njema, huku akiwa ni sehemu ya wafugaji wanaosaidia kuendeleza vizazi bora vya nguruwe Tanzania.
Aliamua kuwekeza kwenye elimu, lishe bora, na mbinu bora za usafi na uendeshaji wa banda. Matokeo yake? Anaingiza faida mara dufu, na ameongeza idadi ya wateja kila mwezi.
💡 Kwa Nini Uanze Ufugaji wa Nguruwe Leo?
🔍 Unahitaji Elimu, Ushauri au Mafunzo?
Katika kazi yetu ya kuzunguka Tanzania nzima, lengo letu ni moja: Kumsaidia kila Mtanzania aweze kufanikiwa kupitia kilimo na ufugaji. Tunashirikiana na wadau mbalimbali kama Koudijs Feed Solutions kuwapatia elimu ya lishe bora, mifumo ya ufugaji, na mbinu sahihi za uendeshaji wa miradi ya nguruwe.
Ikiwa nawe unataka kuanza, umeshindwa mara ya kwanza, au unahitaji maarifa zaidi, usiache kututafuta.
👉 Bonyeza hapa kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa WhatsApp: https://wa.me/255764148221
Usikose nafasi hii. Anza leo! Ufugaji wa nguruwe unaweza kuwa mkombozi wa maisha yako ya kiuchumi.
write your comment here