Wakulima na wafugaji wengi wanatamani kuingia kwenye kilimo biashara, lakini bado kuna mambo ya msingi wanayoyapuuza. Mtu anaweza kuwa na shamba, lakini hajui ukubwa halisi wa eneo lake. Wengine wameanza kulima bila kuelewa aina ya udongo waliokuwa nao, au kama unafaa kwa mazao wanayoyalenga. Na wengine wana ndoto kubwa za kuwekeza, lakini hawana mpango wa kitaalamu wa kuwapitisha hatua kwa hatua.
Hapo ndipo huduma yetu ya farm visit inapokuja. Tunapofika shambani kwako, tunapima ukubwa wa eneo lako kwa usahihi, tunachukua sampuli za udongo na kuzipima, tunakushauri ni kilimo au ufugaji gani unafaa kwa mazingira yako, na kisha tunakuandikia ripoti ya kitaalamu inayokuweka tayari kwa kilimo biashara cha kweli.
Kilimo cha biashara hakihitaji kubahatisha, kinahitaji taarifa na mwongozo wa kitaalamu. Na huo ndio mkono tunaotaka kukushika nao—ili uanze safari yako ukiwa na uhakika wa kile unachofanya na kuona matokeo makubwa.
📌 Usisite, wasiliana nasi leo kwa farm visit kupitia link hii: https://wa.me/255764148221
#KilimoBiashara #FarmVisit #MkulimaSmart #Mafanikio #RubabaMedia #TanzaniaNaKilimo
write your comment here