Miaka kadhaa nyuma, Mama Kuku alikuwa mfanyakazi wa Tanzania Breweries Limited (TBL) jijini Mwanza. Alikuwa na kazi nzuri, ratiba maalumu, na mazingira ya uhakika kama wafanyakazi wengi walioajiriwa. Lakini ndani yake, kulikuwa na shauku iliyojificha—ndoto ya kuwa zaidi ya mfanyakazi, ndoto ya kujenga maisha yatakayomtengenezea urithi, uhuru, na utambulisho.
Zawadi Iliyoandika Hatma Mpya
Wakati wa kutembelea ukweni kwao, mama mkwe wake alimkabidhi zawadi ya kuku wa chotara. Wengine wangeona ni zawadi ya kawaida, lakini kwake iligeuka kuwa mwanga wa safari mpya.
Hapo ndipo moyo wake ulipoanza kumwambia, “Labda hapa ndipo ninapopaswa kuwa.”
Akiwa bado kazini, alianza kufuga kwa hatua ndogo. Aliwalea kuku wale kwa umakini, akajifunza tabia zao, lishe zao, na taratibu za ukuaji wao. Kila siku alikuwa akiona kitu kipya kinachomvutia zaidi.
Kukua Kidogo Kidogo… Mpaka Kuacha Kazi
Hata bila mtaji mkubwa, Mama Kuku aliamua kuwekeza kile alichonacho. Aliuza wachache, akaongeza wachache, akajifunza kutokana na makosa, akapanua taratibu.
Ndoto yake ilikua sambamba na banda lake.
Hatimaye alifikia hatua ambayo moyo wake ulisema kwa nguvu:
“Sasa ni wakati wa kuacha ajira na kufanya kile ninachokipenda.”
Uamuzi huo ulikuwa mgumu, wa ujasiri, lakini ndio uliogeuza maisha yake kabisa. Leo, Mama Kuku ni mmoja wa wanawake wanaotambulika Mwanza na nje ya mkoa kwa shughuli za ufugaji wa kuku—hasa kuku chotara na broiler (kuku wa nyama).
Mwanamke Mpambanaji Anayeinspire
Rubaba TV tulibahatika kumtembelea na kusikia simulizi yake ya kipekee. Mama Kuku si mfugaji tu—ni mwalimu, ni mfano, ni dira ya wanawake na vijana wanaotamani kuanzisha ufugaji lakini wamekwama kwa hofu au ukosefu wa uthubutu.
Anasema mara nyingi:
“Nilianza na kuku mmoja. Siri ni kuanza popote ulipo.”
Safari yake inaonyesha wazi:
Haitaji kuwa na mamilioni ili kuanza. Inahitaji tu uamuzi, utiifu, na shauku.
Kuhusu Shamba Lake Leo
Leo Mama Kuku anaendelea kuzalisha kuku chotara na broiler kwa wingi, akiwauzia wateja kutoka maeneo mbalimbali. Anafuga kibiashara kwa nidhamu ya hali ya juu—kuanzia usafi, lishe, chanjo, hadi mbinu za kuongeza uzalishaji.
Na uzuri zaidi, safari yake inazidi kukua… bado haijafika mwisho.
Kwa Nini Story Yake Ni Ya Muhimu?
-
Inawapa vijana na wanawake ujasiri—hasa wale walioajiriwa lakini wana ndoto ya kujitegemea.
-
Inaonyesha kuwa ufugaji unaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato, endapo unafanyika kitaalamu.
-
Inaonyesha kuwa zawadi ndogo au nafasi ndogo inaweza kugeuka kuwa mradi mkubwa wa maisha.
Tunatoa shukrani za dhati kwa KOUDJIS, wazalishaji wa bidhaa bora za lishe za mifugo nchini Tanzania.
Bidhaa zao zimekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji kama Mama Kuku—kuanzia kuku wa nyama, chotara, kuku wa mayai, ng’ombe, nguruwe, hadi samaki. Na kizuri zaidi, KOUDJIS sasa wanapatikana karibu nchi nzima, hivyo kumrahisishia mfugaji yeyote kupata vyakula vya ubora wa juu.
JIUNGE NA GROUP LETU LA MAFUNZO YA KILIMO NA UFUGAJI KWA KUBOFYA https://wa.me/255764148221


write your comment here