MAgonjwa ya kuku

               Habari za saiz tena,natumaini wewe ni mzima wa afya .Tunaendelea na tulipo ishia na leo ntapenda tuzungumzia tena magonjwa mengine lijulikanalo kama
          MAFUA YA KUKU(INFECTIOUS CORYZA)
Niugonjwa unaoshambulia mfumo wa upumuaji.Husababishwa na kimelea wa aina ya bacteria na huenea kwa njia ya hewa.
                DALILI
-Kuvimba uso na macho.kichwa kujaa maji na kuvimba
-kukohoa,kupiga chafya na kutoa makamasi
-kubadili rangi ya upanga na kuwa wa kibuluu
-kupumua kwa shida kukoroma wakatib wa kupumua
-kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji asilimia 10-40
-kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea vingine
-matukio ya vifo si mengi na wagonjwa hupona baada ya wiki 2-3

      TIBA/KINGA
-Dawa za antibiotic kama vile streptomycin,OTC, na vitamin kwenye maji kwa muda wa siku 7
-usafi wa mazingira na vifaa vya kulishia kuku
-uingizaji wa kuku wageni iwe vifaranga au kuku wakubwa uzingatie kuchagua kuku ambao hawana ugonjwa
-chanjo ipo na utolewa mara mbili baada ya siku 3 wakiwa na umri  wa wiki 4.chanjo itolewe kabla kuku hawajapata ugonjwa

 Bila shaka natumaini umelifahamu vizuri hili gonjwa tiba dalili na kinga yake na omba tuende pamoja tena na tuone gonjwa lingine lijulikanalo kama
                 KUHARA DAMU(COCCIDIOCSIS)
    Hili ni gonjwa la mfumo wa chakula yani digestive systeam kwa lugha ya kitaalam.Husababishwa na vimeleana unatokea zaidi kwenye kuku wanaofugwa ndani moja kwa moja.
        DALILI
-kuhara damu
-kuzubaa na kuacha kutaga
-unaathiri zaidi vifaranga hasa wanapokua kwenye kundi au makundi makubwa.vifaranga kujikusanya pamoja na kujikunyata kama wanaohisi baridi
  TIBA/KINGA
Dawa aina ya sulphonamides kama vile Amrolium, ESB3
-usafi wea mazingira na ndani ya banda
-[fuga kuku  kwenye mabanda yenye sakafu isiyo na matundu
                                    
                               
                                                mfano wa kifaranga mwenye coccidiosis
  Nitumaini langu kua umesoma kwanzia mwanzo had mwisho wa magonjwa haya na nitumaini langu pia umeelewa pia.usisite kunitumia maoni,ushahuri na comment zako
tukutane tena wakati ujao..................................................................

No comments