Ndugu msomaji leo nitakuletea kitu kipya na chenya manufaa
sana ukikizingatia,hizi ni aina ya ng'ombe wa maziwa waliopo duniani
MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA
MAZIWA
Umbo : siku zote ngo'mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbola
pembe tatu, humpless pia awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa kwa sababu
ng'ombe mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi.na
chakula kingine kinabadilishwa na kua maziwa.hivyo ng'ombe mwenye tumbo kubwa
anauwezo wa kutoa maziwa mengi sana.
Kiwele na chuchu: siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa
anakiwele kizuri kimeshika vizuri kwenye mwili na kiwele kizuri hua kinabonyea
kama spongy.na pia kiwele na chuchu vinatakiwa kua kubwa.
Rangi ya mwili : sikuzote ng'ombe mzuri wa maziwa anarangi
moja au mbili tu kwenye mwili wake e.g brown, red white and black.
Asili : siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa anatokea katika
maeneo yenye hali ya hewa ya kati e.g
Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.
.
AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA
Kuna makundi mawili ya ng'ombe kuna wa nyama pamoja na
wamaziwa. na kuna aina nyingine pia ni wazuri kwa nyama pamoja na wamaziwa
mfano mpwapwa na sahiwal.
hizi hapa na aina za
ng'ombe wa maziwa
· Holstein
Friesian
· Brown swiss
· Ayrshire
· Guernsey
· Jersey
· Mpwapwa
· Sahiwal
· Red poll
AINA ZA NG'OMBE WA
MAZIWA NA SIFA ZAKE
1.HOLSTEIN FRIESIAN
Hii ni aina ya
ng'ombe wa maziwa ambayo ni kubwa kuliko aina zote
SIFA
· Asili yake
ni Holland
· wanamabaka
meupe na meusi
· maziwa yao
yana mafuta kiasi cha 3.5%
· wanatoa
maziwa mengi 6000 liters kwa kila msimu
wa kukamua
· watoto wake
wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi.
· jike
anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs
2. BROWN SWISS
Hii ni kati ya aina za zaman sana, ili gunduliwa katika
milima ya Switzerland?
SIFA
· Wame
gunduliwa Switzerland
· hii ni aina
nzito inayo fuata baada Friesian
· wanalangi ya
brown inayo koza
· niwapole
· uzito wa
jike 450-550kg na dume 600-900kgs
3. AYSHIRE
Hii ni aina kubwa inayo fata baada yaFriesian na brown Swiss
SIFA
Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey
wanarangi nyekundu
kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe
asili yao ni South west Scotland
maziwa yao yanamafuta 4%
wanachuchu na kiwele kizuri sana
4. Guernsey
Characteristics:-
wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu
wanarangi nyeupe na nyekundu
maziwa yao yanamafuta 4.5%
wanatoa maziwa 4200litres kwa msimu mmoja wa kukamua
uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs
5. Jersey
hii ndo aina ndogo kuzudi zote
Characteristics:-
· asili yao
ni visiwani kati ya UK na France
· maziwa yao
yanamafuta kuzidi wote 5%
· wanarangi ya
blackish brown
· uzito wa jike
400-450kg dumeto 500-600kgs.
asante mpenzi msomaji endelea kua na mimi upate kujifunza
mengi kwa tasinia ya kilimo pamoja na ufugaji
na pia usisahau kuifollow blog hii hili kipata kile ninacho
kiandika moja kwa moja kwenye email yako
3 Comments
na kipindi cha kukamua hua uchukua siku 305