KILIMO BORA CHA ALIZETI
UTANGULIZI
Alizeti ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana nchini tanzania hasa mikoa ya singida na dodoma.
na nizao ambalo linalimwa hasa kwa lengo la kuzalisha mafuta linatoa mafuta kati ya asilimia 35-40.
pia mabaki yake yani mashudu hutumika kulishia wanyama pia
hivyo wakulima wanashauliwa kufata mambo ya fuatayo ili kupata mavunop mengi na nyenye thamani
KUANDAA SHAMBA
hii ni hatua muhimu na ya hawali kabisa inamaana hatua hii ni moja kati ya atua muhimu za kukufanya wewe mkulima upate mazao mengi na bora.
kama mazao yoyote yale unatakiwa kuandaa shamba mapema na unatakiwa kutifua udongo vizuri ili kuwezesha hewa na maji kupita ndani ya udongo na pia unaweza kuchanganya udongo na thamadi ili kuongeza rutuba.
WAKATI WAKUPANDA
Upandaji wa alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika.
Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya
mwezi Februari.
Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.
KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI WA ALIZETI
Kiasi cha kilo 3 – 4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja.
Panda mbegu 3 – 4 katika kila shimo moja kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita
30 kutoka shimo hadi shimo au sentimeta 75 kwa 40 au Sentimeta 90 kwa 30 kwa mbegu kubwa. Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5 – 5.
Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza mche mmoja na katika kupunguza unazingatia
MBOLEA
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na
rutuba.
Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbolea ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari
moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa
kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye. au Pandia mbolea ya TSP au DSP, au SSP na Kuzia kwa SA baada tu ya palizi ya Kwanza (wiki mbili hadi tatu baada ya mimea kuota)
Wakati wa kuweka mbolea angalia isigusane na mbegu au mche wa alizeti kwani huunguza.
PALIZI
Alizeti hukua taratibu katika wiki chache za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema ili kupunguza
hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo
mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta ili kuzuia kuanguka.
WANYAMA NA WADUDU WAHARIBIFU WA ALIZETI
1..NDEGE
Alizeti hushambuliwa sana na ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao shambani.
Kuzuia
- Usipande alizeti karibu na msitu/pori
- Vuna mapema mazao yako mara tu kichwa kinapobadilika rangi na kuwa manjano
- Panda alizeti kwa wingi katika shamba moja
- Amia ndege kwa mutumia sanamu, makopo na ua kuweka watu ingawa ni gharama.
2..FUNZA WA VITUMBA (American bollworm)
Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na
kukomaa kwa mbegu.
Kuzuia:
- Tumia dawa yo yote ya kuulia wadudu inayopatikana katika eneo lako
MAGONJWA YA ALIZETI
Alizeti hushambuliwa na magonjwa yakiwemo madoa ya majani, kutu, kuoza kwa mizizi, shina, kichwa na
kushambuliwa na virusi.
Kuzuia:
- Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao
- Panda mbegu safi zilizothibitishwa na wataalamu
- Choma masalia ya msimu uliopita
UVUNAJI WA ALIZETI
Unashauriwa kuvuna alizeti mara tu inapokomaa ili kupunguza hasara ya kushambuliwa na ndege. Alizeti
iliyokomaa kichwa hubadilika rangi toka kijani kibichi na kuwa njano. Kata vichwa na kuvianika juani ili
vikauke vizuri.
Piga piga vichwa ili kutoa mbegu za alizeti, kisha upepete na kuendelea kuzianika ili zikauke vizuri.
Utafiti unaonyesha kuwa mkulima anaweza kupata magunia kati ya 10 -12 kutoka katika ekari moja.
Post a Comment