UTANGULIZI
Mihogo ni moja kati ya zao ambalo linalimwa na kutumika maeneo tofauti tofauti kote duniani, mihogo hutumika kama zao la chakula na zao la biashara, wengine hula miogo ikiwa mibichi, kuchemshwa,kuchomwa,kuaangwa na hata pia kukaushwa na kusangwa nakutumika kwa kupikia ugali.
HALI YA HEWA
Mihogo ustawi katika maeneo yenye mvua 1000 hadi 1500mm kwa mwaka, na maeneo yenye mita 1000 kutoka usawa wa bahari, uzuri wa mihogo unakua na kusitawi vizuri katika udomgo wa aina yoyote ile ila inafaa kulimwa maeneo yenye mtelemko 0 had 8% lakini pia 8 hadi 15% unaweza kulima lakini lazima itumike njia ya kuzuia mmomonyoko mfano kulima kwa matuta.
KUANDAA SHAMBA
Kama mazao mengine shamba la mihogo linatakiwa kuandaliwa mapema,kusafishwa na kuwekwa tayari kwaajili ya kupanda mihogo. unaweza kuandaa kwa kutumia jembe la mkono,trekta na jembe la ng'ombe.
pia shamba la mihogo linaweza kulimwa kwa matuta au kwa kusawazisha na kupanda bila kuweka matuta.
AINA ZA MIHOGO
kuna aina nyingi sana za mihogo kama vile golden yellow, lakaini, ku-50 na pr-c-24
lakini aina zimegawanywa katika aina mbili
mihogo mitamu-valesca, msitu zanzibar, kibaha, aipu
mihogo michungu- ali utumba, leonjo
KUPANDA
Mihogo upandwa kwa kutumia miti yake(stalks). inatakiwa iwe imekua angalau miezi 8 tokea ipandwe na inayo shauliwa zaidi ni ili ambayo imevunwa karibuni kwa kua ndo inakua na uwezekanoi mkubwa wa kuota.
miti ambayo inatakiwa kupandwa inatakiwa kutunzwa eneo lenye kivuli na safi.
andaa miti ya kupanda siku moja kabla kwa kuikata ulefu wa setimita 25- 30 na iwe na pengele(nodes) 5 hadi 7
miti inatakiwa kufukiwa 1/3 ya urefu wake na pia ambayo haijashika inatakiwa kurudiwa siku ya 10 hadi 14.
nafasi ya kupanda ni mita 1 kati ya mstario na mstari mmea na mmea ni mita 0.70 inategemea na aina unayotaka kupanda.
MBOLEA NA KUPALILIA
Mihogo ni moja ya mazao ambayo aitegemei sana mbolea lakini shamba la mihogo unaweza kutumia mbolea ya samadi au ukatumia NPK wakati wa kupanda.
kiasi cha NPK kinacho itajika ni kilo 120 kwa hekta lakini ukatumia kilo 60 wakati wa kupanda na kurudia tena kilo 60 baada ya miezi miwili.
Unatakiwa kupalilia mapema ili kuepusha msongamano wa magugu shambani, unapalili mwezi 1 au 2 baada ya kupanda na kurudia tena pale unapo ona magugu yameota kwa wingi shambani kwako. unawaweza kupalilia kwa kutumia jembe la mkono au kwa kutumia chemikali kwa watu wenye mashamba makubwa
KUVUNA
Mihogo inatakiwa kuvunwa pale inapokua imekomaa vizuri, na mda wa kuvuna ni miezi 10 had 12 inategemea na aina ambayo umetumia.
mihogo inavunwa kwa kufukua chini na kuchukua miziz yake ndi mihogo yenyewe. na wakati wa kuvuna unatakiwa kua makini ili kuepushwa kuvunja mihogo na kuiacha chini ya ardhi.
WADUDU NA MAGONJWA
mihogo ni moja kati ya mazao ambayo hayasumbuliwi sana na wadudu na magonjwa, ila unatakiwa kutumia dawa za kuua wadudu pale unapohisi wadudu wamevamia shamba lako. unaweza kutumia sawa kama vile malathon au servin.
napale unapoona inapadilika kua yanjano au majani kudondoka unaweza kuspray demothate spray kwa wiki 2 had 4
unaweza kuangalia ufugaji bora wa nguruwe kwa kubonyeza hapa
0 Comments