KILIMO BORA CHA NANASI



   
UTANGULIZI
Nanasi ni moja kati ya matundwa pendwa sana duniani, hiyo ni kutokana na utamu wake,nanasi huweza kuliwa kwa kukuwata vipande, kwa kupikwa au kwa kutengenezwa kama juisi, na pia nanasi ni chanzo kizuri za vitamin A na B.
Kwa hapa tanzania nanasi usitawi sana katika mikoa ya Pwani, Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza.

HALI YA HEWA
Nanasi usitawi vizuri sana kwenye maeneo yenye muinuko kuanzia mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari lakini pia mananasi  yaliyo limwa kwa usawa wa mita 1300-1750 hufaa zaidi kwa kusindikwa  chini ya hapo hufaa zaidi kwa kuliwa moja kwa moja

jotolidi- nanasi husitawi vizuri zaidi kwenye maeneo yenye jotolidi ya nyuzi joto 18-35.

udongo-pia usatawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye uchachu (PH) 5.5 had 6.0 udongo uwe tifutifu na wenye unyevu nyevu wa kutosha na usio tuamisha maji.


KUANDAA SHAMBA
     Samba la kupanda mananasi linatakiwa kuandaliwa mapema uchafu utolewe na litifuliwe vizuri ili kuwezesha mizizi kuweza kupenya vizuri kwenye udongo.na pia unaweza kuweka mbolea ya kuku kiasi cha tani 10 had 15 kwa heka moja. 

KUPANDA
  chimba mashimo vizuri yenye urefu wa sm 3 kwenda chini
Chagua machipukizi mazuri na yalio madogo kwaajili ya kupanda na yawekwe sehemu yenye kivuli kwa mda wa siku 3.
panda umbali wa sm 60 had 80 kati ya mstari na mstari na sm 30 kati ya mche hadi mche ,weka dawa aina ya diaziron dakika 25 kabla ya kupanda ili kuzuia magonjwa na wadudu
kwa heka moja unaitajika kua na miche 50,000

MBOLEA
tumia mbolea ya kupandia NPK kwa kuweka gram 50 had 70 kwa kila shimo na pia unaweza kurudia kwa mda wa miezi 3 na kurudia tena kwa mda wa miezi 3.

KUVUNA
Mananasi huchukua mda mpaka kufikia wakati wa kuvuna, kawaida mananasi uchukua miezi 12 hadi 15 hadi kuto maua na uchukua tena miezi 5 kutoka mda yanapotoa maua mpaka kukomaa.
mananasi uvunwa pale yanapo komaa kabisa na majani yake kukauka na kua na rangi ya dhahabu.

na wakulima wengine hutumia chemicali aina ya ethanol@100 PPM wakati wa kutoa maua ili kuwezesha maua kutoka vizuri.


MATUMIZI
Kama nilivo sema hawali nanasii moja kati ya matundwa pendwa sana na hua na matumizi mengi kama ifuatavo
  • chanzo cha vitamin A na B 
  • utumika katungeneza mafuta
  • utumika kurainisha ngozi 
  • utumika kutengeneza mafuta ya kujipaka
  • dawa ya magonjwa
  • utumika kutengeneza juis
na matumizi mengine mengi

pata elimu juu ya vitu mbalimbali kuhusiana na kilimo na ufugaji ka kubonyeza hapa


No comments