WADUDU WAHARIBIFU NA JINSI YA KUWADHIBITI SEHEMU YA 1

Maana ya visumbufu vya mazao
 Visumbufu vya mazao ni kitu chochote iwe  mnyama au zao linalo letausumbufu  kwa mmea pandwa. Visumbufu hivyo hua ni kama ifuatavyo.
  • wadudu

  • magonjwa
  • magugu
  • vimelea
  • wanyama
  • ndege

  • minyoo 
Madhara yanayo sababishwa na visumbufu
Husababisha madhao kupunguza uzarishaji shambani na ubora, muda mwingine viharibifu husababisha madhara machache katika uzalishaji hayo madhara kwa kitaalam huitwa uneconomic damage lakini wakati mwingine wakati mwingine husababisha madhara makubwa sana shambani na madhara hayo kwa kitaalam huitwa economic damage hivyo visumbufu hivyo huitaji kuzuiliwa.pale visumbufu vinapo sababisha madhara machache shambani unashauliwa kuto tumia njia za gharama ili kuvizuia.

madhara ya  moja kwa moja ya wadudu waharibifu katika mazao
  1. kula majani ya mimea
  2. kunyea majani
  3. kutafuna mashina
  4. kula mizizi
  5. kula maua na matunda
  6. kufyonza maji ya mmea

unaweza kujifunza mambo mengi kwa kutizama machapisho mengine

madhara yasiyo yamoja kwa moja  ya wadudu waharibifu katika mazao
  1. husababisha mazao kukua taratibu sana
  2. husababisha mazao yanayo vunwa kua na contamination  na kinyesi cha wadudu na wadudu walio kufa
  3. hupunguza ubora wa mazao
 jinsi ya kudhibiti wadudu waharibifu shambani
kama tulivo ona hapo hawali kua wadudu wanaweza kuleta madhara shambani hivyo ni muhimu sana kudhibiti kabla hawajaleata madhara shambani, na kunanjia mbili ya kudhibiti wadudu waharibifu
  • kwa kutumia kemikali (insectisides)
  • kwa kutotumia kemikali

 JINSI YA KUZUIA WADUDU WAHARIBIFU BILA KUTUMIA KEMIKALI

  sheria na kufungiwa kwa mazao, kila nchi in orodha ya wadudu waharibifu ambao hawapatikani nchini humo, kwa hiyo wadudu hatari ambao hawapatikani nchini nilazima wazuie kwa kutumia sheria kwa mfano katazo la kuingiza mazao ambayo yanasadikika kua na wadudu hao mazao yote yanayo ingizwa hukaguliwa ili kubaini kama hayana wadudu waharibifu.
 Pia kama kuna mazao ambayo yanachochea upatikanaji wa wadudu waharibifu flani hukatazwa kulimwa kwa eneo husika mfano Tanzania haruhusiwi kulima pamba katika eneo ya kusini ili kuzuia minyoo wekundu kutoka zambia na mozambique.
 
 Njia ya kitamaduni, pia unaweza kuzuia wadudu waharibifu kitamaduni kwa njia hizi
  • kutumia aina ambazo hazipati magonjwa kirahisi(resistance varities)
  • njia ya kuzungusha mazao (crop rotation)
  • kuondoa majani yaliyo athirika
  • usafi wa shamba
  • kupanda kwa wakati
  • kuvuna kwa wakati
  • kutumia nafasi sahihi
nitumaini langu umejifunza mengi mpaka kufikia hapa hivyo usisite kua na mimi wakati mwingine ili kujua zaidi.

Post a Comment

0 Comments