WADUDU WAHARIBIFU NA JINSI YA KUWADHIBITI SEHEMU YA 2

Kama ulikosa sehemu ya kwanza ya somo hili na ulitamani sana kuisoma unaweza kubofya HAPA

Kwa wale ambao tupo pamoja hii ni sehemu ambayo tuliishia wakati ulio pita.


 JINSI YA KUZUIA WADUDU WAHARIBIFU BILA KUTUMIA KEMIKALI

  sheria na kufungiwa kwa mazao, kila nchi in orodha ya wadudu waharibifu ambao hawapatikani nchini humo, kwa hiyo wadudu hatari ambao hawapatikani nchini nilazima wazuie kwa kutumia sheria kwa mfano katazo la kuingiza mazao ambayo yanasadikika kua na wadudu hao mazao yote yanayo ingizwa hukaguliwa ili kubaini kama hayana wadudu waharibifu.
 Pia kama kuna mazao ambayo yanachochea upatikanaji wa wadudu waharibifu flani hukatazwa kulimwa kwa eneo husika mfano Tanzania haruhusiwi kulima pamba katika eneo ya kusini ili kuzuia minyoo wekundu kutoka zambia na mozambique.
 
(a) Njia ya kitamaduni, pia unaweza kuzuia wadudu waharibifu kitamaduni kwa njia hizi
  • kutumia aina ambazo hazipati magonjwa kirahisi(resistance varities)
  • njia ya kuzungusha mazao (crop rotation)
  • kuondoa majani yaliyo athirika
  • usafi wa shamba
  • kupanda kwa wakati
  • kuvuna kwa wakati
  • kutumia nafasi sahihi
 
(b) huifadhi na utunzaji mzuri wa mazao, hii pia inachangia sana katika kuzuia wadudu wa haribifu kusambaa au kueneo katika shamba lako au kutoka katika mmea ulio athirika kwenda kwa mmea usio athiriwa., njia hii nikama ifuatavyo.
  • kuondoa mimea iliyo athiriwa shambani
  • mzunguko wa mazao
  • kupanda mapema
  • kupanda mimea inayo kinzana na aina flani ya mazao
  • kupanda katika wakati stahiki 
  • kuchangua mbegu ambazo zimedhibitishwa na zisizo  na maambukizi yoyote.
(c)kutumia njia ya kibailogoa, njia ya kibailogia hutumika kwa kutumia mawakala mabao ni viumbe hai wasio na madhara katika mmea yaani viumbe ambavyo hushambulia wadudu flani ambao ni waalibifu mfano wa viumbe hivyo ni Nyigu. na pia njia ya kibaiologia hujumuisha kupanda mazao ambayo hua na athiri ya usumu (pestiside) ndani yake mfano black jack huzuia wadudu wengi.


 (d) kwa kutumia njia shirirkisi (integrated pest management), hii ni njia inayotumika kupunguza kasi ya wadudu shambani kwa kwa kushirikisha njia tofauti tofauti  njia ya kibailogia, yakitamaduni, kemikali na njia zingine.
je unaitaji kufahamu mengi kuhusu kilimo na ufugaji usisite kubofya hapa
 
 JINSI YA KUZUIA WADUDU WAHARIBIFU KWA KUTUMIA KEMIKALI
 Kemikali zinazo tumika kuua wadudu waharibifu huitwa pesticide, kemikali hizo hua katika mifumo tofauti tofauti yaan kimiminika, gasi na poda.
 
MASHARTI YA KUTUMIA KEMIKALI ZA KUUA WADUDU(PESTCIDE)
  • Tumia dozi stahiki
  • tumia kemikali wakati ambao wadudu hawajaathiri sana shambani
  • weka dawa katika sehemu husika
  • tumia njia ya kuweka ambayo nisahii zaidi
  • kemikali nyingi ni sumu kwa wanyama na binadamu hivyo soma maelekezo nazingatia umakini wakati wakutumia
  • tunza kemikali sehemu safi na salama na kwa umakini
  • usivute sigara, kula wala kunywa wakati wa kutumia kemikali au ukishika kemikali bila kunawa kwa maji safi na sabuni.
  • epuka kemikali kuingia machoni, masikioni au kugusana na ngozi
  • baada ya kupulizia kemikali fua nguo zote ulizo tumia
  • pia tunza vizuri makopo ambayo yalitumika kuweka kemikali hizo 
 JINSI YA KUDHIBITI WADUDU WAISHIO KWENYE UDONGO
  Wadudu wengine huishi ndani ya udongo, na wadudu hao wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali zinazo itwa FUMIGANTS, Na fumigants unaweza kuiweka kwenye udongo kwakutumia pamb ya mkono, na inakua katika mfumo wa kimiminika au poda na baadae baada ya kuwekwa kwenye udongo hubadilika nakua katika mfumo wa gasi.
 zingatia kufunika eneo lililo wekewa kemikali ili kuzuia kemikali hizo kuondoka na upepo, na baada  ya mda unaweza kufunua na baadae kuanza kutumia eneo hilo.
 
nitumaini langu umejifunza kitu mpaka hapo tulipo fikia, hivyo usisite kuungana na mimi wakati mwingine ili kujifunza kitu kingine tena

ASANTENI...

Post a Comment

0 Comments