KILIMO BORA CHA MIGOMBA/NDIZI



UTANGULIZI
  Migomba huzaa zao ambalo huitwa ndizi, ndizi huliwa kwa kupikwa, kukaushwa, kuvundikwa au kwa kusangwa na kutengeneza unga wake.

HALI YA HEWA NA UDONGO
  Migomba hustawi vizuri  kwenye maeneo joto kati ya 25oC hadi 30oC na huitaji mvua 1000mm kwa mwaka, pia uitaji udongo ulio na rutuba na unyevu wa kutosha. katika hali tajwa hapo juu mgomba unauwezo wa kuzaa matunda kati ya miezi 8 hadi 12 baada ya kuhamishia shambani(transprating). katika  hali ambayo sio nzuri migomba inaweza kuchukua mda kidogo kuzaa hadi miezi 18. kwa hapa Tanzania migomba hustawi vizuri katika mikoa ya moshi, kagera na mbeya

AINA 
kuna aina mbili za ndizi
  • aina ya dessert 
  • aina ya plantain
Dessert-  Hii ni aina ambayo inaliwa baada ya kuiva yaani sio ya kupika mfano mshale, bukoba,  kisukari, jamaica na mtwika
plantain- hii ni aina ambayo ni nzuri zaidi kwa kupika mfano mzuzu na mkono wa tembo

KUPANDA
  Migomba mara nyingi haiitaji mbegu kupanda, hupandwa kwa kutumia sucker, hivi ni ni vimigomba vidogo ambavyo vinakua pembeni, inatakiwa kuchukua watoto wenye urefu wa 1/2  na ikiwa na upana 15cm hadi 25cm na zingatia kuchagua mimea yenye afya.

migomba  hupandwa mwanzoni mwa masika, chagua sucker katika aina unayo itaji.
chimba mashimo yenye urefu na upana  wa 60cm, mashimo yanatakiwa kua na umbali ufatao
  • aina fupi 3m x 3m
  • aina ya kati 3m x 4m
  • aina ndefu 4m x 4m
 kama kuna histori ya kua na na wadudu aina ya weevel tibu kwa kutumia diedrin kabla ya kupanda.

MBOLEA
Weka vijiko vikubwa 5 hadi 7 ya mbolea ya CAN kwa kila mmea kwa kila mwaka, anza kuweka mbolea kuanzia mwaka wa pili kutoka kupanda, zungushia mboelea kwenye mmea kwa umbali wa 4cm kutoka kwenye mmea.

KUPALILIA, KUNGOLEA NA KUFUNIKIA
   Shamba la migomba hutakiwa kua safi na kutokua na magugu mda wote, unapo palilia zingatia kutoathiri mizizi ya mmea ambayo hukua umbali wa 15cm kutoka juu ya ardhi.
ili kuongeza ukubwa wa ndizi na ubora punguza mashina na kubakiza shina moja katika kila mgomba.
  mashina ambayo hukwatwa wakati wa kupuynguzia yanaweza kutumika kufunikia mmea, kufunikia husaidia kupunguza mmommonyoko wa udongo, kuhifadhi unyevu na pia husaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa magugu.

KUWEKEA MTI WA KUZUIA
Pale mgomba unapobeba mkungu mzito na mkubwa na muhimu kuwekea mti wa kuegeshea ili kuusapport mgomba.

MAGONJWA NA WADUDU
wadudu wakuu katika migomba ni
  • nematode
  • weevel wa migomba
Magonjwa ya migomba na ndizi ni
ugonjwa wa panama

unaweza kuwasiliana na mtaalamu moja kwa moja ili kufahamu zaidi jinsi ya kukabiliana na wadudu na magonjwa kwa kubofya HAPA

KUVUNA
kata shina la mgomba pale ndizi zinapo komaa na kabla hazijawa za njano, pia   baada ya kuvuna kata shina kubwa na yape nafasi mashina yanayo anza kuota.

nitumaini langu umejifunza usisite kutembelea UKURASA WETU kila siku kwa kujifunza mengi zaidi

Post a Comment

0 Comments