SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WAVUVI HARAMU

 Serikal ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli imeapa
kutowafumbia macho viongozi au watu wanaojihusisha na shughuli za uvuvi
wa kutumia zana haramu zilizopigwa marufuku.

Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipokuwa akiteketeza
zana za uvuvvi haramu zilizomakatwa hivi karibuni katika Wilaya za
Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.
Aliongeza kwa kusema kuwa hakuna atakayesalimika katika sakata hilo endapo tu akibainika kutumia zana haramu za uvuvi.Ameongeza
kuwa Serikali ina dhamira kubwa na wavuvi katka ufanyaji wa shughuli
zao na ndio maana imeamua kupiga marufuku zana zote haramu kwa lengo la
kusaidia kizazi kijacho ili nacho kije kinufaike na raslimali za Taifa
hili.

,"Hivyo idara ya uvuvi kamwe hautomfumbia macho kiongozi
yeyote yule ambaye anajishughulisha na biashara hiyo kwa kigezo cha kuwa
yeye ni kiongozi.“Kwa yule atakayebainika kuwa ni kiongozi au mtu
mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu ambao Serikali inatumia
fedha nyingi kukabiliana nao basi cha mtema kunde atakiona juu yake
kwani zana zake zitachomwa,faini na yeye kuchukuliwa hatua za kisheria,”
amesema.

Aidha Ulega amewataka wavuvi kuendelea kusalimisha
zana haramu kabla ya kukumbwa na dhahma kubwa itakayowapeleka mahali
pabaya zaidi ya hali ya sasa jinsi ilivyo.Pia amewahakikishia
upatikanaji wa zana zinazohitajika mapema kwani tayari wamesha anza
kupokea maombi mengi ya mashirika yanayohitaji kusambaza zana halali
katika nchi yetu kwa madhumuni ya kuokoa rasilimali za majini zilizokuwa
zikipatwa na shinda nyingi kutoka kwa wavuvui wasiokuwa waaminifu.

Kwa
upande wake Msimamizi wa Kamati Maalumu ya kuthibiti na kupambana na
uvuvi haramu Kanda ya Simiyu na Mwanza, Nchama Marwa amemuhakikishia
Naibu Waziri kuwa hakuna uonevu wa aina yeyote ile unaofanywa na kikosi
hicho kuhusu kuwawajibisha wale wanaoendelea na shughuli hiyo kwa
kujifisha .Ameongeza kuwa kuna wavuvi ambao wanasalimisha na wengine
bado wanaendelea kuvua kwa kujifisha laniki ni lazima tu watawakamata na
sheria ya uvuvi itafuata mkondo wake bila kinyongo wala uonevu wa aina
yeyote ile.

Aidha kiongozi huyo wa kikosi maalumu aliwasilisha
taarifa kuhusu utekelezaji wa kazi zao kwa Naibu Waziri na kumweleza
kuwa kuwa mpaka sasa wamekamata nyavu haramu za makila 33121,nyavu za
dagaa175,makokoro ya sangara119.Pia nyavu za timba 3,sangara wabichi
kilo 1071,sangara kayabo3463, watu hao waliokamatwa na kikosi kazi
wametozwa faini kulingana na kile walichokamatwa nacho na kufikia kiasi
cha Sh.milioni 767.

Naye Boniface Mkama Mkazi wa Nyamikoma
wilayani Busega ameipongeza Serikali kwa kuwasaidia na vitendo vya
kinyama vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wavuvi wenzao.Hivyo ameiomba kuwawaishia tu zana sahihi ili waendelea na shughuli zao za kila siku za uvuvi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akishiriki shughuli ya
kuteketeza zana haramu za uvuvvi zilizokamatwa hivi karibuni katika
wilaya za Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.

Mkuu wa wilaya za Busega,Tano Seif Mwera akishiriki shughuli  ya
kutekeza  zana haramu za  uvuvi zilizomakatwa hivi karibuni katika
wilaya yake.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akizungumzana na
wavuvi kua mtu yeyote anaejihusisha na uvuvi
haramu zana zake zitateketezwa na yeye atachukuliwa hatua za
kisheria

No comments