HALMASHAURI MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akivaa viatu vilivyotengenezwa
katika Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi kilichopo Senani Wilayani
Maswa wakati wa Ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa pamoja na
viongozi wakuu wa Wilaya ya Maswa wakielekea katika Kiwanda kidogo cha
kutengeneza bidhaa Ngozi katika Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati
wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akifuatilia hatua
mbalimbali za utengenzaji wa viatu vya ngozi kwenye kiwanda cha
kutengeneza bidhaa ngozi kilichopo Kijiji cha Senani kata ya Senani
wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya
wananchi wa Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa, wakati alipotembelea
eneo ambalo kitajengwa kiwanda kidogo cha kutengeneza ungalishe
kitakachomikiwa na shule za Msingi 30 za Maswa,wakati wa ziara yake ya
kutembelea viwanda vidogo wilayani humo.
Halmashauri
ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeshauriwa kuwekeza katika kiwanda
cha kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu, mikoba na mikanda
kinachomilikiwa na kikundi cha Usindikaji Ngozi Senani kilicho kata ya
Senani wilayani Maswa, ili kuongeza thamani ya ngozi zitokanazo na
mifugo.
Ushauri
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa
ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo katika wilaya MASWA.
Mtaka
amesema katika kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania
ya Viwanda , Halmashauri ya Maswa inapaswa kuwekeza katika viwanda
vinavyoanzishwa na vikundi ili kuviwezesha katika upatikanaji wa
malighafi ya kutosha, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo pamoja na
kilimo ili viwanda hivyo viweze kuzalisha kwa tija.
“Tungehitaji
kuwa mkoa ambao utawekeza sana katika viwanda vidogo na ndiyo maana
tulianza dhana ya Wilaya moja bidhaa moja kiwanda kimoja na sasa
tunakwenda kwenye Kijiji Kimoja Bidhaa Moja Kiwanda kimoja; tunataka
kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya Mkoa” alisema Mtaka.Aidha,
ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wanakikundi kuweka mifumo mizuri ya
kutengeneza soko la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni
pamoja na kuuza katika minada yote ya wilaya hiyo na kuimarisha soko la
nje.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,
Dkt.Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri itahakikisha kiwanda hicho
kinapata malighafi ya kutosha ambapo amebainisha kuwa Halmashauri
imeingia mkataba na Chuo cha DIT Mwanza kuhakikisha kuwa inazalisha
malighafi(ngozi) kwa wakati kwa ajili ya kiwanda hicho.
Akiwa
Malampaka ambapo alitembelea Mradi wa Ghala na Mashine ya kukoboa mpunga
na kupanga madaraja, Mtaka amekipongeza Chama cha Ushirika Bumala AMCOS
kwa kuanzisha kiwanda, huku akiwataka wananchi wa eneo hilo kujiandaa
kiushindani katika biashara, kwa kuwa hivi karibuni Serikali inatarajia
kuanza ujenzi wa bandari ya nchi kavu itakayoenda sambamba na ujenzi wa
Reli ya Kisasa(Standard Gauge).
“Ni
lazima mjiandae kiushindani katika biashara, miaka mitatu ijayo katika
Mipango ya Serikali Malampaka haitakuwa kama ilivyo, hapa ni mahali
ambapo Standard Gauge ikianza bidhaa zitakuwa zikisafirishwa kwa wingi;
nimeshaongea na Mkurugenzi kuwa eneo hili lipimwe na Halmashauri imiliki
eneo la uwekezaji” alisisitiza Mtaka.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka alitembelea
eneo la ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza ungalishe katika Kijiji cha
Njiapanda, ambacho kitamilikiwa na shule 30 za Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, kinachoanzishwa kwa lengo la kuongeza kipato cha shule na
halmashauri, kutoa ajira kwa wananchi na kuboresha lishe za watu.
Akitoa
taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Maswa,
Mwl. Mabeyo Bujimu amesema shule za msingi 30 wilayani humo zitanufaika
kwa kulima viazi lishe na kukiuzia kiwanda hicho kama malighafi pamoja
na kuuza bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda.
Huu ni
mwanzo wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ambayo
amepanga kutembelea viwanda vidogo vilivyopo katika wilaya zote za mkoa
huo.
Post a Comment