CHAMA CHA WAFUGA MBWA KUZINDULIWA

 
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Kutetea Maslahi ya Wafugaji Mbwa unaotarajia kufanyika tarehe 3 Februari mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam  Mkurugenzi wa  taasisi hiyo, Dkt Sinare  Sinare (pichani kushoto)  amesema kuwa  uzinduzi una lengo la kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa , kuhamasisha ufugaji na umiliki bora wa mbwa unaojali maslahi ya mbwa kwa wamiliki.


“Uzinduzi wa Chama chetu una lengo la kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa ufugaji mbwa kwa usalama wao pamoja na kusimamia na kushauri kuhusu uzalishaji bora wa mbwa kwa wanachama, wadau na serikali”.


Dr. Sinare ameeleza kuwa katika uzinduzi huo, Jeshi la Polisi kikosi cha mbwa  wanatarajia kufanya maonesho ya kuonesha weledi wa mbwa wao katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Dr. Sinare amefafanua aina tano za uanachama ambazo ni Mwanachama wa kawaida ambao ni kwa ajili ya wamiliki wa mbwa, Mwanachama mshiriki ambae ni mtu au kampuni ambayo shughuli zinahusiana na ustawi wa mbwa, Mwanachama kampuni ambao ni kwa kampuni ambayo shughuli zake zinahusiana na matumizi au uzalishaji wa mbwa.


Nyingine ni uanachama utakaopewa mtu yeyote ambae kwa mawazo ya wanachama atasaidia kuendeleza na kutekeleza madhumuni ya TCAL na Mwanachama mgeni kwa ajili ya wageni ikiwemo watu wa kampuni ambazo sio wenyeji wa Tanzania. 


Dr. Sinare ameeleza kuwa ili kuwa mwanachama wa kundi lolote la uanachama utajaza fomu maalumu kwq ajili ya kujiandikisha kisha umtu atalipia shilingi laki moja  kama kiingilio na kupewa kitambulisho.

No comments