WAZIRI MKUU KUKUTANA NA WADAU WA PAMBA FEB 15-16,2018
WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa, ameitisha kikao cha wadau wa pamba nchini, ili kujadili namna bora ya kuongeza tija ya zao hilo.
Kikao
hicho kitakachofanyika jijini Mwanza Februari 15 hadi 16, 2018,
kinatarajiwa kuondoa sintofahamu iliyogubika sekta ya pamba, kuhusu
mustakabari wa kilimo cha mkataba kutokana na kusudio la Serikali
kuanzisha ununuzi wa pamba kwa njia ya mnada kupitia vyama vya
ushirika.
Hatua
hiyo imekuja siku chache baada ya kuonesha kusudio la kusitisha kilimo
cha mkataba, na uwezekano wa pamba kuuzwa kwa njia ya mnada.Kulingana
na taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba,
kikao hicho muhimu kimelenga kuondoa hali ya sintofahamu, juu ya kilimo
cha mkataba na uuzwaji wa zao hilo kwa njia ya mnada.
Kusudio
hilo la Serikali la kuuzwa pamba kwa njia yamnada, limeonekana kuleta
wasiwasi kwa makampuni yaliyowekeza kwenye sekta hiyo muhimu katika
uchumi wa nchi.
Mkoa
wa Tabora Agrey Mwanri akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo Charles
Tizeba kabla ya kuanza ziara ya kuona utekelezaji wa kilimo cha Pamba na
uzalishaji wa mbegu bora za pamba za UKM08 Msimu 2017/2018 uliofanyika
jana tarehe 04 feb 2018.
Afisa Kilimo wilaya ya Igunga Erasto Konga akiwasilisha taarifa ya wilaya kwa Waziri wa Kilimo.
Akiwa
ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa mkoa huo Agrey Mwanri, Waziri
Tizeba pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakulima na
kugundua kuwa bado elimu ya unyunyiziaji dawa haijakaa sawa.
Na hapa ikawa nafasi ya kutoa darasa upya kwa mkulima huyu.
"Tunakwenda
kujadiliana nao wanunuzi hawa wa pamba, hususani walioingia kilimo cha
mkataba. Asilimia 40 ya Watanzania wote wanategemea uchumi wao kupitia
pamba," alisema Waziri Tizeba.Alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwa ziara ya kukagua mafanikio ya zao la pamba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Waziri
Tizeba akitizama namna mkulima wa pamba ambaye ni Mwalimu wa Shule ya
msingi , Bw. Faustine Francis anavyo nyunyizia dawa.
Afisa ugani Kata ya Mbutu Iddi Uledi akitoa maelezo kwa Waziri Tizeba.
Shamba la zao la Pamba wilayani Igunga.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Gaki Investment inayojihusisha na ununuzi wa pamba,
Gasper Gaki, alisema: “Tunakingoja kwa hamu sana kikao hiki na Waziri
Mkuu, naamini kitakuwa na mafanikio.”
Katika
hatua nyingine, Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo alisifu juhudi za
kilimo cha pamba, ambapo Mkoa wa Tabora umevuka lengo lake la uzalishaji
zao hilo.
Zaidi
ya kilo milioni 187 zinatarajiwa kuvunwa mwaka huu mkoani hapa, kwamba
kasi ya kilimo hicho inaleta tija kiuchumi na pato la taifa.
Idadi hiyo ni kiwango cha juu, kuliko matarajio ya awali ya kuvuna zaidi ya kilo milioni 136 za pamba, msimu huu.
Waziri Tizeba alisema kuwa, takribani sh. Bilioni 50 zinahitajika kwa ajili ya manunuzi ya dawa za kuuwa vijidudu vya mazao.
"Haijawahi
kutokea. Tumepata mafanikio makubwa sana ya kilimo cha pamba mwaka huu.
Viongozi na wananchi hongereni sana, mtauza kwa bei nzuri.
Waziri
huyo aliagiza maofisa kilimo 30 waliopo wizarani kwake, na wengine 30
kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru kuanzia wiki ijayo, kusambazwa
Mikoa ya Tabora, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga, alisisitiza wakulima wa zao hilo
kupulizia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.
"Ukipuliza
dawa mchana hautauwa hawa wadudu. Muda wa kupuliza ni asubuhi, mwisho
saa 3:00 asubuhi, baadaye tena jioni," alisema Mtunga.
Awali,
Ofisa Kilimo Mkoa wa Tabora alizitaja wilaya nyingine za mkoa huo na
idadi ya uzalishaji kilo kwenye mabano kuwa ni Kaliua (kilo 11,554,000).
Nzega (kilo 16,300,000), Urambo (4,307,000) na Uyui inayotarajia kuzalisha zaidi ya kilo milioni 6.81.
Post a Comment