KISHAPU KUFIKIA LENGO LA ZAIDI YA ASILIMIA 75 ZOEZI LA KUPIGA CHAPA NG'OMBE 225,131
Mkuu
wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Dk.
Alphonce Bagambabyaki akishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe.
Wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katiia kijiji cha Wishiteleja kata ya Mondo.
Moja wa ng’ombe akiwa tayari amepigwa chapa katika sehemu ya mguu.
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Halmashauri
ya wilaya ya Kishapu imeweza kupiga chapa jumla ya ng’ombe 225,131
katika zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo linalofanyika katika kata
zote zenye wafugaji wilayani humo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga amesema kuwa zoezi hilo
ni endelevu na limeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo
kwa changamoto kadhaa.
Alisema
zoezi hilo ni agizo kutoka serikalini na kinachofanyika ni kulitekeleza
kwa kiwango kinachotakiwa na kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo
mbalimbali katika kata za wilaya hiyo.
“Zoezi
la upigaji chapa ng’ombe tulilipokea na tumeweza kulitekeleza ingawa
zipo changamoto mbalimbali zikiwemo baadhi ya maeneo kutokuwepo kwa
wafugaji tumefanikiwa kuifikia mifugo hiyo,” alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dk.
Alphonce Bagambabyaki alisema Wilaya imeweza kufikia lengo hilo kwa
zaidi ya asilimia 75 ya lengo ambalo ni ng’ombe laki tatu.
Alisema
vijiji lengwa vyote 125 vimeweza kufikiwa na ingawa zipo baadhi ya
changamoto kama imani potofu kwa baadhi wafugaji kuwa huenda
wakachukuliwa mifugo yao pindi wanapoifikisha vituo vya zoezi la upigaji
chapa.
Zoezi
hilo lilianza rasmi Oktoba 20 mwaka jana ambapo lilizinduliwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba linataka mifugo yote nchini
kutambuliwa kwa kutumia chapa chini ya sheria ya utambuzi namba 12 ya
mwaka 2010.
Aidha,
zoezi hilo limekuwa likitekelezwa na wataalamu wa mifugo kutoka
wilayani makao makuu wakishirikiana na wataalamu wa kata na vijiji
mbalimbali ili kuhakikisha limekwenda kwa ufanisi.
Wakati
akizindua zoezi hilo Mh. Taraba alibainisha kuwa zoezi la utambuzi,
usajili na ufuatiliaji wa ng’ombe kwa kutumia chapa litapunguza
changamoto zinazowakabili wafugaji.
Alibainisha
kuwa Kishapu ni miongoni mwa wilaya ambazo baadhi ya wafugaji wake
wanakabiliwa na matatizo yakiwemo wizi wa mifugo katika unaoweza kutokea
katika maeneo mbalimbali nchini.
Pia
linasaidia kupunguza migogoro migogoro baina ya wakulima na wafugaji
wanaokuwa wanahama hama bila kufuata utaratibu maalumu kwa lengo la
kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao.
Post a Comment